Re: [wanabidii] JAJI WARIOBA APECHE ALOLO

Monday, November 10, 2014


Ile budget ya media nadhani imeshaidhinishwa. Kuna vioja vingi tutavishuhudia kutoka kwa watu wasiokuwa na hoja.

2014-11-10 8:31 GMT+03:00 'Reuben Mwandumbya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Happy;
Unatumiwa vibaya Dadaa,kuwa mwangalifu na kama msomi tumika vizuri.
Unaposhauriwa/kuambiwa cha kufanya changanya na zako utakuwa ktk safe side.
Utaangamia Bibie,hapa hata mtoto akisoma makala hii atasema huyu jamaa katumwa au ni mshabiki wa upande flani na sio mwandishi wa habari,ukiacha makosa ya kimaadili ya kazi yako,makosa ya kiuandishi na kisarufi(gramma) ni mengi mno hata wengine tunapata shida kuamini kama hii inatoka kwa mwandishi wa habari mwenye angalau uzoefu kazini.Hii insonyesha wazi kwamba hushirikishi wenzako kwa kuwa ni kazi ya magam (character assassination)
 
Reuben
 



From: 'A S Kivamwo' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, November 9, 2014 6:34 PM

Subject: Re: [wanabidii] JAJI WARIOBA APECHE ALOLO

Teh teh teh!! eti Mkoa wa Ziwa Magharibi. Hans umenichekesha. Muganda na wewe Apeche Alolo mwenyewe...teh teh teh


On Sunday, November 9, 2014 5:44 PM, 'Fred Hans Kipamila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Je, huyu si yule aliyemfunda mwanamke mwingine kuwa kazi ya mwanamke ni kutafuta utundu wa kumuonyesha mwanaume kitandani?
 Huyu hawezi kuwa na mawazo mazuri hata kidogo ya kuwaambia wanaume kwa vile akili yake inamtuma zaidi kwenye kufikiri jinsi ya kufanya utundu kitandani kwa manufaa ya mwanaume wake.
Ukisoma jina lakwe kama anatoka mkoa wa ziwa magharibiwanakotoka wasomi hapa kwetu. Lakini napata shida kuamini kuwa huyu ni ziwa magharibi labda ni jina tu limeelekea huko.


From: Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, November 6, 2014 6:39 PM
Subject: Re: [wanabidii] JAJI WARIOBA APECHE ALOLO

Hivi ninyi bado mnapoteza muda wenu kumsoma Katabazi? Huyu anajikweza anadhani ataongezewa cheo. Apache alolo mwenyewe.
em

2014-11-06 7:30 GMT-05:00 Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com>:
Nimesoma hii makala kusema.kweli huyu.muandishi.amefanya kazi nzuri.saana kwa wanaomtuma. Nakubaliana nae kabisa kuwa.mzee Warioba kafirisika kisiasa na kifikira ila nisingependa kumuhukumu haraka bila.kumuhukumu mfirisika.namba moja aliempa hiyo kazi.
Lazima uwe na tatizo kidogo mpaka umteue mtu apache alolo kukifanyia kazi nyeti kes taifa hili. Na kwa mwendelezo.huo huyu mpumbavu anaeandika hii habari hakuweza kuiona hiyo mantiki anaongelea final.product hii ni higheet degree ya ujuha tulionayo na bahati.mbaya mijuha.kama.hii inapata.nafasi kwenye sehemu.zetu za kueleimisha jamii.
Jaji warioba na ufirisika wake wa nini vile sijui amebeba mawazo ya wananchi hana pendekezo pale hiyo tume ya wenye bongo.shibe inakaa kwenye vikao na kutoa inayofikiria yanawafaaa wananchi.
Ni kweli itapita lakini sijui huyu muandishi anasoma.anachoandika.au anaandika tu. Unawezaje kutonyesha live kuwa itapitishwa kibabe hiyo katiba na unataka tushangilie
On Nov 6, 2014 1:59 AM, "Oksana Spice" <worldngojobs@gmail.com> wrote:
JAJI WARIOBA APECHE ALOLO 
Na Happiness Katabazi
APECHE ALOLO ni Msemo ambao ulikuwa ni maarufu sana Katika Miaka ya 1990- 2000 Dar es Salaam. Msemo huu ulikuwa ukipendwa kutumiwa na 'watoto wa mjini' ambao walikuwa wakimaanisha Kuwa mtu Fulani HIvi sasa amefirisika kifedha, sera,Hana dira wala mwelekeo, Hana Mpango wowote. Hivyo ambaye alikuwa Hana Fedha,Hana sera walikuwa wakimuita mtu Huyo ni Apeche Alolo.
Hivi sasa watoto wa mjini wanatumia msemo huu Kuwa 'Fulani amefulia' , Shoka Moja Mbuyu chini, Choka Mbaya, kwishineiiii.Wana maanisha Mtu Fulani amefirisika kifedha, sera Hana dira wala mwelekeo na Hana lolote.
Nimelazimika kutumia neno Hilo kwasababu Oktoba 2 Mwaka huu ,ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza Dar es Salaam, kulizuka vagi hali iliyosababisha mdahalo wa kuzungumzia Katiba mpya uliokuwa imeandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuvunjika na mgeni Rasmi ambaye ni aliyekuwa Mwanyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba ambaye aliishia kukutwa na wakati mgumu na kudhalilika kutokana na vurugu hizo.
Kwa zaidi ya Miezi Tisa sasa aliyekuwa Jaji Warioba baada ya kumaliza kazi yake hiyo aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete, jina lake lilikuwa likibeba uzito wa juu Katika vyombo Vya Habari.
Jaji Warioba Mbele ya baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa wa upinzani alionekana ni mtu jasiri na anayeipenda sana nchi yake kuliko wana CCM wenzake na Kana Kwamba Jaji Warioba ndiyo aligeuka Kuwa ni Kama mtu aliyepewa jukumu la kuwafundisha Watanzania Kuwa Katiba mpya ni lazima iwe na vitu ambayo Tume yake ilivipendekeza na baadhi ya watu walimchukulia Warioba kama ndiyo msemaji wa wananchi ,Nyakanga wa kuwafunda watanzania ya jinsi Katiba mpya inayakiwa iweje, na kweli Warioba aliona anapendwa na watu wote na kusikilizwa na kwamba yeye ana akili sana kuliko Watanzania wote.
Jaji Warioba alisahau maneno ya mwanamuziki Mwandamizi wa Bendi ya FM Academia, Mule Mule FBI , aliyoyatoa Katika Wimbo wa Ndoa ya Kisasa uliopo Katika Albamu mpya ya Bendi hiyo inayojulikana kwa jina la CHUKI YA NINI, ambapo Mulemule asikika Katikati ya Wimbo huo Kuwa ( Ukijua Kutendwa basi na ujue na Kutendwa).
Warioba Mtani wangu siku zote alifikiri ataendelea Kupendwa na wananchi anaowahutubia Katika midahalo na akasahu Kuwa ipo siku anaweza Kutendwa na kweli watoto wa kihuni ' watoto wa Mbwa' , Novemba 2 mwaka huu, ndani ya Ukumbi wa Ubungo Plaza, walimtenda .
Sisi Watu wa Kabila la Wanyambo tunaotokea Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera , uhuni aliofanyiwa Warioba tunasema ' Warioba Bamkora Kantu'. Yaani wahuni wamemfanyizia .
Inaniwia vigumu kuamini kuwa kutokana na fezea ile aliyoipata Warioba sijui kama atakubali kirahisi tena mialiko ya kushiriki kwenye midahalo ya kutoa maoni ya kupinga Katiba Pendekezwa.Naona sasa amekoma .
Na kama anafikiri sawa sawa na anawashauri wazuri na hawamuonei haya kama mimi mtani wake, watakuwa na ujasiri kama wangu wa kumweleza hivi kuwa hivi sasa Mtani wangu Warioba ni Apeche Alolo, anatakiwa atulie awe mtazamaji na ale pesheni yake kwa nafasi huku akisubiri siku za Kuitwa na Mwenyezi Mungu kule kwenye Makao yetu ya milele maana hapa Dunia sote sisi tunapita na niwapangaji.
Warioba ni Apeche Alolo kwasababu Tayari baadhi ya watu wameisha Choka kusikia maoni yake kuhusu Katiba Mpya Kwani wananchi wamebaini hata wakiendelea kumsikiliza maoni yake hayo hawawezi kuibadilisha Katiba Pendekezwa na baadhi ya wananchi wamekinai kumsikiliza Warioba kwasababu wabunge wao waliowachagua mwaka 2010 walikuwa ndani ya Bunge kwaniaba ya wananchi Hao wakawatungia Katiba Pendekezwa.
Sasa wananchi hao wanasema ni uwendawazimu kumsikiliza Warioba na kukubalina na mawazo yake kwasababu wao waliwapigia kura wabunge wao na bado wanaimani nao na ndiyo wabunge walienda kuwawakilisha Wapiga kura Hao Katika Bunge la Kutunga Katiba.
Hivyo Warioba ni Apeche Alolo, yaani kafirisika kisera na mawazo hivyo wanachokisubiria hivi sasa ni kuona sura mpya majukwaani zikiipiga kampeni kuhusu Katiba pendekezwa ili waweze kuipigia kura ya ndiyo au hapana. Maoni , mashati anayovaa Warioba ambayo Marehemu Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela alikuwa akipendelea kuyavaa wamechoka kuyaona Kwani ni Kama ya nawatetea kiungulia Kama siyo Kichefuchefu na yenye Lengo la kuleta vurugu nchini.
Lilokuwa Bunge Maalum la Katiba lilitumia madaraka yake iliyopewa kwa mujibu wa kifungu cha 25(2) Cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2012 , ya kuboreshwa na kurekebisha ile rasimu ya Tume ya Jaji Warioba.
Kwa sisi tunaofuatilia mambo mbalimbali ya mustakabali ya taifa letu tulimshuhudia Jaji Warioba na wajumbe wa Chache wa Tume hiyo kila kukicha akitoa maoni yake ya kutaka bunge la Katiba lisitishwe, mara akidi ya wajumbe wa bunge lile haitatimia lakini akidi ikaja kutimia, anashangaa Mwenyekiti wa lilokuwa Bunge la Katiba , Samwel Sitta jeuri anaipata wapi,serikali Tatu hazikwepi.
Na Septemba 26 Mwaka huu, katika sherehe za kutimiza Miaka 19 kwa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu ( LHRC), na kuzindua kitabu cha maisha ya marehemu Dk.Sengondo Mvungi ambaye alikuwa ni mhasisi wa kituo hicho ,pamoja na mambo mengine huku akishangiliwa ,Warioba ambaye alikiwa ni mgeni rasmi alisema hivi sasa kuna watu wanamuita yeye ni shida kubwa, lakini kuna shida nyingine ndogo ndogo kama aliyekuwa mjumbe mwenzake,Humphrey PolePole , hivyo wanawasubiri mtaani wajumbe wa bunge la Katiba na kwamba wapo Tayari.
Binafsi nilikuwa miongoni mwa waalikwa wa shughuli hiyo ya Uzinduzi wa Kitabu kwasababu Mimi ni miongoni mwa waandishi wa hicho kitabu Cha Dk.Sengondo Mvungi ' Breathing the Constitution'. Na niliandika Habari ya tukio Hilo ambayo ilikuwa na kichwa Cha Habari kisemacho : ' WARIOBA ASEMA ANAWASUBIRI WAJUMBE BUNGE LA KATIBA MTAANI'.
Sasa sijui kilichompata Warioba ndiyo wale maadui zake aliyowaaidi Kuwa atakutana nao mtaani wapambane (yaani waliokuwa wabunge wa Bunge Maalum la Katiba) atakutana nao mtaani wameamua kujihami kwanza kwa kuanza kwa kutendea yeye Warioba shambulizi Hilo la kushitukiza? Sijui.
Wakati Jaji Warioba na UKAWA ambayo hivi sasa UKAWA imepachikwa jina la utani huko mtaani Kuwa kirefu Cha UKAWA ni (Umoja wa Kaburi la Wapinzani), wanaharakati kwa Nyakati tofauti wakitumia haki Yao waliyopewa katika Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo inatoa uhuru wa kutoa maoni.
Kuna baadhi ya watu wakiwemo baadhi ya wana CCM wenzake Warioba walijitokeza na kumpinga hadharani na wengine walifika mbali na kutaka Warioba atangazwe kuwa ni ' Shiida'.
Ushahidi upo wa Mimi binafsi nilitumia Karamu yangu kuandika makala za kukemea vurugu na matamshi ambayo yalikuwa yakitolewa Na baadhi ya wanasiasa ambayo matamshi hayo mengine yalikuwa yakiamasisha wafausi wa washiriki Kutenda matendo ya kuvunja Sheria za nchi kwa kisingizio Kuwa mchakato wa Katiba umevurugwa na waliokuwa wakidai mchakato umevurugwa walishindwa kutupa vielelezo vinavyoonyesha mchakato umevurugwa.
Itakumbukwa Novemba 2 Mwaka huu, Katika ukumbi wa Ubungo Plaza Dar es Salaam, Taasisi ya Mwalimu Julias Nyerere, iliandaa mdahalo ambapo Jaji Warioba alifika pale kutoa mada zake ambazo zilihusu pia Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum ya Katiba jinsi Bunge Maalum la Katiba lilivyoacha baadhi ya maoni ya wananchi yaliyotolewa kwenye Tume ya Warioba yakiwemo Tunu za Taifa na Mzee wangu Warioba amekuwa akilipigia sana kelele Hilo la Tunu za Taifa kuingizwa kwenye Katiba Pendekezwa.
Kwa bahati Mbaya mdahalo huo ulivunjika kwa kile kinachodaiwa Kuzuka kwa vurugu ambazo kisheria siwezi Kusema ninani aliyezusha vurugu hizo Kwani Nasubiri mamlaka husika zituambie Katika uchunguzi wao walibaini Chanzo Cha vurugu nini?kwanini walizusha vurugu? ni akina nani walifanya vurugu?
Nitakuwa ni mbumbumbu wa Sheria hivi sasa kutoa hukumu ya Kusema mtu Fulani au Chama Fulani Ndio kilizusha vurugu siku hiyo kwasababu sina ushahidi Katika Hilo na kwa wale wenye ushahidi wa Hilo wakapeleke ushahidi Polisi ili waliotenda uhuni ule washughulikiwe.
Kwani Tayari kuna watu wamemhukumu Moja kwa Paul Makonda Kuwa ndiye Mratibu na alinipigia Mtani wangu Warioba siku ya vurugu. Minimekuwa nikiwataka wananchi hao watimize matakwa ya Kifungu cha 7(1)a,b Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002.
Kifungu hicho ambacho kinamtaka mtu yoyote ambaye ama taarifa za kutendeka au kutaka kutendeka kwa Uhalifu na Mauaji ,Kifungu hicho kinamlazimisha Mwananchi huyo aende Katika mamlaka husika kutoa taarifa hizo na endapo Mwananchi Huyo atakayekaidi atashitakiwa kwa kusaidia kutendeka kwa kosa.
Msimamo wangu tangu zamani huko wazi Kuwa Mimi ni muumini wa Amani na sipendi vurugu hivyo nachukizwa na wavurugaji wa amani na wahalifu hivyo Watanzania tujifunze Kuwa na uvumilivu wa kuvumilia Kusikiliza tusiyopenda na tukosoane kwa njia ya amani licha uvumilivu wa jambo lolote uwa una mwisho wake.
Jaji Warioba Mtani wangu, rafiki yangu,Mshauri wangu, Msaada Kwangu Mzee wangu ,mwanahabari mwenzangu, msomi mwenzangu wa sheria.Awali ya yote pole na balaa lilokukumba Novemba 2 Mwaka huu, naamini tukio lile utasihau Katika Maisha yako.
Kama nilivyosema hapo juu Jaji Warioba ni Mzee wangu na anamchango wake Katika Maisha yangu binafsi baada ya Tume yake kumaliza kazi akaanza kutoa maoni yake ambayo yalionyesha wazi wazi hafurahishwi na kilichokuwa kilifanywa Bunge Maalum la Katiba , nilimpigia simu Mara mbili na kumshauri aache kutoa maoni Yao Kwani inatosha , Ametoa maoni hayo hayo sana watu wameishamsikia, wamemwelewa na wamefahamu yeye msimamo wake ni upi na baadhi ya makala wa Chama Chake ni upi na Watanzaia wenzake ni upi.
Nilimpa wosia huo Miezi minne sasa imepita kwasababu nilikuwa Kama naona mwisho wa siku anaweza akajikuta anapata wakati mgumu kutokana na maoni yake hayo kuna watu maoni yake hayo yanawakera na wanayatafsiri Kuwa yana Lengo la kuchonganisha wananchi na lililokuwa Bunge Maalum la Katiba, serikali .
Chama Chake Cha CCM, na maoni yake hayo yanalengo la kutaka Katiba Pendekezwa isipigiwe kula za ndiyo.
Na pia kuna tuhuma zingine zinaelekezwa kwa Jaji Warioba na watu wazito katika nchi hii kimya kimya kuwa anachokifanya sasa Warioba ni kutekeleza Jiopolitiki Agenda.
Kwa uamuzi wake wa Kujitoa Mhanga kuhusu Kulalamika baadhi ya mapendekezo yake kutupwa na Bunge Maalum la Katiba lililokuwa linaloongozwa Samwel Sitta .
Jiopolitiki agenda maana yake ajenda za Siri za Mataifa makubwa Ulimwenguni ambazo zinataka viongozi wa Mataifa mengine Dunia waifuate ajenda zao za Siri na endapo viongozi wa nchi hizo ambazo Hazina uchumi mkubwa kutekeleza ajenda zake za Siri ndiyo nchi hizo zinaamua Kuwanunua baadhi ya wananchi wenye ushawishi Katika nchi hizo ambazo Mataifa hayo makubwa inalazimisha itekeleze ajenda zake , kuwapatia Fedha ahadi mbalimbali za ki madaraka, mali pindi wakifanikiwa kutekeleza misheni hizo za Mataifa hayo makubwa kwa Mataifa Yao.
Sasa baadhi ya watu wanamhusisha Jaji Warioba na Mpango huo mchafu Kuwa msimamo wake wa Kulalamika Kuwa maoni ya Tume yake likiwemo maoni ya kutaka kuwepo na serikali Tatu ,Kuwa alihongwa Fedha nyingi na Mataifa makubwa ya nje ili aje ashawishi Tanzania iweke pendekezo la serikali tatu Katika Katiba Pendekezwa.
Eti kwa kuwa misheni hiyo imeshindwa kufanikiwa ndiyo maana ameshindwa kuheshimu dhana ya mgawanyo wa madaraka na matokeo yake licha yeye ni mwanasheria kitaaluma anafahamu dhana ya mgawanyo wa madaraka kwa maana kubwa Tume yake ilishafanyakazi yake na ikamaliza bila kubugudhiwa.
Yeye Jaji Warioba alianza kuushambulia mhimili mwingine ambao ni Bunge Maalum la Katiba kwa kila kukicha kutoa maoni yake ambayo sote watanzania nimshahidi wa Jaji Warioba alivyokuwa akitoa maoni yake kuhusu mwenendo wa lililokuwa Bunge la Katiba na hadi alifikia hatua ya kusema kuwa kura za kupitisha Katiba pendekezwa haitapatikana lakini ilipatikana na Katiba pendekezwa ikalatikana.
Hizo tuhuma zinazoelekezwa kwa Jaji Warioba Kuwa eti ni mtekelezaji wa Jiopolitiki agenda.Binafsi tuhuma hizo zitabaki Kuwa ni tuhuma tu kwasababu sina ushahidi nazo , ila tuhuma hizo ndiyo zinazoelekezwa kwake.Pole sana Mtani wangu na Mbea mwenzangu Jaji Warioba.
Zaidi ya Mara mbili niliwahi kumpigia simu Jaji Warioba pamoja na kumpatia ushauri huo pia niliwahi kumshauri aache kunung'unika kuhusu maoni ya Tume yake kuachwa na Bunge Maalum la Katiba Kwani Tayari ameishapaza sana Sauti Vya kutosha na waliomsikia walimsikia na waliomwelewa walimwelewa na waliompuuza waliipuuza.
Nanina Kumbuka nilimwambia Warioba Kuwa Hao wanaomshangilia kwenye midahalo ipo siku ndiyo watakuwa wakwanza kumwangamiza kama siyo kumzomea na ndiyo wanakuwa wa kwanza kwenda kwa Siri kwenda kumchoma kwa viongozi wa Chama Chake na serikali.
Na wale wanaharakati, wapinzani wa Chama Chake ambao siku Chache zilizopita walikuwa wakilitumia jina na Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji Warioba Kama Kigezo Cha kususia Kikao Cha Bunge la Katiba na kujipatia Umaarufu wa kijinga ipo siku watamuingiza mtaroni na kumwacha solemba.Hakunielewa.
Naweza Kusema Kuwa Warioba ameishindwa kwenda na 'biti'' yaani mdundo wa muziki au kusoma harama za Nyakati Kuwa UKAWA waliokuwa wakijifanya wapo nae bega kwa Bega katika kuhakikisha Katiba Pendekezwa haipatikani,wamemtupa mtaroni .
Hivi sasa UKAWA wameibuka na ajenda mpya tena ya moto moto ya kusaini makubaliano ya vyama vyao kushirikiana kwamba Katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 wasimamishe mgombea urais mmoja na ndicho kipaumbele hivi sasa cha UKAWA na Nguvu zake zote imezielekeza Katika jambo Hilo na hawana Habari nae tena, Habari ya Rasimu ya Warioba Kuwa ilichakachuliwa hawana Habari nayo ila Warioba yeye bado anashupalia na muziki wake wa zilipendwa wa ' Maoni ya Tume yake yalipuuzwa'.
Watoto wa mjini wanasema hivi sasa Jaji Warioba Apeche Alolo' , yaani kafulia, Hana sera Hana jipya.
Nilifanya hivyo kwa nia njema tu kwani nafahamu ndani ya nchi hii kuna watu wana tabia za kihuni tena wapo kila kona, ni makatiri sana,hawana subira wala hawana hofu ya mungu.
Wakiamua kutekeleza unyama ,wanatekeleza wazi wazi kwani hawana aibu wala hawaogopi kwenda kuishi gerezani.Na kuchomoa roho za watu Kwao ni jambo la kawaida sana,hawaoni hatari.
Baada ya kumpatia ushauri huo Jaji Warioba aliniambia amenisikia ila ataendelea na harakati zake Kwani anafanamu anachokifanya Kuwa kina maslahi kwa taifa lake.
Kweli aliendelea na harakati zake hizo hadi Novemba 2 Mwaka huu, Katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, alivyokuwa akihutubia Mamia ya wananchi kuhusu mjadala wa Katiba ndipo tafrani ilizushwa na watu wasiyojulikana kusababisha Mdahalo kuvunjika na Mzee Warioba kupata aibu ya Kufunga Mwaka.
Kwani Wafanya Fujo wale ambao mi siwajui hawakujali Kuwa Warioba ,Joseph Butiku ni Mzee ,waliamua Kuzusha tafrani Hali iliyosababisha wazee kukutwa na wakati mgumu na Mungu alisaidia hawakupoteza maisha.
Sisi wasomi wa Sheria tutamkumbuka Daima ,ukiwa hai au ikatokea Mungu amekuchukua Shabani tusomapo hukumu ya Kesi ya rufaa ya kupinga uchaguzi Katika Mahakama ya Rufaa nchini ( Precedent) ambayo mlalamikaji ni Joseph Warioba V Steven Wassira (1997), TLR 272.
Namheshimu Jaji Warioba kwasababu ni miongoni mwa Wazee wangu ambao wamekuwa wakinikazania nijiendeleze kielimu na kunifunza mambo mengi pia Warioba ni Chanzo changu Cha Habari.
Lakini Ikumbukwe Kuwa Jaji Warioba pamoja na madaraka Mbalimbali alivyowahi kushika hapa nchini, pia ndiye Mtanzania wa kwanza Kuwa Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya masuala ya Bahari na Alipomaliza muda , Mtanzania aliyeteuliwa kwenda Kuwa Jaji wa Mahakama hiyo ni Jaji James Kateka ambaye bado hadi HIvi sasa naye Kateka ni Mzee wangu ni Jaji wa Mahakama hiyo ya Kimataifa na anaishi Ujerumani.
Januari 7 Mwaka 2008, Rais Jakaya Kikwete alipomtembelea Wodini Katika Hospitali a Taifa Muhimbili, Saed Kubenea ambaye usiku wa kuamkia Januari 5 Mwaka 2008 ,pamoja na mambo mengi Rais Kikwete aliwashauri waandishi wa Habari wa jilinde Kwani Habari wanazoiandika wengine zinawakera na wengine hawana uvumilivu wataamua Kuwaumiza tena mchana kweupe.
Ushauri huu pia naweza Kusema unamfaa Warioba,Joseph Butiku , Humphrey Polepole, na wengine wote ambao wanaipinga Katiba Pendekezwa Kuwa wakae wakijua kuna watu wanawakera na misimamo Yao hiyo ya kuikosoa Katiba Pendekezwa.
Hivyo tukio Lililomkuta Jaji Warioba,basi na wao hawana jinsi ya kujiandaa kukabiliana na watu wasiyotaka kusikiliza maoni Yao maana Dalili za vurugu zilianzaga mapema siku chache baada ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2012 ,kusaini.
Vurugu la kwanza lilitokea nje ya ukumbi wa Karimjee ambapo siku hiyo kijana mmoja alipigwa na kung'olewa meno Katika mjadala huo ambao ilidaiwa Fujo hizo zilizushwa na baadhi ya watu waliodaiwa Kuwa ni CCM na Chadema.
Na vurugu la pili lilisababishwa na Mbunge wa Arusha Mjini,Godbles Lema ambaye alipokuwa Dodoma Katika vikao Vya Bunge Miaka miwili imepita sasa alienda Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM), na kuwaamasisha wanafunzi Hao wafike kwa Wingi Katika Viwanja Vya Bunge Kuja kutoa maoni Yao wakati Kipindi chao Cha kutoa maoni kilikuwa hakijafika Hali iliyosababisha Polisi Mkoa wa Dodoma kuweka Ulinzi mkali mtaani na kuwakamata wananchi waliokuwa wamekaidi amri ya Polisi iliyowataka wasiandamane.
Warioba ni Mzee wangu na sijafurahishwa kutoka moyoni uhuni uliofanyiwa ila kwasababu ni Mtani wangu nakucheka sana maana watu wa Msomoa mmekuwa mkijiita Nyie ni 'wanaume' kwasababu mnajua kupambana lakini Jumapili ulikutana na wanaume wenzio. Tetete.Kwakweli kitendo kile alichomfanyia siyo Kizuri na Mimi Nikiwa ni muumini wa Amani nakemea vurugu zile.
Mtani wangu Jaji Warioba Kama unavyonifahamu misiyo mnafki ni msema ukweli.
Ebu Warioba kaa chini sasa utafakari ni kwanini vurugu zile zimetokea wakati wewe ambaye kwa siku za HIvi karibuni uligeuka Kuwa mtu maarufu nchini na baadhi ya wananchi wakiwemo wanasiasa wa upinzani kukuona eti wewe ni lulu kuliko wana CCM wenzio wote hadi wanasiasa Hao wengine ni viongozi wa UKAWA kila walipokuwa Wakitoa hotuba zao walikuwa wakisema rasimu ya Tume ya Warioba ili fanyakazi nzuri lakini Bunge la Katiba limeyapuuza.
Wewe ni Waziri Mkuu Mstaafu, Mwanasheria Mstaafu,Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Kimataifa ya Masuala ya Bahari, Ina maana Kabla ya wewe kwenda pale hukuwa umepata taarifa za Kiintelijensia Kuwa kuna Mpango wa kufanyika kwa vurugu kwenye mdahalo ule?
Lakini pia kuna taarifa za chini chini zinaeleza Kuwa Kabla ya kwenda ukumbini kuna raia wema walikufuata wakakutaka usiende kwenye mdahalo huo kwasababu Walikuwa wana taarifa za Kuzuka kwa vurugu lakini wewe uliwapuuza wakakuacha uenda ukajionee.
Je Warioba tahadhari hiyo ulipewa kweli mapema Kabla hujaenda ukumbini Kama baadhi ya watu wanavyodai?
Au ndiyo maana Mzee Joseph Butiku baada ya vagi kumalizika alisema anawafahamu walioanzisha vurugu lile? Lakini na wewe Butiku ulilifahamu Hilo kwanini ulikubali Swahiba wangu Warioba aje ukumbini?
Kauli yako hii Kwangu Mimi inaniacha na maswali?Inadaiwa kuwa Butiku ni miongoni mwa watanzania ambao walishiriki pia kuijenga Idara yetu ya Usalama wa Taifa na yeye aliwahi Kuwa Askari wa Idara hiyo kwahiyo nayeye alikuwa ni 'nusanusa,chatu,nyoka washawasha'.
Inakuwaje Butiku aseme alishawahafamu waliofanya vurugu zile dakika chache Kama zile baada ya vagi kumalizika? Sasa alivyowafahamu Mbona hatutajii hao wahusika na hadi sasa ameishawachukilia Hatua gani?
Je alifanya upelelezi wake akiwa pale ndani?Na Kama aliufanya aliufanya akiwa hayupo sawa maana baada ya vagi Kuzuka Wajumbe wa meza Kuu akiwemo Butiku,Warioba walikumbwa na Hali ya sintofahamu na kuanza kuangaika kuokoa roho zao?
Hivyo napata wasiwasi Kama huo uchunguzi wake upo sahihi? Na Kama alifahamu Kabla ya vurugu kutokea kwanini aliruhusu Jaji Warioba na mdahalo ule ufanyike wakati yeye ni fundi wa mambo ya kiupelelezi na kiusalama ?
Kama Mtani wangu Jaji Warioba ubongo wako Unafikiri sawa sawa Na unajua kusoma alama za Nyakati , unapaswa sasa urejee matamko zaidi ya manne ambayo yamekuwa yakitolewa na Rais Kikwete Kuwa ataakikisha anawaacha Watanzania wakiwa na Katiba mpya na kwamba hana wasiwasi Katiba Pendekezwa ni bora na anawashawishi Watanzania waipigie kura za ndiyo.
Na siyo Kikwete peke yake hata Rais wa Zanzibar, Dk.Mohammed Shein naye amenukuliwa Mara Kadhaa akiisifu Katiba hiyo.Na siyo Hao tu hata Wazee wenzio wa CCM na serikali wameisifia na wanawashawishi wananchi waipigie kura nyingi za ndiyo.
Wewe Warioba ulishashika madaraka makubwa sana Katika serikali na CCM, unajua miongozo ya kiserikali na kichama na mtumishi yoyote wa serikali au Mwana CCM anayesaliti maagizo au msimamo wa Chama anafanya nini. Jaji Warioba Hilo sijui umesahau?
Maana Kama unakumbuka maadiliki, miiko na Misingi ya CCM vizuri pale tu CCM ilipotangaza uamuzi wake Kuwa CCM msimamo wake ni wa serikali mbili na wewe haraka sana ulipaswa kufuata msimamo wa Chama Chako unataka nini.
Kama uliona msimamo wa Chama Chako unakukera na kukukwaza basi ungeama Chama kuliko kujitokeza hadharani kutoa maoni yanayopingana na maagizo ya Chama Chako na Bunge Maalum la Katiba.
Katika akili ya kawaida tu unapoona Rais wa nchi, Kikwete na Rais wa Zanzibar wanatoa matamko zaidi ya Mara Tatu ya kuinadi Katiba Pendekezwa Kuwa ni bora na hawana wasiwasi Kuwa wananchi wataipitisha kwa kura nyingi, wewe Warioba na wenzako mnaoikosoa Katiba Pendekezwa ni wakinanani wa kuweza kufanikiwa kupingana na Hilo au mbaki salama?
Mlivyoambiwa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia basi ndiyo mnavuka hadi mipaka ya Demokrasia yenyewe?.
Elewa wakati mwingine tunasema Demokrasia imeandikwa kwenye makaratasi ila kwenye utekelezaji wa Demokrasia Hasa kwenye nchi zetu za Afrika ni Nadra kuitekeleza kikamilifu.
Jaji Warioba kwa nyadhifa ulizowahi kushika unapaswa ujiulize pia ni kwanini tukio lile la vurugu limetokea Jumapili, watu na Taasisi husika wala hawajalichukualia uzito wa aina yake na viongozi wenzio tena watu wenye umri mkubwa Kama wewe wamejitokeza Kusema kilichokupata ,ulikitafuta kwa muda Mrefu na waswahili wanasema mwenye kilanga aambiwi pole.
Jaji Warioba wengine wanasema unataka kuwafanya Watanzania ni wajinga wasiyojua kutofautisha Maana ya rasimu, Katiba Pendekezwa na Katiba Pendekezwa inapopatikana kisheria rasimu ya Tume ya Kuandika Katiba mpya inakuwa imekufa kisheria.
Binafsi simung'unyi maneno nasema Warioba kilichokutokea , licha kisheria ,kiungwana hakikustahili kutendewa hivyo, ila ulipaswa ujue Kuwa ipo siku ungetiwa displine na watu wasiyojulikana kutokana na msimamo wako huo ambao unakwenda kinyume na wana CCM wenzako, Rais wa nchi na baadhi ya wananchi ambao wanampenda Rais wao na naipenda Katiba Pendekezwa kwasababu wameisoma na wameilewa.
Namaanisha Kuwa wewe umekuwa ukiikosoa Katiba Pendekezwa Kabla na wakati haijapatikana, hivi ulitarajia wale waliyoshiriki Kuitunga, Wapiga kura wao, wanachama wao toka Taasisi mbalimbali waendelee kukukuacha utambe mitaani na kwenye majukwaa bila kukutenda?
Hivi unafahamu matamko yako kwa kiasi Fulani yamesababisha baadhi ya wananchi wawaone wajumbe wote waliotunga Katiba Pendekezwa hawana akili , siyo wazalendo kwa taifa Lao hivyo wewe tu Warioba ndiyo mzalendo kwa taifa hili unawapigania wananchi kuliko waliokuwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba?
Hivi Warioba ulitegemea baadhi ya wananchi wakuache uendelee kutamba kwenye majukwaa wakati Fedha za walipa kodi zimetumika kikamilifu kuakikisha Katiba Pendekezwa imepatikana?
Rais wa nchi ndiye Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ambayo JWTZ, linaloongozwa na Jenerali Davis Mwamunyange, Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) chini Mkurugenzi Mkuu Rashid Othman ( RO), Jeshi la Magereza , Jeshi la Kutenga Taifa (JKT)chini Meja Jenerali Raphael Muhuga na Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Ernest Mangu.
Viongozi hao wote wa vyombo hivyo vya dola na askari wao wanamtii Rais wa nchi, Kikwete akikohoa kidogo wanahaha na wanakesha macho kumlinda na kuakikisha anakuwa salama na yote anayoyaagiza yanatakelezwa kwanza mambo mengine yatafuata baadae na endapo itabainika kuna mtu au nchi inataka kumbughudhi au kumdhalilisha rais na taifa letu basi vyombo hivyo vya ulinzi na usalama umtia adabu mtu huyo kwa njia inazozijua.
Warioba kumbuka pia majeshi hayo yanaheshimu na yanatenda kazi kwa kufuata sheria ,kanuni na Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Na Hao walinzi wanaokulinda wanawajibika na Kumtii Rais na viongozi wao wa kazi ambao viongozi wao wamwonapo Rais Kikwete wanabana mikono na kumpigia saluti .
Hivyo tambua sasa haya matamko yako yanayopingana na Amir Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, ambao Askari wanaokulinda pia wanamtii, hayawafurahishi na sikufichi kuna baadhi ya Wanajeshi marafiki zangu,mapolisi wameniambia wamefurahishwa na uhuni uliofanyiwa maana umezidi kumdhalilisha na kumpinga na kumkosea adabu Boss wao ambaye ni Rais wa nchi ,Kikwete.
Kama ni mwelewa utaelewa hili kwa mapana yake na hutarudia tena kutoa maoni yako ya kuhusu Katiba Pendekezwa Kwani ujijui tu msimamo wako huo ulikuwa umeanzisha vita na Taasisi nyingi zenye nguvu, Rais wa nchi na wananchi wengine vita ambayo huwezi kuishi da na mwisho wa siku utaumia wewe.
CCM Mwenyekiti wake ni Rais Kikwete ambayo wewe Warioba ni Mwanachama wa CCM na ulishawahi Kuwa mbunge wa Chama hicho na hadi sasa unahesabika ni Mwana CCM licha kuna baadhi ya watu mitaani wanasema 'Jaji Warioba ni UKAWA' eti kwasababu anapingana na msimamo wa Chama Chake na kwamba ingekuwa vizuri aame CCM .
Warioba Kumbuka CCM ndiyo Chama Tawala na wananchi wote Rais wetu ni Kikwete ambaye amechaguliwa Katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 na NEC ndiyo ikatangaza Kuwa ndiye Rais ambaye atawaongoza Watanzania.
Sasa Rais Kikwete ametoka hadharani anasema Katiba Pendekezwa ni bora na Hana Mashaka Kuwa itapitisha na wananchi kwa zaidi ya Mara nne Katika matukio tofauti lakini wewe Warioba unasema siyo bora.Hivi unategemea nini?
Wewe Warioba na Ukawa ni nani muweze Kuwa na jeuri na maarifa ya kuweza kupingana wazi wazi na Rais wa nchi na Bunge Maalum la Katiba ambalo baadhi ya wajumbe wake ni wateule wa Rais halafu mfanikiwe?
Makala hii haimaanishi Kuwa vurugu zile zilifanywa na vyombo Vya dola, waliokuwa wabunge Maalum la Katiba, ziliandaliwa na serikali au CCM , la hasha .
Mimi Kama msomi wa Sheria siwezi Kusema nani kufanya vurugu zile kwasababu sina vielelezo vinavyoonyesha nani aliandaa na nani alitekeleza vurugu zile ,tusubiri Upelelezi wa Jeshi la Polisi.
Wabunge wa kuteuliwa na Rais na wananchi Wengi na Bunge lile lilianzishwa kisheria na kufanyakazi zake kwa mujibu wa Sheria na hata maamuzi ya Mahakama Kuu Katika Kesi ya kutaka Bunge Maalum la Katiba lisimame kufanyakazi yake iliyofunguliwa na Saed Kubenea dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mwaka huu,ilitupilia Mbali Kesi hiyo na Kusema Bunge Maalum la Katiba lipo kihalali na lina mamlaka ya kuboresha na kuongeza kitu rasimu ya Tume ya Warioba ( working document) Katika Kuandika Katiba Pendekezwa.
Rais Kikwete Mara kwa Mara hivi sasa kila anakokwenda ananukuliwa akiisifu hiyo Katiba Pendekezwa na kusema ni Katiba Bora na kwamba kuna wana CCM wenzake waliokuwa wakimpinga alipoanzisha mchakato wa kuandika Katiba mpya lakini aliwapatia madaraka Katika mchakato ule wale wote waliokuwa wakipinga Hatua yake ya kuanzisha mchakato ule.
Iliyokuwa Tume ya Jaji Warioba ya kukusanya maoni ya wananchi ambao ili fanyakazi kwa Miezi 18 ilipewa Uhuru na ila fanyakazi yake na ikamaliza.
Tume ile ya Mabadiliko ya Katiba ilikuwa ni mali ya serikali na Tume ile ilitumia kodi za wananchi kufanyakazi zake na Ripoti ya Tume ile ilikufa rasmi kisheria siku Jaji Warioba alipowasilisha Mbele ya Bunge Maalum la Katiba rasimu ya Tume hiyo ambayo ilipokelewa na Bunge lile na Bunge lile kuifanya rasimu ile Kama 'work document' .
Aidha Bunge Maalum la Katiba nalo lilitumia Fedha za wananchi na likamaliza kazi yake na kutoka na Katiba Pendekezwa. Kwahiyo wewe Warioba ndiyo una akili na maarifa sana kuliko Liloliwa Bunge Maalum la Katiba?
Hatua inayofuata kisheria ni Katiba Pendekezwa kupelekwa kwa wananchi waipigie kula lakini Mtani wangu kila kukicha una lalamika Tunu za taifa hazijawekwa kwenye Katiba Pendekezwa.
Ni kweli hazijawekwa na Mwanasheria Mkuu wa serikali Jaji Fredrick Werema alisema Si kila kitu ki nastahili kuingizwa kwenye Katiba Pendekezwa , vitu vingine vitatungiwa Sheria na kwamba kwa asilimia kubwa Katiba Pendekezwa imechukua maoni mengi yaliyokuwa kwenye rasimu ya Tume ya Warioba.
Mtani wangu, tatizo Hasa nini linalokusumbua hadi kila siku wewe tu ndiyo unanukuliwa kwenye vyombo Vya Habari ukiongea mada hiyo hiyo wakati kuna mambo mengi sana ya kuzungumzia na kutufundisha sisi vijana wa kileo na wasomi wa Sheria?
Kwa Mwendo ule uliokuwa ukienda nao uoni sasa ndiyo unawapa uhalali watu kuanza kuamini zile tuhuma Kuwa ni kweli unafanya Jiopolitiki agenda ?
Maana wewe ni msomi wa Sheria , Hakimu au Jaji akishatoa uamuzi au hukumu Katika Kesi Fulani, Hakimu au Jaji Huyo hapaswi tena kuanza kufuatilia mfungwa aliyemfunga Kifungo Cha gerezani je ni kweli anaishi gerezani?anakula huko gerezani?.
Sasa Mtani wangu inakuwaje wewe ndiye uliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ukifanyakazi yako ukamaliza na Rais Kikwete alikupongeza na kukushukuru kwa kazi nzuri, sasa inakuwaje wewe Huyo Huyo Ukaamua Kujitoa fahamu ukaanza kuingia majukumu ya mwili mwingine ambao ni Bunge Maalum la Katiba?
Au Mtani wangu umesahau ulivyokuwa Chuoni unasoma Shahada ya Sheria kuna somo linaitwa somo la Sheria ya Katiba ambalo Moja ya topiki zake ni dhana ya mgawanyo wa madaraka ( Separation of Power) .Mhimili mmoja usiingilie majukumu ya Mhimili mwingine.
Kumbuka Mtani wangu wewe ulikuwa ni miongoni mwa watu wanaonisistiza sana nisome kwa bidii kozi ya Sheria Kwani nawewe ilipohitimu elimu ya sekondari kwanza ulienda kufanyakazi ya Uandishi wa Habari Katika Gazeti la Standard ambalo kwasasa kinaitwa Daily News ukiwa hata Huna elimu ya kozi ya Uandishi wa Habari.
Baada ya muda mfupi ukuaamua kwenda kusoma kozi ya Shahada ya Sheria hadi ukafikia ngazi ya juu kimadaraka na ukataeuliwa Kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali, Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Masuala ya Bahari na hadi sasa una ofisi yako ya uwakili pale Masaki Dar es Salaam.
Nakumbuka Katika mahafali ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, ya Mwaka 2010, Mimi nilikuwa ni miongoni mwa wahitimu wa kozi ya Cheti Cha Sheria ilitolewa na UDSM, Katika maandamano ya mgeni rasmi aliyokuwa akiongozwa na wakuu mbalimbali wa chuo hicho, Warioba ulikuwa ni miongoni mwa wasomi walikuwa wamevalia mavazi rasmi wakiongozwa kuingia Katika Ukumbi wa Mlimani City.
Jaji Warioba ambaye ni chanzo changu cha habari pia aliponiona alishindwa kuficha hisia zake za Furaha na kunishika mkono nakunisogeza karibu yake kwa pongezi Katika maandamano hayo ya wasomi yakitembea ndipo nilipo mwambia tunavunja Itifaki .
Jaji Warioba wakati akiwa ameshika mkono wangu aliniambia Kuwa amefurahi kuona na mimi siku hiyo nikiwa ni miongoni kwa wahitimu wa kozi ya cheti cha sheria na hiyo inaonyesha nilizingatia ushauri wake ulionitaka nijialivyonishauri nisome nimeyazingatia na akanitaka nisonge mbele kwani hata wao leo hii wamekuwa viongozi wa nchi walisoma kwa tabu na walisota sana.
Hivyo licha ushauri wangu uliomtaka aache kutoa maoni hayo Kwani kazi yake alikuwa ameishamaliza ,akapumzike na familia yake.Ieleweke wazi makala hii haitafanya mimi nisitishe urafiki wangu Na Mtani wangu huyu Kwani namheshimu sana.
Jaji Warioba ananiheshimu kutoka na Utendaji wangu wa kazi Katika tasnia ya Habari na ndiyo Manaa Kipindi kile Mwaka 2009 , Kulipoibuka taarifa zisizo rasmi kimya kimya zilizokuwa kisema serikali inampango wakamfungulia Kesi ya jinai Jaji Warioba kwasababu ya wizi wa Fedha za serikali Katika kampuni ya Mwananchi Gold Mine Ltd.
Warioba alianza kujihami naye akaanza Kujibu mapigo kuhusu taarifa hizo za yeye kutaka kufunguliwa Kesi ya jinai ambapo alitumia mbinu ya vyombo Vya Habari vichache sana kufafanua jinsi mchakato mzima wa Utendaji kazi wa kampuni ya Mwananchi Gold Mine ,ambapo , alikuwa akiniita Mimi na waandishi wengine Wawili tu kufika ofisini kwake Masaki kuandika Habari ambazo yeye alikuwa akinieleza Kuwa siyo yeye wala familia yake haijashiriki kuiba Fedha kupitia kampuni hiyo.
Hivyo Mtani wangu Warioba kuanzia sasa usiende kwenye midahalo kwenda kuzungumzia mambo ya Katiba Pendekezwa,wasije Kukutoa roho au kukutengua mguu bure. Sisi Watani zako tunaotoka Mkoa wa Kagera hatuna Fedha za kusafirisha maiti yako kuipeleka kwenu Mkoani Mara kwasababu sisi wenyeji wa mkoa wa Kagera hivi sasa ni Apeche Alolo yaani hatuna hela,Tumefulia ya kusafirisha maiti yako.
Mtani elewa kuna watu wana roho Katiri sana na wala hawana hofu ya Mungu,wapo hapa nchini , wanafanyia watu unyama halafu hawana Habari na asubuhi ndiyo wanakuwa wa kwanza Kuja Hospitali kukutazama au ikitokea ukafariki dunia.
Watu hao ndiyo uwa wa kwanza kufika msibani na kukuandalia hotuba nzuri na watasema marehemu Warioba alikuwa ni mtu mwema sana, jasiri na aliipenda nchi yake ila rohoni mwao wana Furaha kwasababu Tayari wameishakutoa roho.
Wakishamaliza kukuzika makaburi na hiyo familia yako ndiyo watakuwa hawana Habari nayo na Mifano tunayo.
Sitaki hayo yakukute maana ni mambo Mabaya sana.Tulia Mtani wangu nchi hii ina wahuni. ' watoto wa Mbwa' wapo kila kona hata kwenye nyumba za ibada wapo.
Mtani tulia na familia yako pamoja kampuni yako ya uwakili ,vijana wakitaka ushauri wako wa mambo Mbalimbali watakufuata,Mbona mawaziri wakuu wenzio wastaafu, David Msuya, Dk.Salim Ahmed Salim wametulia ni wewe tu vyombo Vya Habari vi nakutumia kuuza magazeti Yao bila wewe kujua.
Ulijijengea heshima kubwa ni kwanini sasa unataka kuivunja heshima yako uzeeni tena kwa jambo ambalo unalolipigania Mbali unajua wazi halitaleta Mabadiliko yoyote Katika Katiba Pendekezwa?
Hao Wanaojifanya wanakushangilia sasa siku ukipata madhara hutawaona Katika Hospitali kama ni Hospitali ya Apolo India na ndiyo watakuwa wa kwanza kukudhihaki Kuwa ulizidi kiherehere.
Jifunze tukio lilompata Dk.Steven Ulimboka, wakati akiendesha mgomo niliandika makala Tatu za kupinga mgomo na kuwatabiria Wagomaji Hao Kuwa ipo siku watakuja kuumia, Dk.Ulimboka kwa kulewa sifa za wenzake ambao walikuwa wakimtanguliza mstari wa Mbele kugomesha madaktari siku alipotekwa na kushughulikiwa kikamilifu hadi Leo amekoma na amefyata mkia.
Wale Wendawazimu wenzake waliokuwa wakimjaza Ujinga hawana Habari nae na kile kiapo walichokuwa wamejiapiza Kuwa hawatarejea maofisini kufanyakazi baada ya kuona Mwenzao Dk.Ulimboka ametiwa adabu na watu wasiyojulikana.
Mmoja mmoja baada ya mwingine Wakaanza kurudi ofisini kufayakazi wakasitisha mgomo wakati hata serikali ilikuwa bado haijamaliza kuwaandalia Stahili zao na hadi sasa hawataki tena mgomo maana ' Displine'aliyotiwa Dk.Ulimboka na watu wasiyojulikana iliwafanya haraka sana wapone wazimu uliokuwa ukiwatuma Kugoma kutibia wagonjwa hadi kusababisha baadhi ya wagonjwa kukosa huduma ya Afya na kupoteza Maisha kwaajili ya mgomo wa batiri.
Sasa ndiyo ujue, hawa Wanaojifanya wanaandaa midahalo ya kujadili Katiba na wanakualika wewe tu na Hao wanahabari kila kukicha wanakupigia simu unawapatia Habari za kukosoa Katiba Pendekezwa na wale wananchi waliokuwa wakikuita eti wewe ndiye Rais ajaye , Kuwa nao makini sana Kwani wengine ni wazandiki wakubwa na wanakulamba Kisogo.
Ulipaswa ujiulize ni kwanini aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume uliyokuwa ikiiongoza, Jaji Augustino Ramadhani, Tume ilipomalizika kufanyakazi yake alisema katu hatazungumzia kuhusu rasimi ya Tume hiyo na huo ndiyo msimamo wake na kweli alisimama na msimamo huo hadi Leo hajazungumza chochote anaendelea na shughuli zake nyingine kabisa.
Pia Jaji Warioba nakuomba uelewa Kuwa sasa hivi taifa linajiandaa kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu na serikali za mitaa. Tambua Lengo la Chama chochote Cha Siasa ni kukamata dola.
Chama Chako Cha CCM bado kinataka kuendelea kukamata dola ila wewe na UKAWA mnaoikosoa Katiba Pendekezwa wakati CCM ,Rais Kikwete na serikali yake inaiunga mkono Katiba Pendekezwa.
Ninavyoifahamu CCM , nataka nikwambie Warioba Kuwa wakati wa uchaguzi ukikaribia CCM Huwa haitaki Masihala wala utani na mtu hata Kama ni mwenzao.CCM inachoangalia ni mbinu ipi watatumia washinde.
Sasa wewe kila kukicha unatoa maoni ya kuikosoa Katiba Pendekezwa ambayo wao CCM wataitumia Kama ajenda ya kuombea kura katika chaguzi zote mbili Kuwa serikali ya CCM ni sikivu sana imeruhusu Tanzania uendeshe mchakato wa kupata Katiba Mpya, unafikiri wataendelea kukuvumilia?
Kama CCM iliweza kumtimua uanachama Seif Sharif Hamad ambaye kwa sasa ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar tena ambaye alikuwa na wafuasi wengi, ndiyo watakushindwa wewe Mtani wangu?
Ni Haki yako kutoa maoni ila Unatakiwa ujitazame wewe ninani na uliwahi kushika nyadhifa gani na maoni yako yanawakera wakina nani?Hao yanayowakera wana Nguvu kiasi gani kuliko wewe?
Ndiyo maana Mtani wangu nakukaribisha njoo GYM tufanye mazoezi ili siku ukiendelea na harakati zako za kusimama majukwaani kuikosoa Katiba Pendekezwa ,vurugu zikizuka uweze kuanza kujiokoa Mwenyewe halafu walinzi wafuate.
Katika vurugu za Jumapili ulinitia aibu Mtani, yaani ulishindwa hata kulala chini au kuchomoa peni kumchoma adui ukategemea walinzi wakusaidie. Ule ujasiri wa wanaume wa Mkoa wa Mara wa kupambana mtani wangu uliupeleka wapi? Tetetee.
Waswahili wanasema ' ukijua Kurusha ngumi ujue na Kukinga'. Wewe Hilo limekishinda.
Elewa kuwa aliyekuwepo madarakani kwasasa ndiyo mwenye Nguvu hata Kama Mtani wangu umemzidi umri, anauwezo wa kuamrisha jambo lolote lifanyike ambalo jambo hilo likifanyika litakuumiza wewe moja kwa moja ama kwa njia ya Siri au wazi na Hakuna mtu yoyote atayemkataza.
Nimalizie kwa kumwambia Warioba na UKAWA Kuwa walishindwa kipindi kile kuzuia Gari lilokuwa limeegeshwa lisitoke Katika eneo husika Gari lile likatoka , ndiyo leo hii wanafikiri wataweza kuzuia gari ambalo hivi sasa Dereva kaisha Tia Gia anateremka kutoka mlimani ? Jibu ni jepesi hawawezi na wakubali wameishindwa.
Msemo huo ninamaanisha kuwa Warioba na Ukawa kipindi kile mlishindwa kuzuia Katiba Pendekezwa isipatikane ,Leo ndiyo mtaweza kuizua NEC isiendelee na mchakato wa kuandaa wananchi kuipigia kura za Ndio au Hapana. Hamuwezi na Tayari NEC imeishatangaza tarehe ya kura za maoni.
Hamuwezi ,sana sana ni sawa mnafurahisha Manyani au mnamvalisha Mbu miwa.
Sijui mtaweka wapi sura zenu pale NEC itakapotangaza Matokeo ya kura zilizopigiwa Katiba Pendekezwa imekubaliwa na wananchi Wengi .Binafsi bila woga Nasema Katiba Pendekezwa ni nzuri Kwani imegusa Katika maeneo mengi muhimu na pia sina Shaka Kuwa wananchi Wengi wataapigia kura za ndiyo.
Tusubiri Tuone. Jaji Warioba 'Mbea wa zamani yaani Mwandishi wa habari wa habari wa zamani ni Apeche Alolo.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Novemba 6 Mwaka 2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.




--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments