Shirika moja la kimataifa linayojulikana kwa jina la International Health SA limeandaa mkutano wa mashoga na wasagaji kutoka baadhi ya nchi za Afrika zinazokandamiza haki za mashoga na wasagaji ili kujadili mustakabali
wa haki zao.
Mkutano huo ambao umeandaliwa na shirika hilo kutoka Afrika Kusini unafanyika katika Hoteli maarufu iliyopo
katikati ya jiji la Dar es salaam kwa siku mbili yaani leo na kesho ambapo pia wahudhuriaji wa mkutano huo
ambao ni mashoga na wasagaji wote wanalala hapo.
Kwa bahati mbaya Nimeshindwa kupata agenda za mkutano huo, kwa sababu nilikuwepo hapo kuhudhuria mkutano mwingine ambao bado unaendelea ndipo nilipoona wanaume na wanawake wengi ambao baadhi wanaonekana wanatokea nchini Uganda wakiwa na muonekana wa kishoga na wasagaji.
Baadhi ya mashoga hao wanatokea katika nchi za Ghana, Afrika Kusini, Kenya pamoja na Uganda ambayo ina wahudhuriaji wengi hawa wa Uganda nahisi wako wengi baada ya Museveni kupinga swala hilo nchini kwake.
Miongoni mwa mashoga hao yuko mmoja anayeonekana kuwa maarufu lakini sikupata kujua uraia wake na alijitambulisha kwa jina la Beyoncé. Huwezi kuamini kama ni mwanaume kwa jinsi alivyo mrembo wa sura na
umbo zuri la kike na sauti nyororo. urembo wake ulinogeshwa zaidi na weupe wake wa asili.
Nilijaribu kutaka kuzungumza na baadhi yao walipotoka muda wa mapumziko, lakini walionekana kutotaka kuongea
na mtu yeyote wasiyemfahamu na mkutano wao ulionekana kuwa wa siri mno, hata wanahabari waliokuwa hapo hawakuweza kujua kinachoendelea.
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/699528-mashoga-na-wasagaji-wa-afrika-wakutana-jijini-dar-kudai-haki-zao.html
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments