Jeshi la polisi mkoani Mara linamshikilia askari wake mmoja mwenye namba G.1420 Gwamaka mwakatundu kwa tuhuma za mauaji ya mwanamke mmoja,ambaye anadaiwa kuuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kamanda wa polisi mkoani Mara kamishina msaidizi wa jeshi la polisi ACP Philip Alex Kalangi,amesema mwili wa mwanamke huyo bi Angela Kigokola umekutwa ukiwa nje ya nyumba askari huyo ambaye ni shemeji wa marehemu katika mtaa wa mkinyerero kata ya Mwisenge katika manispaa ya Musoma mkoani Mara
Nao baadhi ya watu ambao wamefika kushuhudia tukio hilo , akiwemo mwenyekiti wa mtaa huo bw Ragita Nyamwero, wamesema mazingira yanaonyesha kuwa mauaji hayo yamefanyika ndani ya chumba cha askari huyo kisha mwili huo kutolewa na kutupwa nje ya nyumba hiyo kwa lengo la kuficha ukweli…… .bw Ragita Nyamwero-m/kiti wa mtaa Mkinyerero-Musoma na Bi Adira Tarimo-jirani
Mwili wa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 24 umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Mara mjini Musoma kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments