MAMBO 10 YA KIJINGA..
10. Nikiwa na miaka 9 au 10 nimewahi kulala bafuni baada kuona uvivu kwenda chumbani baada ya kumaliza kupiga mswaki
9. Niliwahi kupitiliza na daladala kituoni hadi mwisho baada ya kuona uvivu kuamka kwenye siti. Nilitakiwa kushuka Makonde nikapitiliza hadi Tegeta ilikuwa saa saba usiku nikakosa gari ya kurudi nikalala stendi hadi saa kumi na moja.
8. Nimewahi kulala kwenye mtihani wa taifa wa form two kwa saa zima, mtihani ulikuwa wa saa moja na dakika 15. Ulikuwa ni mtihani wa French na nilikuwa nauchukulia ni mtihani mwepesi sana, baada kuamka nilishindwa kujibu hata swali moja. Nilipata F ingawa nilikuwa naongoza darasani.
7. Niliwahi kunywa dawa ya kikohozi ( mkojo wa punda ) chupa nzima ili nisisumbuliwe kunywa kila siku hadi iishe. Nililewa karibia siku tatu mfululizo ( usiige hii sio pombe)
6. Niliwahi kuzimia kwa dakika kama mbili nilipoanguka nikiwa nacheza mpira, nilipoamka nikagundua nimebebwa nilirudi kuzimia ili waendelee kunibeba. Mwalimu aliogopa nikapelekwa hospitali wakaniweka chini ya uangalizi kwa siku tatu (shenzi nilitamani kusema ukweli)
5. Nimewahi kugeuza boxer nje ndani baada kuivaa kwa siku sita mfulululizo, niliona uvivu kuifua nikaamua kuigeza nje ndani kupunguza makali.
4. Nimewahi kupiga simu kwa mmiliki wa bar ili amuite mhudumu arudi kwenye meza yetu ili tubadilishe oda, mhudumu alikuwa kaunta kama mita nne hivi.
3. Hii imetokea juzi tu, nimevunja sahani kama sita hivi ili wife asizikute chafu baada kuzitumia alipokuwa kasafiri
2. Niliwahi kufunga TV kwenye ceiling ili niweze kuangalia nikiwa nimelala, nilipogundua napitwa na baadhi ya matukio nikaamua niongeze TV kwenye kila angle mpya ninayogeukia, sasa hivi tuna TV nane chumbani na zote zime connectiwa kuonesha kitu kimoja. Wife anatafuta therapist anadhani nahitaji msaada.
1. Hii ndio inaniuma zaidi, hadi leo officially natambulika kwa jina la mdogo wangu baada ya kuona uvivu kumrekebisha mwalimu wangu aliyekuwa ananifanani na mdogo wangu. Hii imesababisha nibadilishe documents zote zifanane na majina yangu ya kwenye vyeti vya shule.
Unadhani kuna mtu mvivu kuliko mimi hapa Afrika mashariki na kati?
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments