[wanabidii] Majina ya Taasisi na Halmashauri zilizofungiwa kushiriki zabuni za Serikali

Wednesday, October 08, 2014
Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imeikabidhi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) majina 10 ya taasisi na halmashauri ambazo zimeonekana kuwa na viashiria vya rushwa katika matumizi ya fedha za Serikali mwaka 2013/14.

Bodi hiyo pia imezifungia kampuni 23 kushiriki zabuni za Serikali, huku ikiagiza menejimenti ya PPRA kufanya uhakiki kwa taasisi 19 ambazo katika ukaguzi, zimeonyesha kufanya ununuzi unaotia shaka wa Sh1.7 bilioni.

Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Marten Lumbanga alisema jana kuwa taasisi zilizoonekana kuwa na viashiria vya rushwa katika ununuzi ni:-
  1. Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
  2. Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
  3. Halmashauri ya Jiji la Mwanza
  4. Halmashauri ya Kondoa
  5. Halmashauri ya Monduli
  6. Halmashauri ya Kilwa
  7. Halmashauri ya Maswa 
  8. Halmashauri za wilaya ya Kigoma
  9. Halmashauri ya Kibondo
  10. Halmashauri ya Tarime
  11. Halmashauri ya Musoma
  12. Halmashauri ya Ukerewe
  13. Halmashauri ya Maswa
  14. Halmashauri ya Kishapu
  15. Halmashauri ya Kilindi
  16. Halmashauri ya Lushoto
  17. Halmashauri ya Mkinga
  18. Halmashauri ya Bunda
  19. Halmashauri ya Butiama
  20. Halmashauri ya Rorya
  21. Halmashauri ya Kondoa 
  22. Halmashauri ya Songea
  23. Halmashauri ya Singida
  24. Halmashauri ya Mwanza
  25. Halmashauri ya Iramba
  26. Mamlaka ya Maji na Mazingira Lindi
  27. Manispaa ya Kinondoni
  28. Manispaa ya Musoma
  29. Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Lindi
  30. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

Mkurugenzi Mtendaji wa PPRA, Dk Laurent Shirima alisema kuwa tatizo kubwa katika ununuzi wa umma ni watendaji kutokuwa makini au kutofanya kazi zao kwa uaminifu. Alisema PPRA imekusudia kuwaita wakuu wa taasisi zilizofanya vibaya ili kujua tatizo.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments