KWA NINI NINYI WAKATOLIKI MNAUNGAMA DHAMBI ZENU KWA PADRE AMBAYE NI MWANADAMU NA MDHAMBI BADALA YA KUUNGAMA MOJA KWA MOJA KWA MUNGU?
Hapa tunaongozwa na maneno ya Bwana Yesu mwenyewe alipowapa amri hiyo mitume wake; "…Pokeeni Roho Mtakatifu. Wowote mtakao waondolea bdambi, wameondolewa; na wowote mtakao wafungia dhambi, wamefungiwa" (Yn 20:22-23). Na huo ndio utaratibu wetu tangu mwanzo wa Kanisa wakati wa Mitume:
" Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na Kuombeana mpate kuponywa" (Yak 5:16a). Ni miongoni mwa maagizo msingi ambayo hatuna mamlaka ya kubadili labda Yesu mwenyewe aliye agiza aje abadilishe. Mungu anayesamehe dhambi ndiye aliyechagua njia ya kutoa huo msamaha, sisi tu nani hata tumpinge na kumpangia njia zetu? Tunamfundisha Mungu kazi ? Inashangaza kusikia siku hizi hata baadhi ya Wakatoliki wameanguka katika mtego huo wakutaka kubadilisha agizo hilo la Yesu, sijui kwa nini wanataka kurahisisha mambo kiasi hicho. Mungu hafanyi kazi zake hewani bali kupitia kwa watu wake.
Tunapoomba msamaha, tunategemea kusikia maneno haya: "nimekusamehe",hatutaki kuamini kwamba mtu akinyamaza au akiongea kimoyomoyo basi ametusamehe. Yesu kwa kujua umuhimu na kazi ya neno hilo, alilitumia mwenyewe akiwa binadamu (Lk 7:48) na alitaka aendelee kulitumia hata utimilifu wa dahari katika hali ya kibinadamu, ndo maana aliwaachia binadamu (baada ya yeye kuondoka duniani na kurudi mbinguni) kwa niaba yake. Kuondolewa watu dhambi ni moja ya utume wa Yesu (Mk 2:10), ni pamoja na kazi hiyo aliwaachia mitume wake (Yn 20:23)
Tukilinganisha na mfano wa mtume Petro baada ya kumkana Bwana, tunaweza kujifunza kwamba tunapoongea na Mungu peke yetu ni katika hali au hatua ya toba na majuto ( Lk 22:61-62) hivyo bado tunadaiwa kuungama ili kuondolewa dhambi zetu (Yn 21:15-17)
Cha kushangaza ni kwamba Wakristo wote tunaamini kwamba Sakramenti ya Ubatizo inatuletea ondoleo la dhambi ya asili na nyingine zilizotendwa kabla ya ubatizo na huwa hatujibatizi wenyewe wala hatubatizwi na Mungu bali na wanadamu wenzetu, sasa kama huyo mwenzetu anatubatiza na tunaondolewa dhambi zetu, iweje tukija kwenye kitubio tunapinga ushiriki wa binadamu mwenzetu wakati matokeo yanayotarajiwa ni yale yale? Iweje akisima, " Nakubatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu" hakuna shida ila akisema, "Nakuondolea dhambi zako kwa Jina la Baba na la Roho Mtakatifu iwe shida? Huoni kama unajipinga na kujichanganya mwenyewe?
-- Hapa tunaongozwa na maneno ya Bwana Yesu mwenyewe alipowapa amri hiyo mitume wake; "…Pokeeni Roho Mtakatifu. Wowote mtakao waondolea bdambi, wameondolewa; na wowote mtakao wafungia dhambi, wamefungiwa" (Yn 20:22-23). Na huo ndio utaratibu wetu tangu mwanzo wa Kanisa wakati wa Mitume:
" Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na Kuombeana mpate kuponywa" (Yak 5:16a). Ni miongoni mwa maagizo msingi ambayo hatuna mamlaka ya kubadili labda Yesu mwenyewe aliye agiza aje abadilishe. Mungu anayesamehe dhambi ndiye aliyechagua njia ya kutoa huo msamaha, sisi tu nani hata tumpinge na kumpangia njia zetu? Tunamfundisha Mungu kazi ? Inashangaza kusikia siku hizi hata baadhi ya Wakatoliki wameanguka katika mtego huo wakutaka kubadilisha agizo hilo la Yesu, sijui kwa nini wanataka kurahisisha mambo kiasi hicho. Mungu hafanyi kazi zake hewani bali kupitia kwa watu wake.
Tunapoomba msamaha, tunategemea kusikia maneno haya: "nimekusamehe",hatutaki kuamini kwamba mtu akinyamaza au akiongea kimoyomoyo basi ametusamehe. Yesu kwa kujua umuhimu na kazi ya neno hilo, alilitumia mwenyewe akiwa binadamu (Lk 7:48) na alitaka aendelee kulitumia hata utimilifu wa dahari katika hali ya kibinadamu, ndo maana aliwaachia binadamu (baada ya yeye kuondoka duniani na kurudi mbinguni) kwa niaba yake. Kuondolewa watu dhambi ni moja ya utume wa Yesu (Mk 2:10), ni pamoja na kazi hiyo aliwaachia mitume wake (Yn 20:23)
Tukilinganisha na mfano wa mtume Petro baada ya kumkana Bwana, tunaweza kujifunza kwamba tunapoongea na Mungu peke yetu ni katika hali au hatua ya toba na majuto ( Lk 22:61-62) hivyo bado tunadaiwa kuungama ili kuondolewa dhambi zetu (Yn 21:15-17)
Cha kushangaza ni kwamba Wakristo wote tunaamini kwamba Sakramenti ya Ubatizo inatuletea ondoleo la dhambi ya asili na nyingine zilizotendwa kabla ya ubatizo na huwa hatujibatizi wenyewe wala hatubatizwi na Mungu bali na wanadamu wenzetu, sasa kama huyo mwenzetu anatubatiza na tunaondolewa dhambi zetu, iweje tukija kwenye kitubio tunapinga ushiriki wa binadamu mwenzetu wakati matokeo yanayotarajiwa ni yale yale? Iweje akisima, " Nakubatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu" hakuna shida ila akisema, "Nakuondolea dhambi zako kwa Jina la Baba na la Roho Mtakatifu iwe shida? Huoni kama unajipinga na kujichanganya mwenyewe?
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments