[wanabidii] AJIRA NA UTENDAJI KAZI WA DR. CHACHA BHOKE MURUNGU WA TPDC UTATA MTUPU

Tuesday, October 14, 2014
AJIRA NA UTENDAJI KAZI WA DR. CHACHA BHOKE MURUNGU WA TPDC UTATA MTUPU. PCCB CHUNGUZENI!

Sisi ni wafanyakazi wazalendo wa TPDC. Tunaamini kuwa TPDC ni Shirika ambalo endapo litaongozwa vizuri linaweza kuwa mkombozi wa wanyonge maana rasilimali ya gesi iliyopatikana nchini inaifanya nchi yetu kuwa na kila sababu ya kutoka katika wimbi la umasikini uliokithiri. Hata hivyo, baadhi ya mambo yanayotokea katika uendeshaji wa Shirika la TPDC yanatutia mashaka na kuhatarisha njozi ya kuwa na Tanzania bora.  Leo, tunajikita katika kuwaeleza watanzania uozo na uovu unaofanywa na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria ndugu Chacha Bhoke Murungu.

Dr. Chacha Bhoke Murungu aliajiriwa na TPDC mnamo March 2014.  Lakini mazingira ya kuajiriwa kwake yanaharufu ya rushwa na ukabila. Chacha aliajiriwa kama Principal Legal Officer II bila kuwa na kigezo cho chote cha kuajiriwa. Sifa kubwa kwa nafasi aliyoajiriwa ilitakiwa kuwa na uzoefu katika tasnia ya mafuta na gesi asilia. Pia mwombaji alitakiwa kuwa na cheti cha ICSA (Institute of Chartered Secretary and Administrator). Vigezo hivi vyote Chacha hakuwa navyo! Kabla ya kuajiriwa TPDC Chacha alikuwa anafundisha UDOM. Katika shahada yake ya uzamili na uzamivu alizopata katika Chuo Kikuu cha Pretoria alisoma masuala ya sheria za haki za binadamu na siyo katika sheria ambazo ni muafaka katika sekta ya mafuta kama sheria za kodi, mazingira, sheria za biashara na bima. 

Chacha hana hata cheti kimoja cha mafunzo katika tasnia ya mafuta na gesi asilia! Mnamo  April 2014, Chacha alipewa nafasi ya kukaimu Ukurugenzi wa  Kitengo cha Huduma za Kisheria. Tetesi zinaonyesha kuwa nafasi hii ya kukaimu pamoja na kuwa alikuwa hana sifa kabisa na alikuwa na mwezi mmoja tu kwenye Shirika aliipata kutokana na kukingiwa kifua na baadhi ya wajumbe wa Bodi ambao ni wenyeviti wa baadhi ya Kamati za Bodi wanaotoka nyumbani kwake Musoma. Hali kadhalika, kuna tetesi kuwa baadhi ya vigogo wa wizara ya nishati ambao ni wa kabila lake au wanatoka mkoa mmoja wa Mara ndio walimpigia chapuo apewe nafasi hiyo.

Lakini tangu apewe nafasi ya kukaimu ukuregenzi wa kitengo cha huduma za sheria, Chacha ameyumbisha sana idara ya Sheria na Shirika. Kwanza anadharau sana wafanyakazi wenzake. Anaona kama wote hawafai na ye ye ndio anafaa. Kwa mfano amekuwa akisikika mara nyingi akisema wajumbe wenzake kwenye menejimenti hawana uwezo(incompetent). Amekuwa na kauli za matusi ya wazi kwa maafisa wenzake. Amekuwa akitumia madaraka yake kukomesha watu walioko chini yake. Kwa mfano watu wenye uzoefu na kazi za Shirika amewabagua kabisa kinyume na Sheria na anafanya kila njia kuwakatisha tamaa kwa kutowashirikisha kwenye kazi na vikao. Pia, amekuwa akieneza uzushi ili kufarakanisha wafanyakazi. Amekuwa akitoa fursa za safari za kikazi kwa upendeleo wa wazi ikiwa ni pamoja na kutoa fursa kwa wanawake ili kujipatia rushwa ya ngono!

Tangu aajiriwe na TPDC, Chacha ameshalipoteza Shirika kwenye mambo mengi na kulisababishia hasara kubwa!. Kwa mfano, alishauri vibaya Shirika liwafukuze wafanyakazi wawili Flora Salakana Marealle na Braison Kunyalanyala ambao walilitumikia Shirika kwa muda mrefu na kwa uaminifu mkubwa.  Sasa hivi wafanyakazi hawa wamepeleka mgogoro CMA na kuna kila dalili na sababu kuwa watashinda na hivyo Shirika litalazimika kulipa mamilioni ya pesa kama siyo mabilioni.

Chacha hana welewa kabisa katika sheria za mafuta na gesi asilia-Sheria ya Utafutaji na Uzalishaji wa Petroli ya 1980 (Sura 328), Sheria ya Petroli ya 2008 na Mikataba ya Uzalishaji na Ugawanaji (PSAs). Matokeo yake ni kuwa anashauri vibaya Shirika. Kwa mfamo ameshauri vibaya sana TPDC kuhusiana na mpango wa kampuni ya BG ya kujiondoa katika Kitalu na 3. Hatimaye TPDC ikaishauri vibaya Serikali. Hivyo, tangu Julai 2014 mpaka leo kumekuwa na malumbano yasiyona na tija na yasiyoisha kati ya TPDC na BG!. Chacha anakiburi na hataki kukubali ukweli kuwa hanauzoefu na elimu kwenye tasnia ya mafuta na gesi. Hata hivyo watu wenye uzoefu wa muda mrefu na waliosomeshwa kwenye tasnia ya mafuta na gesi anawapiga vita na hataki kuwashirikisha kwa sababu anaogopa 'challenge'. 
Pia, Chacha amekuwa akivunja kanuni za Shirika. Kanuni zinasema ofisi inatakiwa kukaimishwa kwa afisa mkuu anayekuwepo ofisini (most senior officer) lakini kwa jeuri yake amekuwa akiamua kukaimisha ofisi mtu ye yote bila kujali cheo hasa akizingatia masilahi yake binafsi. Pia hama uzoefu wa kuongoza idara na kuwa kwenye menejimenti. Amekuwa akiendesha ofisi bila kuzingatia ngazi za kiutendaji. Yeye kama kaimu mkurugenzi anatakiwa kuwasimamia maafisa waandamizi, na maafisa waandamizi wanatakiwa kuwasimamia maafisa wadogo. Lakini matokeo yake yeye anataka kusimamia peke yake maafisa wote kinyume na taratibu matokeo yake anasababisha vurugu kwenye Kitengo.

Chacha amekuwa akiandaa vikao vya kamati ndogo ya Kamati za Bodi na kujilipa posho zile zile kama za wajumbe wa Bodi kinyume na taratibu. Pia amekuwa akichukua au kuwapa rafiki zake pesa ya wajumbe ambao hawajafika kwenye vikao ambao kimsingi ni ubadhilifu wa mali za umma! Chacha pia, amekuwa akiandaa vikao hewa ili kujipatia pesa. Kila wiki kumekuwa na vikao vingi sana vya Bodi au Kamati za Bodi na hakuna minutes za vikao husika. 

Hayo ni baadhi tu ya mambo machache tuliyowaletea Watanzania ili mjue jinsi ambavyo maradaka mliyowapa baadhi ya watu yanavyotumiwa vibaya kuangamiza taifa letu na masilahi yenu. Tutaendelea kuwapa taarifa nyingi ambazo tunazo ili tuweze kusaidia kusafisha uchafu uliopo katika ofisi za umma. 

Sisi ni watanzania wazelendo, tunaipenda nchi yetu. Hatuko tayari kuona watu wapuuzi wanaongoza mashirika kwa misingi ya ukabila, chuki na ubinafsi. Sisi tunaamini kuwa madaraka ni dhamana na ni lazima yatumiwe kwa uchaji na unyenyekevu. Na wale wanaopewa maradaka ya umma lazima wawe mfano katika mienendo yao katika jamii.

Hivyo tunaomba sana vyombo vya Serikali, hasa PCCB wafanye uchunguzi wa  ubadhilifu wa mali za umma unaofanywa na Chacha. Kwa kuanzia, itabidi kuchukua vocha zote za malipo ya vikao vya Bodi kuanzia April 2014 mpaka sasa na kuangalia minutes za vikao zilizosainiwa ili kujiridhisha na wajumbe waliokuwepo. Hapo ndipo haya tunayosema yatadhihilika. Pia, mamlaka za Serikali ni vema ziunde Kamati ya kufanya uchunguzi wa madai yote  tuliyoyasema hapa juu ili kuhakikisha masilahi ya nchi hayaendelei kuangamizwa.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments