[wanabidii] SERIKALI YAKANUSHA KUTOKUWEPO KWA UPUNGUZWAJI WA MAFAO YA PENSHENI YA PSPF NA LAPF

Sunday, July 27, 2014
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imekanusha tamko liliotolewa na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisiza Elimu (THTU) na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) la kudai kwamba kuna mpango wa kupunguza Mafao ya Pensheni ya wanachama mifuko ya LAPF na PSPF.

Akizungumza Dar es Salaam leo Kamishna wa Kazi wa Wizara ya Kazi na Ajira, Saul Kinemela alisema taarifa hizo sio za kweli ambazo kwa namna nyingine zinalenga kupotosha umma.

"Tunaomba wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii na umma kwa ujumla kuwa kinachoendelea ni majadiliano na wadau wa sekta ya hifadhi ya jamii yenye lengo la kuboresha mafao ya wastaafu" alisema Kinemela.

Alisema kuwa Chama cha Walimu Tanzania ( CWT) na THTU wakiwa ni wadau sekta ya hifadhi ya jamii wanayo haki ya kikatiba ya kukutana na kujadiliana masuala mbalimbali yakiwamo ya sekta ya hifadhi ya jamii.

Alisema Serikali inachukua fursa hiyo kuwatoa hofu wastaafu na wanachama wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii.

"Tunaomba wadau wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa watulivu na kujiepusha na maneno yoyote ya upotoshwaji na mwisho kuwachanganya wanachama na hivyo kupunguza ufanisi wa kazi na utendaji," alisema Kinemela.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments