[wanabidii] Mwaliko kwenye Kongamano Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 27/07/2014

Thursday, July 24, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mwaliko kwenye Kongamano Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 27/07/2014

Kwa niaba ya Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), napenda kukukaribisha kwenye Kongamano la kujadili mchakato wa kupata Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kongamano hilo litafanyika tarehe 27 Julai 2014 siku ya Jumapili kuanzia saa 8 mchana ndani ya ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kongamano hilo litarushwa moja kwa moja na Star TV. 


Mada kuu ya kongamano hilo ni, "Tujadili na Kutafakari Mchakato wa Katiba Mpya kwa Manufaa ya Taifa Letu". 


Tunapenda kuchukua fursa hii kwa heshima kubwa kuwakaribisha wananchi wote ili wawe miongoni mwa watu watakaotoa mchango wao mkubwa katika mchakato wa kuleta maridhiano ya kitaifa kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya ya taifa letu la Tanzania. 


Tutanguliza shukrani zetu za dhati kwa ushiriki wako kwenye kongamano hili. 


Ndimi


Imetolewa na Bw. Faraja Kristomus. (Katibu – UDASA).

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments