[wanabidii] Hizi Takwimu Zinatuambia Nini Kuhusu Akili Zetu Kama Taifa?

Thursday, September 11, 2014

Hizi Takwimu Zinatuambia Nini Kuhusu Akili Zetu Kama Taifa?

MABASI YA ABOOD:

1/12/2010 - Basi la Abood iliua watu 2 maeneo ya Misugusu
4/1/2011 – Basi la Abood likielekea Morogoro lagonga waendesha pikipiki na kuwaua papo papo, abiria wajeruhiwa
23/ 1/ 2011 – Basi la Abood lagonga Trekta na kumgonga Mpanda Baiskeli maeneo ya Mtego wa Simba nje ya Morogoro – watu wajeruhiwa.
2/6/2011 – Basi la Abood lapata ajali huko Mbeya, 31 wajeruhiwa 
4/10/2011 – Basi la Abood lagonga kwa nyuma basi la Super Feo na kujeruhi watu kadhaa akiwemo dereva aliyebanwa na usukani. z
8/10/ 2011 – Basi la Abood lapata ajali Makambako, Iringa kwa kugonga kundi la ng'ombe.
17/2/2012 – Basi la Abood lapata ajali Mbezi ya Kimara, watu kadhaa wajeruhiwa
10/31/2012 – Basi la Abood lapata ajali eneo la SAE kwa Mbilinyi (1 afa) (Namba T545 AZE).
28/11/2012 – Basi la Abood lagonga basi dogo la wanafunzi (Hiace) likiwa limeegeshwa. Lajeruhi watoto 7. (Basi Namba T 527 AZE)
12/6/2013 – Basi la Abood likielekea Morogororo lapata ajali eneo la Mkambarani, Mbezi ya Kimara.
6/8/2014 – Basi la Abood lapata ajali Msitu wa SAO Hill Mufindi, Iringa, watu wote wanusurika.

MABASI YA HOOD

4/8/2013 – Basi la Hood lapata ajali kwa kugongana na gari dogo maeneo ya Igulusi.
12/19/2013 – Basi la Hood likitokea Mbeya lapata ajali eneo la Melela, Mvomero Mkoani Morogoro – mtu mmoja afa na 27 wajeruhiwa
11/3/2014 – Basi la Hood lapata ajali eneo la Same, mtu mmoja afa na 16 wajeruhiwa.
3/25/2014 – Basi la Hood lapata ajali eneo la Inyala Mbeya watu 4 wahofiwa kufa.
4/2/2014 – Basi la Hood lapata ajali kwenye Msitu wa Mufindi, Iringa
11/3/2014 – basi la Hood lapata ajali eneo la Mwanga, Kilimanjaro
26/8/2014 – Basi la Hood lapata ajali maeneo ya Kikatiti, Arusha, abiria wanusurika lakini watu 4 kwenye daladala wapoteza maisha

MABASI YA SUMRY

26/5/2011 – Basi la Sumry likitokea Arusha kwenda Mbeya lilipata ajali eneo la Igawa na kuua watu 13 papo hapo
2/3/2013 – Basi la Sumry likitokea Sumbawanga kwenda Mbeya lilipata ajali maeneo ya Songwe. Abiria 50 wanusurika maisha
5/7/2013 – Basi la Sumry lilitumbukia mtoni na kuua watu 9 na kujeruhi 53. Ajali ilitokea wilaya ya Mlele Mkoani Katavi
28/4/2014 – Basi la Sumry lilipata ajali huko Ikungi Mkoani Singida na kuua watu 18. Hapa kulikuwa na ajali ya awali ya lori kumgonga mwendesha Baskeli. Maafisa 4 wa Trafiki waliokuwa wakipima eneo la ajali walikuwa miongoni watu waliokufa wengine 14 waliokuwa wamekusanyika kwenye eneo la ajali waligongwa na basi la Sumry na kupoteza maisha hapo hapo!

Baadhi ya Ajali za Mabasi Zilioua na Kujeruhi Watanzania Wengi

8/12/2012 – Basi la Usokomi Tours lilitumbukia kwenye korongo Mlima Ihemi huko Iringa Vijijini – Watu 9 Wafa
9/12/2012 – Basi la Sabena linapinduka eneo la Kitunda, Sikonge Tabora – Watu 17 Wafa
20/1/2014 – Basi
21/4/2014 – Basi la Luhuye Express likitoka Tarime kwenda Mwanza liliacha njia na kugonga nyumba kupinduka huko Busega, Simiyu – Watu 20 wafa
30/7/2014 – Basi la Moro Best likitoka Mpwapwa kwenda Dar lilipata ajali eneo la Pandambili, Kongwa Dodoma (eneo hili si geni kwa ajali za magari) – Watu 20 wafa

Na hapo sijaweka takwimu zozote za hivi karibuni au nyingine nyingi....

My Take: Ndege japo wanafanana kwa kuruka angani wana akili tofauti sana. Wapo ndege wajanja na wengine wapo wapo tu. Kati ya ndege wanaosifiwa kwa akili sana ni kunguru na njiwa na kati yao ni kunguru ambaye anatajwa kuwa ni miongoni mwa ndege wenye akili sana. Kungura ni ndege mwenye uwezo mkubwa sana wa kujifunza na kupitisha kile alichojifunza kwa makinda wake na hivyo vizazi vya kunguru vina hazina kubwa ya ujuzi. Ndio maana kuna msemo "Kunguru Hafugiki".

Lakini wapo ndege wengine ambao wanaishi kwa kuishi tu; hawajifunzi lolote. Ndege hawa wanaweza kukaa kwenye waya wa simu au kwenye mti na mmoja wao akapigwa kwa jiwe la manati wengine wote watashtuka na kuruka mbali kabisa wakiamini ni hatari. Baada dakika chache ndege wale wale watarudi kwenye mti ule ule au nyaya zile zile! Na inawezekana hata hawajagundua kuwa mmojawao hayupo nao milele!

Hizi naziita akili za manyoya; akili za ndege; ndege wasiojifunza kwa sababu hawana uwezo wa kujifunza. Naogopa kusema nafananisha hili na akili zetu kama taifa... tunashtuka, tunasikitika, tunalalamika; halafu tunapenda mabasi yale yale na tunachagua watu wale wale kuturudisha kwenye mti ule ule au nyaya zile zile...

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments