[wanabidii] MAKAO MAKUU YA BUTIAMA NI WAPI?

Sunday, July 20, 2014
Ndugu wanabidii binafsi nimeshangazwa sana baada ya kuamua kuzuru kijiji cha BUTIAMA mwezi juni kwa malengo makuu mawili 1. ilikuwa kutembelea kaburi la baba wa TAIFA kwani tangu mwaka 1999 wakati wa mazishi yake nilikuwa sijapata kurudi huko ambayo ni sambamba na kuwapeleka watoto wangu ambao wengine wana zaidi ya umri wa miaka 26 lakini hawakuwahi kufika eneo hilo la kihistoria, 2. nilipanga kutembelea ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo ambayo wapi ijengwe iliwahi kupata nafasi kwenye vyombo mbali mbali hapa nchini. Nilipouliza wenyeji wakasema DED anadai miundo mbinu isiyofaa, Hapo nikajiuliza hivi serikali huwa inaweka mipango yake sambamba na malengo yaliyopo au? wazo lingine lililoniijia huyu DED angepangiwa BUSEGA (Nyashimo) au KYERWA (Rwenkorongo) angehamia baada ya miongo mingapi? RAI YANGU kwa serikali ni kwamba maeneo muhimu kama BUTIAMA waweke viongozi wazoefu wa vijijini.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments