[wanabidii] BUNGE LA KATIBA LAPEWA WIKI 2 LIWE LIMESIMAMISHA SHUGHURI ZAKE

Friday, September 12, 2014

BUNGE LA KATIBA LAPEWA WIKI 2 LIWE LIMESIMAMISHA SHUGHURI ZAKE
Jukwaa la Katiba Tanzania limesema linatoa wiki mbili kwa Bunge Maalum la Katiba kusimamisha shughuri zake vinginevyo jukwaa hilo litahamasisha wananchi kwenda Dodoma na makufuri kuzuia shughuri za bunge hilo na kufunga milango ya majengo ya bunge hilo.

Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Deus KImbamba amezungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar e Salaam saa 5:00 eneo la Sinza katika ofsi za jukwaa hilo.
KImbamba amesema hatua hiyo imekuja kutokana na Rais Jakaya Kikwete na kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kukubaliana katiba mpya haitapatikana badala yake mchakato uendelee baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

KImbamba amesema kuendelea kwa bunge hilo ni kufuja fedha za watanzania na kwa kuwa hakuna maridhiano ya kisisa hivyo vikao vya bunge hilo vinapaswa kusimama mara moja mpaka pale maridhiano yatakapokuwepo.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments