[wanabidii] BURAQ AU CHOPPER?

Sunday, November 16, 2014
BURAQ AU CHOPPER?
(
Dkt.Muhammed Seif Khatib)

Kulingana na imani ya dini ya Kiisilamu inaaminika kuwa kulitokea miujiza
kwa Mtume wao Muhammad.Ilikuwa katika karne ya kumi na saba huko
Arabuni ilitokea safari ya ghafla ya usiku mmoja uitwao usiku wa Miraji.Usiku
Muhammad alikuwa amelala huko Makka.Usingizini akatokea malaika Jibril
aliyetumwa na Mwenyezi Mungu kwa Nabii Muhammad.Jibril akamtaka huyu
Muhammad stoke nje haraka kuna safari muhimu ya kutekelezwa.Huko nje
alikuwpo buraq.Huyu ni mnyama anayefanana na farasi.Ni mweupe lakini
ana mbawa mbili kubwa katika mapaja yake ya miguu ya mbele.Muhammad
akaongozwa ampande mnyama huyo ili ampeleke safari muhimu na maalumu.
Buraq akapaa angani kwa mwendo wa kasi katika usiku huo mmoja.Huko
katika mbingu ya kwanza alionana na Nabii Adam.Alipofika mbingu ya pili
wakakutana na Yesu au Nabii Issa.Alipofika mbingu ya Sita akakutana na
Nabii Mussa na katika mbingu ya saba akakutana na Nabii Ibrahim.Alipofika
mbingu ya tisa akaoneshwa peponi, jahanamu na kuzimu.Aidha pia inaaminika
kuwa alipokuwa huko aliwaombea wafuasi wake wa dini ya Kiisilamu
tahafifu ya idadi ya sala.Mwisilamu alitakiwa asali sala hamsini kwa siku lakini
yeye aliwaombea idadi hiyo ipunguwe ziwe tano kwa siku.Ombi lake lilikubaliwa.
Tokea siku hiyo hadi leo Waisilamu wanasali sala tano kwa siku ni lazima au
wenyewe huita faradhi siyo suna.Mtume Muhammad alirudi duniani usiku ule
ule na kushukia katika hekalu huko Yeruselem.Inaaminika kuwa hata Nabii
Ibrahim wakati wake akipanda huyo buraq kutoka Makka kwenda Syria
kwa mkewe aitwaye Sira. Kwa mnasaba huu baadhi ya mashirika ya ndege
ya nchi za Kiisilamu yalitumia jina la mnyama huyu wa ajabu na miujiza aitwaye
buraq.Kulikuwa na Buraq Airline ya Libya au Buraq Airline of Indonesia.La
msingi la kukumbuka ni kuwa buraq ni mnyama aliyetumiwa na baadhi ya
Manabii.
Tumeona viroja na vituko vya baadhi ya vyama vya upinzani badala ya
kutangaza na kueneza sera na itikadi zao wanaendesha Opresheni Futa
CCM.Nao wamejaribu kutafuta buraq ili wapaye mbinguni wakaombe
huko juu kwa Allah ili CCM isiwepo Tanzania. Wangependa na wao kama
Muhammed wakutane kwanza na Mitume hiyo wakiwemo Adam,Issa,Mussa,
na Ibrahim.Wapinzani nia yao waruhusiwe waingiye wao Ikulu.Ni bahati
mbaya tamaa yao kumpata buraq ili awafikishe mpaka mbingu ya tisa
ikagonga mwamba.Wameamua wakodi helkopta (chopper).Helkopter inaweza
kuruka angani kwa kuondokea popote kama buraq.Helkopta inaweza kuruka
na ikiwa angani inaweza ikenda nyuma,mbele,pembeni au hata kuzunguka
ilipo bila shida kama buraq.Buraq imeipiku helkopta kwa vile imeweza kuruka
hadi mbingu ya tisa wakati helkopta hata mbingu ya kwanza haifiki.Buraq
ameruka na kusafiri usiku wa bila taa na kukamilisha kazi yote kwa usiku
mmoja.Helkopta isingeruka usiku na hata kufika huko juu katika mbingu
ya tisa.
Kwa tofauti hiyo chopper ya upinzani wataweza kuifut CCM?Fitina zao
hazifiki mbinguni ila zitishia chini ya mawingu ya mvua ambapo chopper inaweza kufika.Opresheni yao ya kuifuta CCM itkufa kifo cha mende kama
zilivyokufa ' opresheni sangara' pale CCM walipogeka samaki wa furu.Hivi
sasa wakati wanaruka na chopper na kusafiri kwa magari vitanzi kwa maelfu
vimetyarishwa huko vijijini,vitongojini na mitaani vinawasubiri.Mafundo
mafundo ya vitanzi yameshikwa na wanachama,wakereketwa na wapenzi
wa CCM wakisubiri shingo za wapinzani wazikabe na kuzinyonga hadi
watoke ngama. Siku ya tarehe 14.12.14 ni siku ya kusuka au kunyoa.Mauti
ya kisiasa yatawafika kwa sababu serekali ya CCM imewaletea Watanzania
mabadiliko makubwa katika maisha yao.Hao viongozi wa upinzani ni
miongoni ya watu wanaofaidika.Tuoneshwe mahekalo ya makaazi wanaoishi.
Tuoneshwe magari wanayopanda.Wabainishe akiba zao bengi.Waaje amali
na biashara zao pamoja na vitega uchimi vyao.
Wakati wapinzani wamo safarini kutekeleza azma yao ya kuifuta CCM kwa
kwa kutumia chopper na magari wakumbuke Chopper yao inatua na kuruka kwa
kutumia viwanja vilivyojengwa na serekali ya CCM.Wanatembeza magari yao
na kufunga viyoo huku ndani wakupuliziwa baridi nyepesi na kula mziki huku
magari yao yakiteleza katika barabara ya lami ilojengwa na serekali ya CCM. Wanasafiri
usiku na mchana kwa salama na amani yapaswa wakumbuke kuwa ni CCM ndiyo
muhimili wa usalama wao.
Miaka ishirini na tano sasa tokea CCM yenyewe bila kushuritishwa iruhusu kuwepo
kwa vyama vya upinzani.Nusu karne hiyo imetionesha kuwa chama cha CCM pale
mwanzo kwa sababu za ulimbukeni baadhi ya viongozi walitoka.Wengi sana walirudi
na kujutia waliyoyafanya.Chama cha upinzani mwaka 1992 kilianza kimoja.Hivi sasa
vimo vyama ishirini vya upinzani na vyengine vipo njiani. Migogoro iliyomo ndani ya
vyama vyao wanaihusisha na CCM.Vyma vina ukabila wa Uchaga na Upemba.Vyama
vina ubabe na udikteta. Vyama vina vina wizi na ubadhirifu.Matokeo yake vyama
vya upinzani vinasambaratika.Wakiona vyama vinakimbiwa vineelekeza vidole CCM.
Wale wanaotaka vyama vyao na kuunda vyengine hupewa majina ya ajabu.Huitwa
vibaraka,mapandikzi na kadhalika.
Mwaka huu Disemba 14 kutakuwa na uchaguzi wa serekali za mitaa,Vijiji na vitongoji.
Wapinzani walipata kipigo cha mbwa koko cha kukimbia na kufyata mkia kwa uchaguzi
wa mwaka 2009. Unakumbuka yaliyowakuta? CUF walipata Asilimia 3.8
(Wenye viti wa Vijiji)Asilimia 5.4(Wenyeviti wa mitaa)Asilimia 4.2 (Wenyeviti wa
Vitongoji).Nao CHADEMA walipata Asilimia 2.7(Wenyeviti wa vijiji)Asilimia 4.9 (Wenye
Viti wa mitaa) Asilimia 3.1 (Wenyeviti wa vitongoji).Ni yepi kwa motekeo ya chama
ambacho kinatakiwa kifutwe? CCM kimepata Asilimia 92 (Wenyeviti wa Vijiji)Asilimia
89.1 (Wenyeviti wa Mitaa) na Asilimia 91.0 (Wenyeviti wa Vitongoji). Na matokeo ya
jumla pamoja na wajumbe wengine ni CHADEMA ni asilimia 2.76; CUF ni Asilimia
3.94 na CCM kilishinda kwa Asilimia 91.71.Kwa matokeo haya yupo awezaye
kukifuta?Wakipata buraq wataweza lakini kwa chopper CCM haifutiki ng'o!


Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments