KUELEKEA UCHAGUZI BAVICHA NGAZI YA TAIFA
Salaam kwenu wanachama wa CHADEMA ambao ndio msingi wa chama hiki tokea ngazi ya Msingi hadi Taifa, salaam hizi nazitoa kwa heshima ya dhati kabisa kwenu Makamanda. Bwana Yesu Asifiweeeeee, Asalaam Alyakum...
Ninazitoa salaam hizi kutokea ndani ya moyo wangu kwani natambua fika kuwa nyie ndio mmekuwa mawe na simenti pamoja na matofali ya kukijenga chama hiki tokea kilipoasisiwa mwaka 1993, nyie ndio mmekifanya chama hiki kuendelea kubaki kwenye dira ya siasa za Tanzania, nyie ndio mmekiletea heshima kubwa chama hiki katika rubaa za kisiasa kitaifa na kimataifa. Nyie ndio mmekuwa ngao ya chama hiki pale kilipotikiswa na mishale na mikuki ya maadui, Nyie ndio mmekifanya chama hiki kusimama na kuweza kupigana na maadui, nawaheshimu sana Makamanda.
Sote tunajua na kutambua kuwa chama chetu kwa sasa kiko kwenye uchaguzi wa ndani wa viongozi, zoezi ambalo limechukua mda kidogo kwa sababu chama kina mizizi mirefu na kimefanikiwa kupanuka na kufika kila sehemu ya nchi yetu. Hivyo basi tumeweza na tunaendelea na zoezi la kuwapata viongozi ambao watakivusha chama katika bahari SIASA kwa miaka ijayo, ni wakati sasa wa kila mwene nia ya dhati na chama kusimama na kuwa tiyari kukiokoa chama na kukivusha ng'ambo ya mto. Sote tunajua kuwa kuna watu wengi wametangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali za BAVICHA_Taifa na wengine wanaendelea kutangaza au wanangoja, ni mda muafaka sasa wa kuwa makini zaidi ya kipindi chochote maana hapa ndipo adui anaposimama na kujiandaa kulipua.
Ndio mda ambao bila kuwa makini sana tunaweza kukipasua chama kwa sababu huu ndio mda amabao maadui watajitahidi kujenga makundi ndani ya chama.
WE HAVE TO BE VERY ENTUSIASTIC
Ni mda sasa wa kuchambua yupi ana nia njema ya Kumrithi kamanda wetu aliyepigana kwa mda sasa bila kuchoka na kufanikiwa kuifanya BAVICHA kuwa taasisi yenye kuheshimika kimaamuzi na kimisimamo John Heche, John alifanikiwa kuiletea BAVICHA heshima kubwa sana na daima tutaukumbuka mchango wake kwa chama.
BAVICHA inamhitaji mtu mwenye mtizamo wa kimapunduzi na kimaendeleo ambaye ataifanya iweze hata kujitegemea kirasmali na kiuchumi, mtu ambae hana hila na mwenye kunuka harufu ya Makundi ndani ya chama, mwenye rekodi nzuri ndani ya chama, mwenye kusimama kwa miguu yake bila kuvutwa mikono , mwenye siasa safi zisizo za majungu na vijembe. Tunamhitaji mtu mwenye elimu ya asili (Here I do not mean PhD, Masters or Bachelors), hapa namaanisha elimu ya utambuzi ambayo inamsadia kutokuwa mjivuni na Maringo. Awe ni mtu wa watu kweli, awe ni mtu mwenye ushawishi akisimama na Kuongea kweli aweze. Ujue unaweza ukawa fundi wa kuandika makala nzuri lakini ukashindwa kuwa mwenye ushawishi jukwaani. Hilo tuliangalie sana Makamanda.
BAVICHA haihitaji mtu ambaye kwake rekodi za kufukuzwa shuleni au vyuoni ndiyo anaona kuwa ni rekodi nzuri ya Ukamanda na kaziweka kwenye CV yake ya kuutaka uongozi BAVICHA, yaweza kuwa alikuwa akifukuzwa kwa sababu ya Ulevi au Umalaya (Who Knows?) Kwa hiyo wanachama na wapiga kura tuweni makini sana na hili.
Mwisho nipende kuwambia kuwa Msingi wa demokrasia ya dhati na Maendeleo huletwa na wenye nia njema na ujasiri, msingi huu ndio huwa chachu ya kuwafanya wanyonge waliokata tamaa kupata nguvu ya kuinuka na kuteta yao ya moyoni na hata kuchukua hatua. Msingi huu utaletwa na wasio na tamaa na wasiopenda sifa.
TUWENI MAKINI, CHAMA SIYO CHUMBA CHA KULALA KUWA KILA MMOJA ANAWEZA TANDIKA NA KULALA
J.K. Nyambeya
Mwanachama CHADEMA.
-- Salaam kwenu wanachama wa CHADEMA ambao ndio msingi wa chama hiki tokea ngazi ya Msingi hadi Taifa, salaam hizi nazitoa kwa heshima ya dhati kabisa kwenu Makamanda. Bwana Yesu Asifiweeeeee, Asalaam Alyakum...

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments