[wanabidii] HITORIA YA KABILA LA WAPARE

Saturday, August 09, 2014
Wapare wanaishi katika miteremko ya milima ya Upare Kaskazini, iliyopo Mashariki ya Milima ya Usambaa; na Kusini Mashariki mwa mlima Kilimanjaro. Kwa mujibu wa historia kutoka katika machapisho mbalimbali, lugha inayozungumzwa na watu wa eneo hili, inajulikana kama Chasu. Wenyeji wakaitwa Vaasu, hivyo kabila hilo lilijulikana k ama kabila la Waasu. Historia inaeleza kuwa katika Karne ya 18, Waasu walikuwa wenyeji wa Kenya eneo la Taita na Taveta. Lakini, baada ya kusikia habari za maajabu ya Kilimanjaro, walifanya mikakati ya kuhama ili waishi katika mteremko wa mlima huo. Waasu walipofika karibu na maeneo ya mlima wa ajabu, yaani Kilimanjaro, walielekea sehemu za Kaskazini ili waishi karibu na Kilimanjaro, wakiwa na matumaini makubwa ya kuishi huko. Tofauti na matarajio yao, walikutana na wenyeji wa eneo hilo, Wachaga. Hata hivyo, hawakukata tamaa, waliendelea kuweka mazingira ya kujenga himaya hayo. Wachaga walipoona wanaingiliwa, waliitana na kuanza kuwafukuza huku wakipiga makelele wakisema "wapare… wapare", ikiwa na maana wapige… wapige! Ili kuokoa maisha yao, Waasu walikimbia kuelekea sehemu za mteremko hadi eneo la Mwanga na Same, Kusini mwa mlima Kilimanjaro; ITAENDELEA.....

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments