[Mabadiliko] Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu sasa Imechanganyikiwa

Thursday, November 13, 2014
Kama ilivyotolewa na Salva and Co.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anaendelea na matitabu yake nchini Marekani, leo, Jumatano, Novemba 12, 2014, anatarajiwa kutoka wodini katika Hospitali ya Johns Hopkins na kuhamishiwa kwenye Hoteli Maalum ambako ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.

Rais Kikwete amekuwa kwenye Hospitali ya Johns Hopkins tokea Jumamosi iliyopita wakati alipofanyikwa upasuaji wa tezi dume 
(prostrate) na afya yake imekuwa inaimarika kiasi cha kuanza mazoezi ya kutembea.

Kutokana na kuondolewa kwa bandeji kwenye mshono ambao 
nao umeanza kukauka vizuri, Rais Kikwete baadaye leo atahamishwa kutoka wodini kwenda kwenye Hospitali Maalum yenye uhusiano na Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko karibu na hospitali hiyo.

Akiwa kwenye Hoteli Maalum hiyo, Rais Kikwete ataendelea kupatiwa matibabu, kutembele
wa mara kwa mara na madaktari na kuwa chini ya uangalizi wa wauguzi muda wote. Wiki moja baadaye, Rais Kikwete atafanyiwa tathmini ya kuwawezesha madaktari kuamua hatua inayofuata ya matibabu yake.

Wakati huo huo, kwa sababu ya wingi wa ujumbe mfupi wa simu (sms) ambazo amekuwa anazipokea Rais Kikwete, imeanzishwa namba maalum ya simu ambako wananchi wanaweza kuwasiliana kwa sms na Mhe. Rais. Namba hiyo ni +1-646-309-2295.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, 
Ikulu, 
DAR ES SALAAM.
12 Novemba, 2014


My take:

Kuna matatu, kurugenzi ya mawasiliano imechanganyikiwa, Rais ni mgonjwa sana (prostate/prostrate) au kwenye para ya mwisho, kuna kampeni ya kura ya ndio kwa SMS.
tangu lini rais akaomba kutumiwa sms, kurugenzi ikawa desparate mpaka kutengeneza number maalum ya kumtumia sms za pole?


--
Awesome.
''Everybody is a genius. But if you judge a fish by its ability to climb a tree, it will live its whole life believing that it is stupid." 

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAJJMsUt%2BWOGFaYD-bs4smd%3DUAgzFdPee9bNDV3vxK93Xm%2BrLog%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments