[Mabadiliko] UGUA POLE MKUU, LAKINI HALI YA AFYA NDANI YA NCHI NI MBAYA MNO.

Thursday, November 13, 2014



Mkuu wetu amepata nafuu na ametoka hospitali.

Ni jambo jema kibinadamu kwamba mtu muhimu sana katika nchi yetu ametibiwa salama, wengi tunaombea afya yake iimarike.


Lakini kama taifa, lazima tuendelee kuhoji hali mbaya ya huduma za afya nchini kwetu. Lazima tuendelee kuhoji mamia na maelfu ya wananchi wanaokufa kila siku kwa kukosa pesa kidogo tu za matibabu, dawa na vipimo.


Ukweli ni kuwa, hapa Tanzania matibabu ya kibinadamu na ya kuridhisha wanayapata wanasiasa wakubwa, watu walio nazo au ndugu na jamaa zao wa karibu. Hohehahe wengine kwa mamilioni huweza kufa muda wowote kwa kukosa matibabu kidogo tu.


Hao madaktari tunaowafuata huko nje, tunaweza kabisa kuwatengeneza hapa kwetu na tukawalipa. Hayo mahospitali makubwa tunaweza kabisa kuyajenga hapa kwetu na tukayawekea vifaa vya kisasa na viongozi wetu wakatibiwa katika ardhi yao na hayo mabilioni ya kutibiwa nje tukayaweka kwenye maeneo mengine ya kupambana na umasikini.


Jukumu langu hapa ni kusema yaliyo wazi bila unafiki. Kama nikikugusa potezea.


J. Mtatiro.



...................
    

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments