Wadau hivi karibuni nilishuhudia vyombo vya habari vikinadi kuwa serikali ya Tanzania imeingia makubaliano na serikali ya kenya kuuziana mahindi kaisi cha tani 80,000 toka Tanzania.
Je , mahindi hayo yamekwishauzwa?.Ninachoelewa tayari bodi ya mazao mchanganyiko iko kwenye full operation maana walishapewa kinu cha iringa kusindika mazao ya Nafaka, huu ndiyo muda muafaka sasa wa bodi hiyo kufanya biashara ya kuuza unga ndani na nje ya nchi kupitia mikataba kama hii .
Aidha wafanyabiashara na wasindikaji wakubwa kwa wadogo nao waruhusiwe kuuza bidhaa za unga kwenda nje ya mipaka yetu, hii itakuza ujasiriamali nchini.
Kuna faida kubwa kuuza bidhaa zilizosindikwa kuliko kuuza malighafi! tutakuza uwekezaji kwenye sekta ya viwanda nchini.
~ ni ushauri tu~
Mboje, G.
Tanzania
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAJi0OxQm4NnqCWAUAHp13vCLGnKHE%3D2%3DVnBb8wHgJ7eBVTqDDg%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments