[wanabidii] POLISI AMENODHALILISHA MLIMANI CITY

Saturday, September 13, 2014

POLEE SANA KAKA KUNAHITAJIKA NIDHAMU ZAIDI KWA JESHI LETU LA POLISI...

Derek Murusuri

MLIMANI CITY NI HATARI SANA!!! LEO HII 2/9/2014 MTU MMOJA ALIYEJITAMBULISHA KWANGU KUWA NI POLISI, BADAYE NIKAJUA KUWA ANAITWA D8612 SGT DENIS MTOKA, ASKARI KANZU, MREFU, MWEUSI, MNENE, KITUO CHA CHUO KIKUU, MKOA WA KIPOLISI WA KINONDONI, ALINITAKA NITOKE NJE YA MLIMANI CITY WAKATI NIKITOKEA EXIM BANK KUCHUKUA FEDHA NA KUWEKA KATIKA AKAUNTI MBALIMBALI ZA WABOBEZI WA LIFE MEDIA.

ALISEMA ANANITILIA SHAKA KUWA MIMI NI JAMBAZI KWA SABABU ANAONA NAONGEA SANA NA SIMU HALAFU NAINGIA KATIKA MABENKI. HAKUTAKA NIJITAMBULISHE LICHA YA KUTOA UTAMBULISHO FASAHA NA WASIFU WANGU NA KUWA NI MDAU DUKA MOJA KUBWA HAPO MLIMANI CITY (SUPPLIER) LAKINI HAKUTAKA KUNISIKILIZA AKAWA ANATAKA ANIPELEKE KITUO CHA POLISI.

HAKUTAKA KITAMBULISHO NA AKANIKATAZA NISIPIGE SIMU. ALICHUKUA BETRI YA SIMU YANGU ALIPOIANGUSHA CHINI. MUDA WOTE SIKUTOA TUSI WALA NENO KALI WALA UPINZANI. NILITAKA KUMFAHAMU NA PIA KUJUA KOSA LANGU. ALINISHIKA SURUALI NYUMA KAMA MWIZI AKINITAKA NIENDE NJE YA JENGO. NILITII. BAADA YA KUMUONA MMOJA WA WAFANYAKAZI WA EXIM BANK KATIKA KUNDI, NIKAMKABIDHI HELA NILIYOKUWA NAYO NA KUAMBATANA NAE HUKO NJE. UMATI ULIKUWA MKUBWA SANA. HUKO NJE ALITAKA KUNIPELEKA KITUO CHA POLISI NISICHOKIJUA KWA KOSA NISILOLIJUA. HUKO NJE ALITOKEA INSP EVELYN MSOBI AMBAE ALINICHUKUA PAMOJA NA ASKARI KANZU DENIS NA KUNIHOJI. BAADAE INSP MSOBI AKASEMA YAISHE.

AFANDE DENIS AKANIULIZA KUWA NINAELEKEA WAPI FROM THERE??? NIKAMJIBU, UNA MAANA GANI? AKASEMA NATAKA NIKUPE ULINZI NIHAKIKISHE UNAFIKA OFISINI KWAKO SALAMA....

HAYA YANAKUJA BAADA YA KUNIDHALILISHA MBELE YA KADAMNASI PASIPO KOSA LOLOTE BAADA YA KUTOKA BENKI. HII NDIO HALI HALISI. MWENYE UFAHAMU AELEWE HAYA. CAMILUS WAMBURA, RPC NA CLASS MATE WANGU MILAMBO SEKONDARI, HII NDIO HALI HALISI. BWANA WA MAJESHI AENDELEE KUTUPA ULINZI WAKE. AMEN

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments