[wanabidii] Tanzia; TGNP Mtandao Yampoteza Mwanachama Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Kwanza

Wednesday, June 04, 2014

Tanzia; TGNP Mtandao Yampoteza Mwanachama Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Kwanza
 
1940 - 2014
TGNP Mtandao tumepata pigo kubwa  kwa kumpoteza mwanaharakati na Mwenyekiti wa kwanza wa shirika, aliyefariki Juni 2, 2014 Ubungo Msewe Dar es Salaam.
Fides Chale alikuwa ni mwalimu na kiongozi aliyegusa maisha ya wengi hapa Tanzania, Mwanaharakati mtetezi wa haki za wanawake, wasichana na makundi mengine yaliyoko pembezoni.
Dada Fides amekuwa mtu wa watu, mcheshi, mwenye upendo, utu, huruma, mpole, mwenye sura ya kutabasamu muda wote hata alipokuwa kwenye hali ya ugonjwa.
Tunapoombeleza kumpoteza dada yetu Fides Chale, tunasheherekea maisha yake  mchango wake mkubwa jinsi alivyojitolea kwa hali na mali kulilea shirika tangu lilipoanza  hadi mauti yalipomfika. Fides Chale  alishika uongozi  TGNP wakati shirika likiwa changa, kuliwekea misingi imara na endelevu wa kiuongozi, kiutawala, na  mfumo mzuri wa kubadilishana uongozi unaoendelea hadi leo.
Mipango ya mazishi inaendelea nyumbani Ubungo Msewe. Alhamis 05/06/2014 ibada itafanyika katika Kanisa Katoliki Mt. Petro  Osterbay na kufuatiwa na mazishi katika makaburi ya Kinondoni.
Imetolewa na
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
TGNP Mtandao

____________________________________________________
Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments