[wanabidii] TAMKO LA IKULU KUHUSU KATIBA LAWACHANGANYA UKAWA

Friday, August 15, 2014
Mtakumbuka kuwa Jumanne tarehe 12 Agosti 2014, viongozi wa UKAWA walitoa tamko la pamoja lililosomwa na James Mbatia la kumtaka Rais kuvunja Bunge Maalum la Katiba vinginevyo wataitisha maandamano nchi nzima.

Baada ya tishio hilo la UKAWA, jana Alhamis tarehe 14 Agosti 2014, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, SALVA RWEYEMAMU ametoa tamko. Katika tamko hilo, Rweyemamu amesema kuwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba haina kipengele kinachomruhusu Rais kuliahirisha wala kulivunja Bunge hilo kutokana na sababu yoyote ile. Kuhusu maandamano, Rweyemamu alisema kuwa hayataleta msaada wowote katika kupata katiba mpya sana sana yatasababisha vurugu nchini kitu ambacho serikali haitavumilia hali hiyo kujitokeza.

Baada ya kauli hiyo ya Ikulu, wadau wangu ambao wapo Karibu na Mwenyekiti wa CHADEMA, FREEMAN MBOWE na ambao wanaratibu kwa karibu vikao vya UKAWA, amenifahamisha kuwa kauli hiyo ya Ikulu imemshtua sana Mbowe. Kwamba, Matarajio ya Mbowe yalikuwa kumtisha Rais ili akishatishika, wao watumie mwanya huo kujijenga kisiasa. Kwamba, kama Rais angevunja Bunge, wangetumia fursa hiyo kujijenga kwa wananchi kuwa nguvu yao imemfanya Rais wa nchi kusitisha mchakato wa katiba na hivyo ingekuwa credit kwao. Kuhusu msimamo wa serikali wa kuhusisha maandamano hayo na vurugu, Mbowe amesikika akisema kuwa ikiwa huo ndo msimamo wa Ikulu, ni wazi kuwa maandamano yao hayatakuwa na mafanikio. Pia Mbowe amesema kuwa UKAWA hawakuwa na mpango wa kufanya maandamano bali walikuwa wanamtisha tu Rais ili alivunje bunge la Katiba kwani kuendelea kwa vikao vya bunge hilo kunawanyong'onyesha sana viongozi wa UKAWA.

Mbowe amesema kuwa kwa sasa wanakabiliwa na msukumo mkubwa kutoka kwa wabunge wao ambao wengi wameonesha nia ya kuendelea kwenye bunge la Katiba. Kwamba, wamefanya uchunguzi na kugundua kuwa wabunge wengi wameonesha nia ya kurejea isipokuwa wanaogopa kufanya hivyo kwa kuhofia kuwajibishwa na vyama vyao. Kutokana na hali hiyo Mbowe amesema kuwa wamelazimika kuwapa kiasi cha fedha (ambacho hakukibainisha) baadhi ya wabunge ili kuwaziba midomo. Hata hivyo, amesema kuwa kiasi walichopata hakilingani na malipo yanayotolewa kwa wabunge wa bunge hilo hali ambayo anahisi kuwa itawaletea matatizo kwa siku zijazo.

Kutokana na hali hiyo, wadau wangu hao wamesema kuwa Mbowe amewasiliana na viongozi wenzake wa UKAWA juu ya tamko hilo la Ikulu. Kwamba, viongozi wa UKAWA watakutana na watatoa tamko kuhusiana na msimamo huo wa Ikulu. Katika tamko hilo, UKAWA inakusudia kulazimisha maandamano ili jeshi la Polisi lichukue hatua ya kuyadhibiti hali ambayo haitawaletea aibu kwao. Kwamba ikiwa watafanya maandamano hayo na jeshi la Polisi litayazima, itakuwa ahueni kwao kuliko wasifanye kabisa.

Aidha, wadau wangu wamemsikia Mbowe akionesha wasiwasi na msimamo wa Lipumba na Mbatia. Kwamba Lipumba na Mbatia wanaonekana kutokubaliana na baadhi ya mapendekezo na msimamo wa CHADEMA wa kutumia nguvu kuzima bunge ka Katiba. Kwamba wanasiasa hao wanapendekeza kuendelea na mazungumzo hali ambayo wao CHADEMA hawaitaki. 

http://www.jamiiforums.com/katiba-mpya/707389-msimamo-wa-ikulu-wamchanganya-freeman-mbowe-na-ukawa.html

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments