[wanabidii] RIPOTI YA KIBANDA: JUKWAA LA WAHARIRI MPOOOO!

Monday, August 11, 2014
Kwa muda nimekuwa nalalamika kwa ujumla tu juu ya taarifa za upotoshaji ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya watu, hasa zikiwa na lengo la kuonyesha jamii kuwa mimi nimehusika kwa namna moja ama nyingine na tukio hilo la kishenzi. ripoti ya jukwaa la wahariri licha ya kuwa lilikuwa la aibu kutokana na kuwa chini ya kiwango, lakini lilijaa upotoshaji, unafiki, uongo na ujanjaujanja. baadhi ya watu katika ripoti wametaja watu tofauti kama wahusika, lakini wakija hapa hunitaja mimi. sasa madhali nimepata ripoti yote, nakusudia kuanza kuichapa hapa ili muone nani alimtaja nani kwa kumtuhumu.
   swali ambalo lazima hawa watu wajibu ni kama pesa walizopewa na TMF zilitumika kwa kazi ya uchunguzi ama walijifungia chumbani wakatafuna mamilioni na kuandika mawazo ya watu wakiita uchunguzi? mfano kuna mtu katika ripoti, akiwa mtuhumiwa, lakini jukwaa limemruhusu kutoa hotuba na akatuhumu na watu wengine na dhahiri jukwaa ama timu ya uchunguzi ikawa na hitimisho ambalo kwa kiasi kikubwa linakubaliana na mtuhumiwa huyo.
   Niseme mapema kabisa kuwa jambo hili ipo siku litajulikana ukweli wake kwa sababu dola inafanya kazi yake, na MUNGU ni mlinzi wa wanyonge kama mimi. sasa uchunguzi wowote u7napaswa kujibu baadhi ya maswali muhimu.lakini ripoti ya jukwaa la wahariri haijibu swali hata moja,badala yake inaibua maswali mengi kuliko hata yaliyokuwepo kabla ya uchunguzi. hii inasema jambo moja kubwa, tukio hilo halijachunguzwa kutoshwa na watu wananitumia mimi kuficha maovu yao. ipo siku watalipa. tutaona majina yaliyo kwenye ripoti hii, ambayo nadhani makusudi hayajawahi kuwekwa hadharani, bali jina langu ndiyo limewekwa na tangia hapo kila mmoja ameshindilia tuhuma kwangu ili kuficha wengine. tutayaona majina hayo.
   Ndugu, watu wamezidi kunitumia kama shimo la takataka. uvumilivu unaniishia sasa, ninaanza kusema yale baadhi wanataka nibaki kimya wanitumie kutenda maovu yao. kikosi cha uchunguzi kinasema hakikukamilisha ripoti yao mpaka mwezi august. mimi nilitoka gerezani mwezi wa saba. kikosi hakikuona haja ya kunihoji hadi leo. kimehoji watuhumiwa wengine wote, ila mimi kimechagua kutokunihoji na lakini kimehitimisha humo kuwa ninatiliwa shaka. kwa nini kikosi hiki hakikutaka kupata maelezo yangu? MUNGU hawafichi wanafiki.
   nakuja hivi karibuni na undani wa ripoti hii.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments