[wanabidii] NAWAKUMBUSHA TU: MWALIMU NYERERE ALIPOMWAGA MACHOZI DODOMA KUPINGA HOJA YA TANGANYIKA

Tuesday, August 19, 2014

MWALIMU NYERERE ALIPOMWAGA MACHOZI DODOMA KUPINGA HOJA YA TANGANYIKA

 
KIKAO CHA PILI DODOMA 14:10:I993

Nilipokwisha kuhakikishiwa kuwa sasa sera ya Serikali Tatu ndiyo sera rasmi ya Bunge la Muungano na Serikali ya Muungano, nilijaribu kupata maelezo kutoka kwa viongozi wetu; lakini sikufanikiwa. Waziri mkuu nilipomuuliza kama kweli wamebadili sera, alicheka tu!
Nilikuwa na safari ya kutembelea nchi za Asia kwa ajili ya shughuli zinazotokana na uenyekiti wangu wa Tume Nchi za kusini. Niliporudi kutoka safari nilijaribu tena kuonana na viongozi wetu ili nipate maelezo lakini sikufanikiwa kumpata kiongozi yeyote mhusika.
Nilipopata habari kwamba Halmashauri Kuu ya Taifa itakutana Dodoma, nilihisi kuwa bila shaka viongozi wetu wataeleza kwa nini wameacha msimamo wa Chama na maagizo ya Kamati Kuu ya kupinga hoja ya Utanganyika, wakaamua kukubali hoja hiyo.
Basi nikaomba angalau nipatiwe nafasi nihudhurie kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya Taifa, ili nami nisikie maelezo watakayotoa. Baada ya maajabu ambayo haina maana kuyaeleza, nilikubaliwa nikaenda Dodoma.

KIKAO CHA FARAGHA

Safari hii tulikuwa na vikao viwili. Kwanza kikao cha faragha wakiwapo viongozi wakuu wote wa Chama na Serikali, na wengine wa nyongeza. Kilikuwa kikao kirefu na kigumu.
Sina kawaida ya kulizwa na mambo ya siasa, lakini katika kikao hiki nilishindwa kujizuia kulia. Sikupata maelezo ya maana ya kuwafanya watu wafanye walivyofanya. Nilipouliza kwa nini hawakupinga hoja ya Serikali tatu kama tulivyokuwa tumekubaliana, majibu ya viongozi wetu Wakuu yalikuwa ni ya ajabu kabisa. Ati wabunge wenye hoja baada ya kuonana na mimi Msasani walikwenda Bungeni wakiwa wakali kama mbogo! Tena walikuwa wakiwatukana wenzao (yaani wabunge wa Zanzibar), kwa kuwataja majina.
Hizi ni sababu za ajabu sana za kuwafanya viongozi watu wazima watekeleze msimamo mzima wa Chama chao na makubaliano ya watu makini kuutetea msimamo huo, na waamue kuikumbatia hoja ya mbogo wakali! Huu ni uongozi wa ajabu kabisa!
Nilipowabana zaidi niliahidiwa kuwa maelezo mazuri yatatolewa kesho yake na waziri wa Sheria na mambo ya katiba katika kikao cha Halmashauri Kuu ya taifa.

KIKAO CHA HALMASHAURI KUU:
Hakika siku ya pili yake waligawiwa 'TAARIFA YA SERIKALI JUU YA AZIMIO LA BUNGE KUHUSU HAJA YA KUUNDA SERIKALI YA TANGANYIKA NDANI YA MUUNDO WA MUUNGANO'. Taarifa yenyewe ni ndefu ina maelezo mengine ya mapambo tu, au ya kiini macho. Lakini vipengele vinavyohusika na suala lenyewe vilikuwa vichache na nimevinukuu kwa ukamilifu.
9. "Tarehe 30 Julai, 1993 wakati wa mkutano wa bunge la bajeti ukiendelea, zaidi ya wabunge 50 kwa pamoja walitoa taarifa ya kusudio la kuwasilisha hoja Bungeni ambayo inadai, miongoni mwa mambo mengine;
Kwa kuwa kuendelea mfumo huu wa Muungano usiowaridhisha wananchi wengi wa upande mmoja ni kuhatarisha kuendelea na kudumu kwa Muungano na pia kuathiri uelewano kati ya watu pande zote mbili; na
Kwa kuwa uwezekano wa kuunda serikali moja ya Jamhuri ya Muungano kwa nchi nzima kwa mambo yote haujajionyesha;
Hivyo basi wabunge hawa wanaliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano katika mkutano wake wa kumi na mbili unaofanyika Dar es salaam liazimie kwamba;
Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilete Muswada Bungeni, kabla ya Februari 1994, kurekebisha Katiba ya Jamhuri ya Muungano ili kuwezesha uundaji wa "Serikali ya Tanganyika" ndani ya Muungano.
Tarehe 12 Agosti, 1993 hotuba ya kuwasilisha Makadirio ya Wizara ya Sheria na Mambo ya Katiba ilisomwa Bungeni.

Inapatikana hapa: http://brotherdanny5.blogspot.com/2014/08/mwalimu-nyerere-alipomwaga-machozi.html



--
"Kama hawatuwekei mgombea mzuri, kwanini watutawale?" ~ Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam, 1995

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments