[wanabidii] KigwangaLLA AKIMBILIA KWA MADAKTARI WENZAKE; AJITETEA KUHUSU NIA YAKE

Saturday, September 13, 2014
source: jamii forums 

Haya ni maelezo ya Mhs Dokta Hamis Kigwangalla akijieleza ni kwa nini ameamua kugombea na kwa nini madaktari wenzake wamuunge mkono, haya ni kama nilivyoyanasa kutoka kwenye mtandao wa matabibu waliosoma naye muhimbili.


"Ndugu zangu katika fani,


Ninawashukuru sana kwa maoni yenu juu ya nia yangu ya kugombea Urais mwaka 2015.

Silengi kumjibu hata mmoja wetu humu ila nalenga kuwaomba sana mdumu katika kunifanyia dua na kunikumbuka katika maombi. Kuutaka Urais si jambo la lelemama, ni jambo zito, Urais siyo Urais wa DARUSO, siyo Uenyekiti wa Intern, siyo U-CR wa MD1, siyo unaharakati wa kupambana na UKIMWI vyuo vikuu, siyo Ubunge, ni jambo lenye mambo mengi, na sasa ndo kwanza saa 11 asubuhi, jogoo amewika, bado hakujacha...tuna kazi kubwa mbele yetu...tuna milima ya kupanda na mito ya kuvuka...lakini, tukiamini, tukishikamana, tukajipanga, hakuna kinachoshindikana. Mimi ninaongozwa na falsafa kubwa sana kwenye maisha yangu kwamba, 'ndoto hufanya vitu vitokee, hakuna kinachoshindikana ilimradi tu uamini.' Ninawaomba tuamini pamoja, tushikamane pamoja, tupigane pamoja, tutashinda pamoja. 

Hakuna mtu huwa ameiva kuwa Rais wala ambaye hayuko tayari kuwa Rais; ni wito wa kuitumikia nchi yako, ni uwezo wa kuwashawishi wana wa nchi yako wakuunge mkono, ni namna unavyoweza kuionesha future ya nchi yako itakavyokuwa kwa wana wa nchi yako na wakashawishika kukuunga mkono kinacho-matter! Urais, kwa mtazamo wangu, is not about the past, but about what you will do as a leader in the future and for the future of your country...I think and believe I have a new vision for our country, I have solutions for the most pressing challenges in our country today and in the future na kutangaza kwangu nia kunatoa fursa kwa wana wa nchi yangu kunipima na kunihoji ni nini nitaifanyia nchi yetu kama nitapewa fursa. Katika waliojitokeza, sijaona hata mmoja anayezungumzia mambo ambayo naamini ndiyo msingi wa kuwepo hapa tulipo na ni namna gani tutatoka: mambo kama nidhamu ya kazi, uwajibikaji, a culture of excellence in whatever we do, uadilifu na uzalendo, mfumo wa motisha etc hakuna anayeya-address - kila mtu anazungumzia maji, elimu, afya, miundombinu etc etc tunasahau kwamba ili tuendelee inabidi tubadilike kama Taifa kwa ujumla - siyo kutegemea kila kitu kitafanywa na serikali tu...we need a 'game changer', an overhaul of the system we use to think about our development strategy, na hii haihitaji uzee ama ujana, inahitaji ujuzi, uwezo, utayari na uelewa wa nini cha kufanya. 

Watu wakinitazama mimi wanaona kama bado vile, siwashangai. Wengine wanadhani nina umri mdogo, wengine wanadhani sijaiva 'kiserikali serikali' - mimi ninawaambia hapa kwamba hiyo pengine ndiyo comparative advantage yangu kubwa, na pengine ndiyo itakayolisaidia Taifa, kwamba you put in place someone atakayefanya mambo kwa utofauti kwa kuwa hafumbwi fumbwi na system ya bureaucracy kama ilivyo maana hajaizoea kivile! Hata hivyo kwenye dunia ya sasa ya biashara ninaamini tunahitaji mtu tofauti na mwenye sifa tofauti, aliyekulia si tu kwenye serikali, pia kwenye profession na kwenye corporate world ili aingie kazini na skills na experiences za corporate and professional worlds. Sifa ambazo mimi ninazo na ndiyo maana I have offered my humble self to the service of my country. Ninaamini sifa hizi zinahitajika kwa zama hizi zaidi ya sifa ya kuwa Waziri kwa miaka 10 kwa mfano! 

Tusiifanye kazi ya Rais ni ya wanasiasa 'pure' peke yao, tuangalie na nje ya wanasiasa tunapotafuta Rais. Japokuwa wanasiasa wengi wana advantage wakigombea kuliko wengine kwa kuwa wanakuwa ni maarufu na wanamitandao na hivyo wanachaguliwa kirahisi. 

Mimi nime-develop knowledge, skills and experience nikijifunza kutoka kwenye duru mbalimbali; kwenye sayansi, kwenye harakati, kwenye NGO, kwenye consulting, kwenye biashara, na sasa nimeingia kwenye siasa - hivi wasomi kama sisi hapa, hatuoni kama hizi ni advantages kwa daktari mwenzetu na kwa Taifa? Hebu tutafute kama kuna mgombea mwingine miongoni mwa waliojitangaza na wanaotajwa tajwa, ni nani ana sifa na mchanganyiko kama huu? 

Wengine wanadhani mimi bado sijawa na mtandao mpana kwenye chama na kwenye mfumo wa serikali: kwanza si kweli, nimejipanga kwenye hili. Lakini pia tujiulize, hivi kama wana mfumo wa afya wote tukisimama nyuma ya Daktari mwenzetu nchini, tukakusanya na marafiki zetu wa sekta nyingine nyeti kama za ualimu, kuna mtu atasimama na sisi? Leo mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya TAMISEMI, hivi huu mtandao wa MA-RC, maDC, ma-DED na watendaji wote wa Halmashauri tukiweza kuutumia kwa faida yetu - bado kuna mtu atasema tu kuwa 'HK hana uzoefu, ama mtandao mrefu kwenye serikali?' 

Vile vile mimi wakati mwingine huwa ninafikiri perhaps tunapaswa kupata Rais asiye na mitandao sana ya wanasiasa wenzake ili awe huru kufanya kazi kwa uhakika aweze kufanya mapinduzi ya namna tunavyoendesha business nchini. Kuwa na mtandao wangu mdogo inaweza kuwa advantage kwangu na kwa nchi kama nitapata fursa, maana sintokuwa na madeni ya kulipa fadhila! 

Nikiwatazama hao wenye uzoefu (kwenye siasa na utumishi wa umma) kunishinda, sioni, kutoka moyoni mwangu kabisa vision yao, zaidi miongoni mwa wengi wao naona rekodi mbovu tu ya rushwa na ubadhirifu, na kwa wale walio wasafi basi kwa wengi wao sioni ubunifu bali naona 'business-as-usual', wakati mwingine natamani JK angeendelea, ama tumrudishe Mzee Mkapa tu...

Nimalize kwa kuwashukuru na niki-share nanyi funzo moja nililojifunza over the few years I am blessed to have lived; kuwa 'there is nothing more powerful than a young man with a dream.' Lets allow ourselves to dream big, and work on our dreams...for life without dreams doesn't exist, kila mtu huwa anaota sema mara nyingi tunaruhusu woga utawale fikra zetu na hivyo kuota vitu vidogo vidogo. Lets think outside the box and push ourselves kufanya mambo makubwa kwa ajili yetu binafsi na ultimately kwa Taifa letu na dunia nzima. Theodore Roosevelt aliwahi kusema: 'dare mighty things.' I am daring, pals. 


Be blessed,
HK. "

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments