Kampuni ya TTCL Yatoa Zawadi ya Eid El Fitr kwa Yatima Dar
[caption id="attachment_48993" align="aligncenter" width="617"]<img src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/07/IMG_0876.jpg" alt="Wawakilishi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mama Theresa kilichopo Mburahati, wakipokea msaada wao toka kwa Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL." width="617" height="480" class="size-full wp-image-48993" /> Wawakilishi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mama Theresa kilichopo Mburahati, wakipokea msaada wao toka kwa Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.[/caption][caption id="attachment_48991" align="aligncenter" width="584"]<img src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/07/IMG_0852.jpg" alt="Vikundi vya Watoto Yatima vya Mama Theresa kilichopo Mburahati, Kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni na Kituo cha Chakuwama cha Sinza katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea zawadi zao jijini Dar es Salaam." width="584" height="480" class="size-full wp-image-48991" /> Vikundi vya Watoto Yatima vya Mama Theresa kilichopo Mburahati, Kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni na Kituo cha Chakuwama cha Sinza katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea zawadi zao jijini Dar es Salaam.[/caption][caption id="attachment_48990" align="aligncenter" width="531"]<img src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/07/IMG_0858.jpg" alt="Wawakilishi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mwandaliwa cha Mbweni wakipokea msaada wao toka kwa Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL." width="531" height="480" class="size-full wp-image-48990" /> Wawakilishi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mwandaliwa cha Mbweni wakipokea msaada wao toka kwa Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.[/caption]
<strong>KAMPUNI</strong> ya Simu Tanzania (TTCL) imetoa msaa wa vyakula kwa vituo vitatu vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu vya jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuvisaidia viweze kusherehekea vizuri siku kuu ya Eid El Fitr.
Msaada huo wenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 3 umekabidhiwa na Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, ambaye alisema utaratibu huo ni wakawaida kwa kampuni yao kusaidia makundi na taasisi na idara anuai kwa masuala ya kijamii.
Bi. Mwakalebela alivitaja vituo ambavyo vimekabidhiwa msaada huo ni pamoja na Kituo cha Watoto Yatima cha Mama Theresa kilichopo Mburahati, Kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni na Kituo cha Chakuwama cha Sinza vyote vya jijini Dar es Salaam.
"…Msaada huu ni maalum kwa ajili ya kusherehekea siku kuu ya Eid El Fitr, jambo hili la leo ni utaratibu wa kampuni ya TTCL kusaidia makundi, taasisi na idara mbalimbali kuhusu mambo yanayohusu maendeleo na ustawi wa jamii," alisema Bi. Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura.
Msaada uliotolewa kwa vituo hivyo ni pamoja na mchele, mafuta ya kupikia, sukari, unga, unga wa sembe, maharage pamoja na katoni za juisi za maboksi.
Kwa upande wao wawakilishi wa vituo hivyo waliishukuru Kampuni ya TTCL kwa uamuzi wake wa kuwakumbuka watoto yatima ili nao waweze kusherehekea vizuri siku kuu ya Eid El Fitr kama ilivyo kwa familia nyingine majumbani.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments