Ndugu zangu ,
Nimeona baadhi ya watu wakisambaza ujumbe kwenye mitandao haswa facebook kuhusu tatizo la mpesa la kampuni la Vodacom lililotokea siku kadhaa zilizopita na ambalo limeshakishwa .
Msambazaji wa ujumbe huo anayejiita mwandishi wetu anasema mpango ulisukwa na vigogo 2 wa ccm wenye hisa nyingi kwenye kampuni hiyo ya Vodacom , baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom ili kuvuruga mtandao wa mpesa wao waweze kupata fedha za kuhudumia bajeti .
Napenda kusema kwamba hata na mimi nilikumbwa na tatizo la mpesa , nilijaribu kutoa hela kutoka kwa wakala wa mpesa , nilituma ujumbe lakini sikupata majibu na hata wakala wangu hakupokea ujumbe wowote ndio baadaye kuuliza tuliambiwa kuna shida , lakini nilipojaribu kununua umeme na kulipia huduma nyingine ilifanyakazi .
Huduma iliporudi sikuona hela yoyote kupungua wala zaidi ya zile nilizonunulia huduma mbalimbali .
Huduma za mawasiliano hazijaikumba Tanzania tu , hata Zambia kampuni ya Airtel Ilipatwa na tatizo hili lakini wao waliomba radhi toka jana asubuhi , Malawi Kampuni yao ya mawasiliano ilipata tatizo hili , Botswana na Zimbabwe kulikuwa na shida kama hii .
Tukirudi kwenye suala la Bajeti , Bajeti ni mpango wa mapato na matumizi ya serikali kutokana na Vyanzo vyake ambavyo vingi vinajulikana na hawa VODACOM ni moja ya vyanzo vya mapato ya serikali kwa sababu kampuni inalipa kodi mbalimbali kupitia kwa wafanyakazi wake , huduma zake mbalimbali kama za MPESA na nyingine nyingi .
Tatizo la VODACOM ni kutokutoa taarifa kwa wateja wao mapema na hata huduma iliporudi kuendelea kukaa kimya na hapo ndipo wengine walipopata fursa ya kuandaa Ujumbe unaosambaa mitandaoni sasa hivi .
Ndugu zangu tujitahidi kuondoa siasa kwenye masuala ya kitaalamu na ufundi kama haya , mawasiliano ni suala nyeti na muhimu sana kwa usalama wa taifa , tunapoleta siasa na upotoshaji kwenye suala kama hili tujue tumekusa usalama wa taifa moja kwa moja .
Kampuni za simu kama VODACOM na wengine wawe na utamaduni wa kutoa taarifa kwa wateja wao inapotokea shida yoyote , kwani kuna shida gani kutuma ujumbe mfupi tu kwa wateja wao kwamba kuna shida hii na hii kuliko kuacha watu watunge yao ?
Institut d'études de sécurité - SA
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments