[wanabidii] MWANASHERIA MKUU WA SMZ AJIUZURU KAMA KAJITOA BMK

Saturday, September 06, 2014
MWANASHERIA MKUU WA SMZ AJIUZURU KAMA KAJITOA BMK

Ndugu zangu ,

Nimepokea kwa masikitiko habari ya kwamba mwanasheria mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar amemuandikia barua mwenyekiti wa bunge maalum la katiba kuhusu kusudio la kujiondoa kwenye Bunge maalum la Katiba .

Kama kweli hii imefanyika namshauri mwanasheria huyo ajiuzuru pia nafasi yake kama mwanasheria mkuu wa Zanzibar ili mwingine ateuliwe aweze kutumia fursa hiyo kama yeye ameshindwa kuvumilia na kuendelea na harakati za kuandika katiba mpya .

Kama taifa tusidhubutu kuvumilia viongozi kama hawa wanaoshindwa kuvumilia hoja tofauti na wanaotaka kupeleka maoni ya makundi yao au watu wao ndani ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania .

Kama kweli ameandika barua , aruhusiwe kujiondoa lakini pia aandike barua ya kujiuzuru uwanasheria mkuu wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar .

Ameshindwa kazi apewe mtu mwingine atakayeweza kuwakilisha maslahi ya taifa kwa ujumla .



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments