BUNGE MAALUM LA KATIBA LIKAE KWA WIKI MBILI NA SIO
MIEZI MIWILI
TAMKO LA JUKATA KUHUSU HAJA YA RATIBA MPYA YA
MCHAKATO WA KATIBA MPYA TANZANIA
1.0. UTANGULIZI
Tangu tarehe ya awali ya ratiba ya Mchakato wa Katiba Mpya Tanzania ipite bila kuipata Katiba, kumekuwa na ukimya wa muda mrefu bila mwongozo wowote madhubuti juu ya tarehe mpya za hatua zinazofuata za Mchakato huu adhimu na muhimu wa ustawi wa demokrasia, utawala bora, uwajibikaji na mshikamano ndani ya Nchi yetu. Ukimya huo umeleta ombwe kubwa katika Mchakato wenyewe na kusababisha kila mtu kusema lile aliloweza kusema huku kuhitilafiana baina ya makundi mbalimbali ndani na baina ya vyama vya Siasa na Makundi mengine ya Kijamii. Kwa uchunguzi wa JUKATA, hata ufa wa Mchakato kati ya wanaopendelea muundo wa Muungano wa Serikali mbili na wale wanaotaka serikali tatu ni sehemu ya mivutano ya Kisiasa inayotokana na wanasiasa kuendelea kujipima umaarufu wao kwa kutumia Katiba Mpya. Kukosekana kwa ratiba Mpya ya Mchakato pia kulipelekea mfarakano ndani ya Bunge Maalum baina ya makundi ya vyama vya Siasa ya UKAWA na Tanzania Kwanza huku kila upande ukijaribu kuitazama Katiba mpya kwa minajiri ya kufanikisha au kukwaza ushindi wao katika uchaguzi Mkuu ujao wa Mwakani, 2015.
Kutokana na ukweli kwamba muda kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 umekaribia sana, joto la kisiasa linazidi kupanda na tayari Taifa linakabiliwa na michakato mikubwa sita ya kitaifa katika kipindi kifupi cha miezi 15 tu iliyobaki hadi mwishoni mwa Oktoba 2015 ambapo ndipo Uchaguzi Mkuu utalazimika kufanyika kwa kuwa muda wa kukaa madarakani kwa viongozi wetu wa kuchaguliwa serikalini na Bungeni utakuwa umekwisha kikatiba. Michakato hiyo ni pamoja na:-
i) Uandikishaji wa vitambulisho wa Taifa unaofanywa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ulioanza mwaka 2013 na mpaka sasa umefanyika katika mikoa ya Dar Es Salaam, Zanzibar na Pwani pekee, huku Mikoa ya Lindi na Mtwara ikitarajiwa kuanza zoezi hilo mwezi mmoja ujao. Hadi sasa, hata theluthi moja ya nchi haijafikiwa na zoezi hilo na bado yapo mategemeo kuwa zoezi hili litakamilika mapema mwaka 2015, kwa mujibu wa ndoto za NIDA.
ii) Uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Kisheria mwezi Oktoba 2014 na ambao kwa jadi husimamiwa na ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), huku ukitanguliwa na uandikishaji wapiga kura unaojitegemea.
iii) Uandikishaji upya wa wapiga kura kwa mfumo wa kielektroniki yaani Biometric Voter Registration (BVR), unaotarajiwa kufanyika kuanzia mwezi Septemba 2014 kwa awamu za kikanda ukisimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Uandikishaji huu umepangwa kufanyika kwa siku angalau 14 kila kituo kwa kila Kanda, labda kukiwa na ulazima wa kuongeza muda.
iv) Upigaji wa kura ya maoni kuamua hatma ya Katiba Mpya unaofikiriwa kufanyika mwezi Machi 2015 na kuendeshwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Kabla ya uchaguzi huo, kutakuwa na muda wa kuendesha elimu ya uraia na elimu ya mpiga kura ambayo hata hivyo inaonekana kutopewa muda na kipaumbele cha kutosha katika mipango rasmi ya Mchakato huo. Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Kura ya Maoni, 2013 kutapaswa kuwa na
muda wa kufanya kampeni kwa makundi ya Kamati zitakazojisajili ama kupigia debe kura ya NDIYO au kura ya HAPANA.
v) Uhakiki wa daftari la kudumu la Wapiga kura unaofikiriwa kufanyika mnamo mwezi Juni/Julai kama sehemu ya kutimiza matakwa ya sheria za Uchaguzi zinazotaka daftari hilo kuhakikiwa mara mbili ndani ya miaka mitano kati ya uchaguzi mmoja na mwingine. Lengo la uhakiki huu itakuwa ni kuondoa wafu katika daftari pamoja na kushughulikia waliopoteza kadi za mpiga kura.
vi) Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba 2015, kuchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar, Wabunge wa Bunge la Tanzania na Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na Madiwani katika Halmashauri zote za Tanzania Bara.
Kutokana na na michakato na mambo hayo makuu sita muhimu hapo juu ambayo yanatakiwa kufanyika ndani ya miezi 15 tu ijayo huku mengine yakiratibiwa na kuendeshwa na taasisi zilezile na kuwahusisha wananchi walewale na rasilimali za Taifa hilihili ambazo ni finyu JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tunapendekeza masuala muhimu mawili kama hatua ya kupunguza matumizi mabaya ya muda, vifaa na rasilimali fedha tukiwa na lengo la kuongeza ufanisi wa mazoezi haya pia :-
a) Kuahirisha uchaguzi wa serikali za mitaa ili ufanyike pamoja na uchaguzi mkuu mwezi Oktoba 2015 na kusimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) kwa kutumia daftari la Kudumu la Mpiga kura watakaloliandaa mwaka huu 2014 na kulihakiki katikati ya mwakani 2015.
b) Kusimamisha mchakato wa kuandika katiba mpya mpaka mara baada ya uchaguzi Mkuu wa 2015.
c) Kwa sababu ya pendekezo (b) hapo juu, kufupisha Mkutano ujao wa Bunge Maalum la Katiba unaoanza tarehe 05 Agosti 2014 mjini Dodoma kutoka siku sitini (60) alizowaongezea Mheshimiwa Rais,Bunge hilo likutane kwa kipindi cha wiki mbili pekee ili kufanya kazi moja tu muhimu ya kujadili, kuridhia na kupendekeza ratiba mpya ya Mchakato
wa Katiba Tanzania. Ratiba hii itapaswa kuwasilishwa na serikali kama
Rasimu ya Ratiba baada ya HOJA MAHSUSI ya kulitaka Bunge Maalum kupokea na kujadili Rasimu ya Ratiba Mpya ya Mchakato wa Katiba Mpya Tanzania. Hoja Mahsusi inaweza kutoka serikalini au kutolewa na Mjumbe yeyote wa Bunge Maalum. Baada ya kutolewa hoja hiyo mahsusi, Waziri mwenye dhamana ya Mchakato wa Katiba atawasilisha RASIMU YA RATIBA MPYA YA MCHAKATO WA KATIBA MPYA TANZANIA. Hoja hiyo itajadiliwa kwa siku zisizozidi tano na ratiba kupitishwa kama pendekezo kwa Bunge la Tanzania ambalo ndilo litakuwa na Mamlaka ya kupokea na kupitisha hoja hiyo kama sehemu ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 (kama ilivyorejewa hadi mwaka 2014).
2.0. PENDEKEZO LA RATIBA MPYA YA MCHAKATO WA KATIKA MPYA TANZANIA
NAMBA | SHUGHULI | | MUDA |
| | | |
1 | Bunge Maalum la | Katiba kukutana na | 05 – 15 Agosti,2014 |
| kupokea, kujadili na kuridhia hoja ya haja | | |
| ya RATIBA MPYA YA MCHAKATO | | |
| WA KATIBA TANZANIA | | |
| | | |
2 | Bunge Maalum la | Katiba kuahirishwa | 16 Agosti, 2014 |
| rasmi hadi baada ya Uchaguzi Mkuu wa | | |
| 2015 | | |
| | | |
3 | Bunge la Jamhuri | ya Muungano wa | Novemba, 2014 |
| Tanzania kupokea rasmi HOJA ya | | |
| pendekezo la kuahirishwa kwa Mchakato | | |
| wa Katiba Mpya hadi baada ya Uchaguzi | | |
| Mkuu, 2015 na kupokea Muswada wa | | |
| Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya | | |
| Katiba, 2014 ikiwemo kuingiza ratiba | | |
| (roadmap) mpya katika Sheria. | | |
| - Muhimu pia kurejesha kifungu cha | | |
| 37 cha Sheria ya Mabadiliko ya | | |
| Katiba hadi 2012 kuibakiza Tume | | |
| katika wajibu | wa kuwepo katiba | |
| | | |
Bunge Maalum la Katiba kukutana kwa | Novemba | – | Disemba, | |||
| ajili ya kuendelea kujadili Rasimu ya | 2016 | | | ||
| Katiba Mpya iliyoandaliwa na Tume ya | | | | ||
| Mabadiliko ya Katiba, 2013 | | | | | |
| | | | |||
8 | Bunge la Katiba Kupitisha katiba mpya | | Januari-Juni, 2017 | |||
| | | | |||
9 | Wananchi kupiga kura ya maoni | | Julai – Novemba,2017 | |||
| | | ||||
10 | Katiba mpya kutangazwa, kutiwa saini na | 1 Januari,2018 | ||||
| kuzinduliwa rasmi | | | | | |
| | | ||||
11 | Kutunga na kurekebisha sheria 50 kusaidia | Januari- Juni,2018 | ||||
| utekelezaji wa Katiba Mpya | | | | | |
| | | ||||
12 | Kutunga katiba ya Tanganyika na | Julai-Desemba, 2018 | ||||
| Mabadiliko makubwa katika Katiba ya | | | | ||
| Zanzibar | | | | | |
| · Kuunda Kamati ya | Mabadiliko | ya | | | |
| Katiba | | | | | |
| · Kukusanya maoni ya wananchi | | | | | |
| · Kuunda bunge la katiba | | | | | |
| · Kupitisha katiba | | | | | |
| · Kupiga kura ya maoni | | | | | |
| · Kutangaza katiba mpya | | | | | |
13 | Ukamilishaji wa uundaji vyombo muhimu | Januari- Oktoba,2019 | ||||
| vya Kikatiba na Kisheria kwa mujibu wa | | | | ||
| Katiba Mpya | | | | | |
| | | | | ||
14 | Uundaji upya wa Majimbo ya uchaguzi na | Novemba | – | Disemba, | ||
| taratibu mpya za uchaguzi | | | 2019 | | |
| | | ||||
15 | Uchaguzi Mkuu kama sehemu ya | Agosti-Oktoba,2020 | ||||
| utekelezaji wa Katiba Mpya | | | | | |
| | | | | ||
16 | Marekebisho ya kisheria kulingana na | Januari | – | Disemba, | ||
| matatizo yaliyojitokeza | wakati | wa | 2021 | | |
| uchaguzi Mkuu 2020 | | | | | |
| | | | | | |
3.0. MAPENDEKEZO JUU YA HAJA YA MABADILIKO (MINIMUM REFORMS) YA MASHARTI MBALIMBALI YANAYOHUSIANA NA UCHAGUZI KATIKA KATIBA YA TANZANIA NA KATIBA YA ZANZIBAR PAMOJA NA SHERIA ZA UCHAGUZI
Kutokana na hoja yetu ya haja ya kusogeza uchaguzi wa serikali za Mitaa ili ufanyike wakati mmoja na Uchaguzi Mkuu, hoja nyingine ya kuahirisha Mchakato wa Katiba Mpya hadi baada ya uchaguzi Mkuu ujao, ipo haja ya kufanyika mabadiliko kwenye Masharti mbalimbali ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na Sheria kadhaa za uchaguzi na zile zinazohusu usimamizi na ulinzi katika mazoezi ya uchaguzi ili kupunguza au kuondoa kabisa malalamiko ya wadau wa uchaguzi vikiwemo vyama vya Siasa juu ya usimamizi, uratibu na uendeshaji wa zoezi zima la uchaguzi nchini. Katika kufikia azma hiyo, JUKATA tunapendekeza yafuatayo:-
3.1. MABADILIKO KATIKA BAADHI YA MASHARTI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 1977
· Kubadili muundo na uteuzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
· Kuingiza mgombea binafsi katika chaguzi za ngazi zote
3.2. MABADILIKO KATIBA BAADHI YA MASHARTI YA KATIBA YA ZANZIBAR, 1984
· Kutazama upya maeneo yanayokataza ufunguaji wa Mashauri ya rufani kwa mambo yanayohusu haki za binadamu katika uchaguzi na ambayo yamekosa majibu ndani ya ngazi zote za mahakama za Zanzibar
· Kupitia vifungu vinavyohusu muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuvitafakari upya kwa minajiri ya kuimarisha zaidi muundo huo
3.3. SHERIA ZINAZOHITAJI KUTAZAMWA UPYA NA KUFANYIWA MABADILIKO
· Sheria ya Uchaguzi
· Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
· Sheria ya Gharama za Uchaguzi
· Sheria ya Usajili wa Vyama
4.1. MUUNDO WA UTEKELEZAJI WA MABADILIKO YA KATIBA NA SHERIA
Mabadiliko kama haya yatahitaji uwazi na uwajibikaji ili yasilalamikiwe. Ili kuwezesha uwazi na ushirikishi katika mchakato wa mabadiliko haya JUKATA tunapendekeza iundwe kamati ya ufundi ya vyama vyote vilivyoko bungeni itakayoshirikiana pia na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Msajili wa Vyama vya Siasa na Tume ya Uchaguzi kuandaa miswada yote na kuipeleka bungeni katika bunge litakalokaa Novemba 2014 kwa ajili ya kusomwa kwa mara ya kwanza kabla ya wadau kutoa maoni yao na kupitishwa rasmi mwezi Februari, 2015.
5.0. HITIMISHO
JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tunatoa tamko hili baada ya kufanya tathmini ya kina juu ya mchakato wa Katiba Mpya ulipofikia kwa jicho la michakato mingine inayoendelea nchini. Nia yetu ni kuhakikisha kuwa michakato hii inapata muda wa kutosha na kufanya demokrasia ya ushiriki ipate nafasi katika michakato hii, hasa ule wa Katiba Mpya. Itakuwa ni busara kwa vyombo na taasisi zilizopewa majukumu katika tamko hili kupokea majukumu hayo kwa moyo mkunjufu na kuwa tayari kuyatekeleza bila kuzidi kupoteza muda kwa mabishano mengine kama ilivyotokea mwanzoni mwa mchakato unaoendelea wa Katiba Mpya nchini. Mabishano mengi ingawa yanaleta afya kwa mchakato pia huwa na athari mbaya ya kuchelewesha utekelezaji wa hatua husika. Itafaa sana kuweza kukubaliana mambo ya msingi yaliyopendekezwa na kuanza utekelezaji kwa kuwa kwa muda uliobaki haiwezekani kutimiza ndoto zote tulizonazo kwa ufanisi unaohitajika na bila kuleta madhara katika ubora wa baadhi ya Michakato.
Kwa umuhimu wa haja ya Mabadiliko ya Kikatiba na Kisheria kuhusu maeneo yenye athari kwa uchaguzi, JUKATA tumeteua Jopo la Wanasheria na Wataalamu ili kuandaa pendekezo la Masharti yote ya Katiba na Sheria yatakayoathiriwa na mabadiliko hayo na kupendekeza jinsi yatakavyofanana katika sura zake Mpya baada ya mabadiliko. Jopo hilo litaongozwa na Wakili Armando Swenya wa JUKWAA LA KATIBA TANZANIA.
Imetolewa na kutiwa Saini kwa niaba ya JUKATA na;
Deus M Kibamba
Mwenyekiti
25 Julai, 2014
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments