[wanabidii] HONGERA 'FISADI' BISWALO MGANGA KUWA DPP

Tuesday, October 07, 2014




HONGERA 'FISADI' BISWALO MGANGA KUWA DPP

: KIKWETE KATOA KITU (FELESHI),KAWEKA KITU MGANGA

Na Happiness Katabazi

 OKTOBA  6 Mwaka huu, Ikulu ilitoa taarifa kwa umma uliyosema Rais Jakaya Kikwete alimteua Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Aseti na Rikava   ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), ambaye Cheo cha Kitaaluma ni Wakili Mkuu wa Serikali, 'Fisadi' , Biswalo Mganga kuwa DPP mpya Tanzania.

PICHA HIYO:  Kushoto ni Wakili  wa Serikali Mkuu, Dk.Deo Nangela, Biswalo Mganga ambaye kwasasa ni DPP mteule  mimi Happiness Katabazi , Hamidu Mwanga ambao wote hao walikuwa ni mawaliki wa upande wa jamhuri ambao waliendesha kesi hiyo mwanzo hadi mwisho.Maarufu kwa jina la  Siafu wa aliyekuwa ' DPP  wa wakati huo ,Dk.Eliezer Feleshi.

Picha hii ya ukumbusho baina yangu na mawakili ilipigwa na mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima,Francis Dande, Februali 23 Mwaka 2012 Kwenye mlango wa Mahakama Kuu Kitengo Cha Biashara, Dar es Salaam, ikiwa ni dakika Chache baada ya Jaji Agustine Mwarija kumaliza kusoma hukumu ya Kesi ya Uvuvi haramu Katika Ukanda wa Bahari ya Tanzania kwa kutumia Meli ya Tawariq1 maarufu Kama 'Kesi ya Samaki wa Magufuli'. Jaji Mwarija alitoa hukumu ya Kuwafunga washitakiwa Wawili Miaka 30 Jela baada ya kuwakuta na hatia Katika Mashitaka yaliyokuwa yakiwakabiri.

Mimi  na Mawakili wengine wa serikali akiwemo DPP Mteule Mganga,Michael Luena, Thadeo Mwenepazi,Arafa Msafiri, Oswald Tibabyekomya, Thadeo Mwenepazi, Angaza Mwipopo, Benard Kongora, Ponsian Lukosi, Tumaini Kweka,Shadrack Kimaro, Timothy Vitalis, Malangwe Mchungahela na Fredrick Manyanda ambaye kwasasa ni Katibu wa Tume ya kuchunguza malalamiko ya Operasheni Tokomeze inayoongozwa na Jaji Mstaafu, Msumi na Jaji Feleshi, kila tunapokutana au kusalimiana Kwenye simu salamu ya kwanza ni 'mambo vipi fisadi au wao wananisalimia mambo wao wananiambia mimi mambo vipi Mama Sheikh Ponda?

Hakuna mtu wa kutuzuia tusisalimie kwa majina hayo ,kwani chanzo cha kusalimiana kwa majina hayo ni Mawakili Hao wa serikali  kuendesha kwa muda mrefu kesi za wizi wa fedha katika kaunti ya Madeni ya Nje (EPA), na mimi nilikuwa nao bega kwa bega kuripoti kesi hizo tangu zilioofunguliwa rasmi Novemba  4 mwaka 2008 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, hadi nilipoacha kazi kwa hiari yangu uandishi wa habari hasa habari za mahakamani nchini katika gazeti la Tanzania Daima ,Agosti Mosi mwaka huu na kwenda kuwa Ofisa Habari wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), Chenye Makao makuu yake Mikocheni Kwa Warioba ,Dar es Salaam.

Hivyo Mimi binafsi Sitaacha kutumia salamu yangu hiyo kwa DPP- Mganga na hata Jana jioni nilivyompigia  simu ya kumpongeza, alipoitika nilianza kwa kumwambia ' Hongera Fisadi ' kuteuliwa na  Bwana Khalifan yaani Rais Jakaya Khalifan Mrisho Kikwete Kuwa DPP'. Alicheka sana. 

Kwa wale ambao hamhusiki Kwenye Mtandao wetu wa utani huo, msidiliki kumuita   Mganga 'Fisadi' Kwani Mganga siyo Mtu au Wakili wa serikali wa kuchezewa hata kidogo.Hilo mlijue mapema.

Na kwa wapenda kuvunja Sheria za nchi na wahalifu kwa ujumla Kama hamtataka kubadilika, basi mjiandae kukutana Na rungu la Mganga.

Ibara ya 59B(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 , ndiyo inampa mamlaka rais wa nchi, kumteua DPP. Na kifungu cha 89 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 kinataja Kuwa kutakuwa na mtu mwenye Cheo hicho.

Hivyo Cheo Cha DPP ni Cheo Cha Kikatiba majukumu ya DPP yameanishwa  wazi Katika Ibara ya 59B(2) na kuanzia Kifungu cha 89 Cha CPA.

Awali ya yote kwanza napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa Rais Jakaya Kikwete  kwa Kumteua Mganga Kuwa DPP Kwani namfahamu Mganga vizuri sana nje ,ndani.

Mimi nadiriki Kusema wazi Mganga ni  'Zao, Siafu wa Dk.Jaji Eliezer Feleshi'. Kwani Feleshi alipokuwa DPP alikuwa vijana wake ambao niliwapachika jina la 'Siafu wa DPP- Feleshi'  na Mganga ni miongoni mwa 'Siafu' hao ambao Feleshi aliwapika Katika medani ya uendeshaji wa Mashitaka ya jinai na Walipikika vyema na hadi Leo hii nao wanateliwa kushika nyadhifa za juu ikiwemo kuvaa viatu vya Felelshi ya ni Mganga kuteuliwa kuwa DPP.Hongera sana Mtani wangu Mganga.

Mganga 'Fisadi'ameteuliwa kujaza nafasi hiyo iliyokuwa imeachwa wazi na aliyekuwa DPP wakati huo Dk.Feleshi ambaye alivunja rekodi ya Kuwa DPP kwa Muda mrefu tangu Tanzania ipate Uhuru ambaye alikaa kwa Miaka saba 2007- 2014 .

 Agosti 13 Mwaka huu, Kikwete aliteua jumla ya Maji 20 akiwemo Dk.Feleshi kuwa majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Mchango wa Feleshi wa kitaaluma na uadilifu, uchapakazi Utakumbukwa Katika Ofisi hiyo ya DPP.Ni wajinga wachache wasiyojua hayo watapinga na kukebehi.Tumeishawazoe,hawanisumbui ndiyo kwanza wananipa hamasa ya kuandika makala zenye faida kwa taifa langu.

Namfahamu Mganga Kama Kaka yangu,Mtani wangu, msomi wa Sheria na Mwendesha Mashitaka mzuri tu wa mashauri ya jinai, namfahamu, nilipata fursa ya kumuona Mara kwa Mara mahakamani wakati akiendesha Kesi mbalimbali za jinai zikiwemo Kesi za EPA, Kesi za Samaki wa Magufuli, Kesi ya Kupinga dhamana ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Soka Mkoa wa Pwani, Hassan Hassanor anayekabiliwa na kesi ya kusafirisha kontena la Pembe za Ndovu kutoka Tanzania kwenda China zenye thamani ya Sh.Bilioni 1.1,Mbele ya Jaji Zainabu Mruke wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambaye alikubaliana na pingamizi la Mganga lililotaka Hassanor anyimwe dhamana kwasababu alitenda kosa wakati yupo nje kwa dhamana ya Kesi nyingine.

Mganga  ni miongoni pia mwa Mawakili wa serikali waliokuwa wakiiendesha Kesi za Mauaji , kesi za unyang'anyi wa kutumia silaha Katika Benki ya NMB Tawi la Mwanga.

Mganga Kwangu Mimi na Kwa wale Tunaomfanamu kindakindaki ,ni miongoni mwa maofisa wa serikali waadilifu, wachapazi, wazalendo na anayechukizwa na uhalifu wa  aina yoyote.

Ndiyo maana jana baada ya taarifa ya Ikulu kutolewa, watu tunaomfahamu Mganga tulifurahi sana na karibu usiku kucha tulikuwa tukipigiana simu ,kutumiana ujumbe mfupi  wa kupongezana na kumpongeza Kikwete na vyombo vyote vya dola vilivyoshiriki kikamilifu kupendekeza Mganga ateuliwe kushika wadhifa huo nyeti kwasababu Rais Kikwete amemteua Mtu sahihi na safi kushika wadhifa huo.

Alipoondolewa Feleshi katika Wadhifa wa DPP na kupandishwa cheo kuwa jaji wa Mahakama Kuu ambapo kwasasa Feleshi amekuwa ni miongoni mwa watunga sheria na watafsiri sheria na kesi anazoziamua sisi wasomi wa sheria Tunaziita ' Precedent' ambazo maamuzi yake yanazitaka mahakama za chini ifuate maamuzi hayo, yaani Jaji wa Mahakama wa Mahakama Kuu, licha mambumbu wa sheria wanaaminisha watu ujinga wa makusudi kuwa Feleshi ameshushwa madaraka wakati amepanda daraja.

Watu tulio  karibu sana na Ofisi ya DPP na wafanyakazi wa ofisi hiyo ,tulishikwa na ganzi ya kimya kimya na kukubali ni kweli Rais ana mamlaka ya kumteua DPP na kumuondoa.

Lakini  amemuondoa Dk.Feleshi pale ambaye alikuwa ni DPP mwenye misimamo yake isiyoyumba, ambaye alitaka 'fair  trial' , alitenda kazi zake kwa kumshirikisha mungu kwani Feleshi ni miongoni mwa viongozi ambao wamemshika Mungu,saa 12 asubuhi kaisha ingia ofisini  na anatoka usiku ,  alikataa rushwa za watu wengi tu ambao wengine na wajua na wakati mwingine alikuwa akiwindwa kudhuliwa na watu ambao walitumia njia zote za kumhonga lakini alikataa rushwa zao Hali iliyosabisha aongezewe Ulinzi. 

Hali iliyosabisha baadhi ya maofisa wenzake wa serikali ambao walikuwa wanataka kuburuza kwa maslahi Yao kumuita ' Feleshi ni Jeuri'. Siku zote Feleshi alikuwa akinieleza Kuwa  yeye ni Mtoto wa Mkulima na Mchungaji na yupo Katika Ofisi ya DPP Kutenda Haki bila kuyumbishwa na mtu yoyote.

Tulikuwa yunajiuliza Je Mungu ataziongoza Taasisi husika kumpelekea Rais Kikwete jina la mtu ambaye ni mwadilifu ambaye ameyatoa Maisha yake kwaajili ya kulitumikia taifa? Tulikuwa na fikra hizo Kwani nafasi ya DPP ni kubwa mno na endapo Rais atateua  mtu asiyefaa ,anaweza kuleta Shida Kubwa.

Lakini Mungu  ni Mwema ameziongoza mamlaka  husika na hatimaye Rais amemteua Mganga ambaye sio Kama namfagilia Hapana,namfahamu nimefanya nae Kazi za wazi na za Siri Kwa maslahi ya umma  ni kweli ni Mtu mhadilifu  na mchapa kazi na anaweledi Katika tasnia ya uendeshaji Mashitaka nchini, hivyo watoto wa mjini tunasema Kikwete hajakosea alichofanya Kikwete ' Ametoka chombo'Feleshi' ,kaingiza Chombo Biswalo Mganga'. Safi.

Ila wakati naandika makala hii ya kumpongeza Mganga , nimejikuta nikilengwa na Machozi Kwa kumkumbuka Gwiji la Waendesha Mshitaka nchini ambayo Kamwe Katika Uhai wa Maisha yangu sitamsahau yeye binafsi na mchango wake kwa taifa hili, , Wakili Wa Serikili Mkuu, Marehemu Stanslaus Boniface Makulilo Kwani Enzi za Uhai wake aliyefariki Mei 27 Mwaka 2012, Feleshi akiwa DPP Katika Kesi nzito alikuwa akituma Siafu wake mahakamani wakaendeshe Kesi hizo ambazo ambao 'Siafu Hao' wakiwemo wakina Mganga, Michael Luena, Shadrack Kimaro, Arafa Msafiri, Thadeo Mwenepazi, Prudence Rweyongeza, Timonth Vitalis, Bernad Kongora , Fredrick Manyanda ambao walikuwa wakiongozwa na 'Siafu Mkuu', Marehemu Boniface' Jembe'.

Hivyo Leo Timu yetu hiyo tunayosalimiana kwa kutania kwa kutumia ' Fisadi hujambo' ,wakati tukifurahi  'Fisadi mwenzetu - Biswalo Mganga kuteuliwa Jana na Rais Kikwete ' Bwana Khalifan' Kuwa DPP mpya wa Tanzania, hatuna budi pia kumkumbuka Marehemu Boniface Kwani  licha Mganga amesoma kozi ya Sheria vizuri lakini pia sisi tunaofahamu kindakindaki Ofisi ya DPP, tunasema hadi Rais  mamlaka zimemuona Mganga anafaa Kuwa DPP ni kwasababu pia na mafundisho ya kikazi aliyoyokuwa akiyapata Mganga kutoka kwa waliokuwa wakubwa wake wa Kazi Marehemu Boniface  na Dk.Feleshi.

Mganga , Dk.Feleshi na Boniface wameondoka Katika Ofisi hiyo vizuri bila ya Kuwa na maskendo ya utovu wa Maadili.Walivumilia mengi na waliheshimu mkubwa na mdogo, walionacho na wasiyo nacho.Hawakuwa na makuu na MTu utafikiri walikuwa hawana madaraka Makubwa.

Hivyo Mganga'Fisadi' tulizana tena utilize akili, omba  sana Mungu akuongoze Katika Kutenda Kazi Katika Cheo Chako kipya.

 Nimekuwa Mwandishi wa Habari za mahakamani kwa Miaka 16 nafahamu uchafu uliokuwa Katika Ofisi ya DPP Kabla Feleshi amateuliwa Kuwa DPP alipoteuliwa Kuwa DPP mwaka 2007, Feleshi alijishusha akatafuta watu wenye akili timamu,wazalendo kwa taifa Lako ambao walisaidiane nae kikamilifu kutokomeza tabia chafu ya Nolle Prosequei Kuuzwa Kama njugu.

Kusambaratisha  Mtandao mchafu uliokuwa umeweka kambi pale nje ya Viwanja Vya MaHakama ya Kisutu, Ilala Mtaa wa Mkwepu nyuma ya Club Billicanas ambao Mtandao huo ulikuwa Kazi ya Kutengeneza hati za vifo nyumba zilizoghushiwa ambazo walikuwa wakilitumia Kuja kuwadhamini baadhi ya washitakiwa mahakamani.

Leo hii Mimi ni shahada Mtandao huo umesambaratishwa kupitia Feleshi na timu yake aliyokuwa akifanya nayo Kazi wakiwemo Askari wa Jeshi la Polisi.Mabingwa wale wakutengeneza Nyaraka zile za kughushiwa Leo wamekuwa Malofa wa kutupa ,maana hawana tena Fedha.

Mganga nakuasa samehe wale wote waliokuwa wakikupiga  vita vya wazi ambao wengine walikuwa ni wakubwa wako wa kazi na ambao walishaanza kujiaminisha kuwa wao ndiyo watateuliwa kushika wadhifa huo, nawafahamu.

Kwa Kuwa Bwana Khalifan yaani Rais Kikwete alishawahi Kusema urais wake Hauna ubia, ni kweli tumeshuhudia Katika kupitia matukio  mbalimbali Kikwete neno lake hilo alilowahi kulitoa,ua anamaanisha.

Bwana Khalifan amekuamini  ndiyo mAana la kakuteua Kuwa DPP,  nenda kachape Kazi kwa kufuata Katiba na Sheria za nchi.Usikubali kutumiwa kuumiza mtu kwaajili ya madaraka yako, ukifanya hivyo Kumbuka malipo ni hapa hapa Duniani, Mungu  atakuadhibu tu.Tenda Haki Kwa mujibu wa Sheria.

Mganga ,Nikiwa bado ni mwanahabari nakushauri Mganga Inapobidi kutoa taarifa kwa umma kupitia vyombo Vya Habari Toa ila utoe kwa mipaka na uangalie  ni aina gani ya Mwandishi wa Habari , Ofisi yako inampa taarifa hizo Kwani siyo Siri kuna waandishi wa Habari wengine ni wapotoshaji wa Habari.

Nimekufahamu Mganga  kwa Miaka saba sasa, ni mwadilifu na Katika makala hii nimekutaja Kuwa ni mwadilifu, na siku Nikija kukushuhudia  umekengeuka ,nakuadi Mimi ndiyo nitakuwa wa kwanza kutoka hadharani  Kusema na kuandika Kuwa DPP- Mganga sasa amekengeuka  na amekuwa fisadi wa ukweli ukweli.Na unanijua vizuri tu vilivyo.

Hongera sana Biswalo Mganga kuteuliwa Kuwa DPP. ' Rais  Kikwete Ametoa Kitu 'Feleshi ' ameingiza 'Kitu' Biswalo Mganga. Safi.

Chanzo: Facebook: Happiness Katabazi
0716 774494
Oktoba 7 Mwaka 2014








Sent from my iPad

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments