[Mabadiliko] TUMAINI MAKENE NA HUJUMA DHIDI YA ACT!!!

Wednesday, November 12, 2014

Wakuu,
kumewekwa taarifa hapa na emmanuel muganda na goefrey kundi wakinukuu gazeti la mtanzania na jamiiforums. na baadhi wameomba niseme kitu juu ya taarifa hizo.
  Nasema kidogo hapa siyo kama kiongozi wa chama maana miye hata siyo mwanachama wa ACT bali kueleza baadhi ya taarifa zilizopelekea kuandikwa kwa habari hizi.
  juzi kulikuwa na pilika nyingi sana Tumaini Makene akimwelekeza mwandishi Mwinyishehe kuandaa press comference ambayo alielekeza ifanyike Protea hotel, na kwamba makene angewalipa elfu 20 kila mmoja. baadaye venue ilibadilishwa hadi landmark kwa sababu protea ina uhusiano na kiongozi wetu na pia gharama ni kubwa ili kukwepa kuulizwa chanzo cha fedha za kugharimia hotel bei kubwa kama ile.
   Makene akiwatumia akina Nyakarungu na Mahona kutoa tamko hilo, anadhani atadhoofisha chama cha ACT kilichobeba matumaini ya watanzania.
   Sababu na namna ilivyokuwa mpaka akina nyakarungu na mahona wakawa katika mambo ya namna hiyo natumaini kama itakuwa lazima na muhimu chama chao kitaeleza.
   Lakini nijuavyo mimi kwa taarifa zangu za kiintelijensia, mahona na nyakarungu wameshikwa na propaganda za CHADEMA kuwa chama chao kina fedha nyingi sana. kwa sababu hiyo wameanzisha madai kuwa chama cha ACT kiwalipe posho ya laki 3 kwa mwezi. inaonekana chama hakijaweza kumudu gharama hizo kwa watumishi wake kwa sasa. kwa sababu hiyo wameamua kuchafua viongozi wa chama chao kwa maslahi ya chadema.
  Baada ya press ya Landmark waandishi walikuwa wanampigia simu makene ili awatumie fedha aliyo waahidi lakini hakupokea na baada ya hapo wakawa wanakopa elfu 10 kwa kijana mmoja ambaye ndiye alikuwa akiwafuatilia, naye akawajibu alikuwa na elfu 5 tu ya kupandia bodaboda.
  Undani wa tukio hili zaidi chama kitatoa ufafanuzi.
  Mwl.Ludovick.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CACMr6Qi3dTtgc%3D_53rtBUmHMnNUE4ZFXKzSg_e%2B7kEec%2BLaQ3Q%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments