TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete, baada ya kushauriana na Tume
ya Utumishi wa Mahakama, amewateua
wafuatao kuwa Majaji wa Mahakama Kuu
ya Tanzania kuanzia tarehe 13 Agosti, 2014.
WATUMISHI WA MAHAKAMA Bw. Penterine Muliisa KENTE, ambaye
kabla ya uteuzi alikuwa Msajili wa
Mahakama ya Rufani, Dar es Salaam.
Bw. Benedict Bartholomew MWINGWA,
ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili
wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam. Bw. Edson James MKASIMONGWA, ambaye
kabla ya uteuzi alikuwa Katibu wa Jaji
Mkuu.
Bw. David Eliad MRANGO, ambaye kabla ya
uteuzi alikuwa Msajili, Baraza la
Ushindani, Dar es Salaam. Bw. Mohamed Rashid GWAE, ambaye
kabla ya uteuzi alikuwa Msajili,
Mahakama Kuu, Kitengo cha Kazi, Dar es
Salaam.
Dkt. John Eudes RUHANGISA, ambaye
kabla ya uteuzi alikuwa Msajili, Mahakama ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki, Arusha.
Bw. Firmin Nyanda MATOGORO, ambaye
kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu
Mwenyekiti, Baraza la Rufaa la Kodi, Dar
es Salaam.
MAWAKILI WA SERIKALI NA TAASISI MBALIMBALI ZA SERIKALI Dkt. Eliezer Mbuki FELESHI, ambaye kabla
ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi wa
Mashitaka, Dar es Salaam.
Bi. Barke Mbaraka Aboud SEHEL, ambaye
kabla ya uteuzi alikuwa Kaimu
Mkurugenzi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.
Bi. Winfrida Beatrice KOROSSO ambaye
kabla ya uteuzi alikuwa Katibu Mtendaji,
Tume ya Kurekebisha Sheria, Dar es
Salaam.
Bi. Lilian Leonard MASHAKA, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Naibu
Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa, (TAKUKURU), Dar
es Salaam.
Bi. Leila Edith MGONYA, ambaye kabla ya
uteuzi alikuwa Msaidizi wa Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dar es Salaam.
Bw. Awadhi MOHAMED, ambaye kabla ya
uteuzi alikuwa Mchunguzi Mkuu, Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,
(TAKURURU), Dar es Salaam.
MAWAKILI WA KUJITEGEMEA Bw. Lugano J.S. MWANDAMBO, kutoka REX
Attorneys, Dar es Salaam.
Bw. Amour Said KHAMIS, kutoka AKSA
Attorneys, Dar es Salaam.
Dkt. Paul KIHWELU, ambaye kabla ya
uteuzi alikuwa Wakili wa Kujitegemeana Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu Huria,
Dar es Salaam.
Bi. Rose Ally EBRAHIMU, ambaye kabla ya
uteuzi alikuwa Wakili wa Kujitegemea,
Bulyankulu Gold Mine Ltd, Shinyanga.
Bi. Salma MAGHIMBI, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mjumbe, Tume ya
Ushindani, (FCC), Dar es Salaam.
WATUMISHI WA VYUO VIKUU Dkt. Mary Caroline LEVIRA, ambaye kabla
ya uteuzi alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitivo
cha Sheria, Chuo Kikuu Kishiriki cha
Ruaha.
Dkt. Modesta Opiyo MAKOPOLO, ambaye
kabla ya uteuzi alikuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu, Mzumbe,
Morogoro.
Wateuliwa wote wataapisha tarehe 15
Agosti, 2014 Saa 05.00 asubuhi katika
Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam. Imetolewa na Mkurugenzi Idara ya habari Maelezo 13 Agosti, 2014
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments