[Mabadiliko] Mkwamo Wa Katiba; Kuna Njia Ya Tatu...

Wednesday, August 13, 2014


Ndugu zangu,

Alfajiri ya leo kupitia vituo vya redio vya Kwanza Jamiina Nuru FM nilishiriki kuongoza mjadala uliotokana na yaliyomo kwenye magazeti ya leo.

Habari kubwa ilikuwa ni UKAWA kutishia kuandamana nchi nzima kama Rais Jakaya Kikwete hatovunja Bunge la Katiba na kumruhusu CAG kukagua hesabu za Bunge la Katiba.

Mtazamo wangu katika hilo ni kuwa huu ni mwendelezo wa mkwamo katika kuipata Katiba. Niliweka wazi, kuwa tuko katika mgogoro wa kisiasa kuhusiana na Katiba.

Kuna mapungufu katika pande zote mbili, lakini, jawabu kwa sasa si kwa Rais kuapewa masharti ya kuvunja Bunge vinginevyo kuwepo kwa maandamano ya nchi nzima. Kuna njia ya tatu ya kwenda mbele kutoka hapa tulipo; nayo si nyingine bali ni NJIA YA MAZUNGUMZO. Kwamba pande hizi mbili hazina namna yoyote ile ya kuikimbia meza ya mazungumzo. Wana mawili tu ya kuchagua; kuikwepa meza na kuhatarisha nchi kuingia kwenye mgogoro mkubwa zaidi na kisha kurudi tena mezani huku nchi ikiwa imepata hasara kubwa sana.

Hivyo, lililo la hekima na busara ni kutafuta suluhu na mariadhiano ya mezani KWANZA na hivyo hakutakuwa na madhara makubwa kwa nchi hapo baadae.

Na hakika, itakuwa ni upumbavu wa viongozi wetu kushindwa kutumia njia ya mazungumzo kwa kuaminiana na kuheshimiana na hivyo kumaliza kadhia hii. Maana, ni upumbavu huo ndio unaoweza kutuingiza kwenye matatizo makubwa kama taifa.

Unaweza kusikiliza mjadala huo nilioshiriki kupitia...http://www.mjengwablog.com/habari-za-kijamii/item/13820-sikiliza-kipindi-cha-soko-la-habari-kariakoo.html

Maggid Mjengwa,
0754 678 252

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye7yVYZ4isK9MiJXSAF7WC0Nzfmw%3DOTDqD2v8aNTNhm27A%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments