[wanabidii] Gazeti la SANI laonywa kuhusu habari linazochapisha

Friday, August 15, 2014
SERIKALI imelionya gazeti la SANI kwa kuchapisha habari na picha zisizokuwa za kweli na kuzua hofu kwa wananchi.

Hatua hiyo inafuatia na gazeti hilo kuchapisha habari zilizokuwa na kichwa kisemacho ''EBOLA YATUA na kuonyesha picha za maiti bila kueleza kuwa sio za tukio lililotokea nchini.

Onyo hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Assah Mwambene wakati akiongea na waandishi wa habari.

"Sio vizuri na kuleta mizaha katika habari makini na zinazogusa maisha ya wananchi kama ugonjwa wa EBOLA kwa unasababisha hofu miongoni mwa jamii" amesema Mwambene.

Amesema kuwa hadi hivi sasa hakuna mgonjwa yoyote aliyeripotiwa kuwa na ugonjwa huo hapa nchini na wala haujafika.

Hata hivyo Mwambene ameongeza kuwa pamoja na kutokuwa na mgonjwa yoyote hapa nchini, Serikali imeshachukua hatua mbalimbali katika kukabiliana na ugonjwa huo endapo utaripotiwa kuingia nchini.

Ametaja hatua hizo ni Kutenga vituo maalum vya kuwapima wagonjwa watakaohisiwa kuwa na ugonjwa huo katika viwanja vya ndege na sehemu zote za kuingilia nchini.

---
JOVINA BUJULU

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments