Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014....
1. Je unajua kuna uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa?
2. Je unajua ni nani utamchagua kama Mwenyekiti wako wa serikali ya kijiji au serikali ya mtaa?
3. Je unajua ni nani utamchagua kuwa mjumbe wa serikali ya kijiji au serikali ya mtaa?
4. Je ulijiandikisha kupiga kura? Kama ulijiandikisha unajua kadi yako ilipo?
Au unasubiri kulaumu, kulalamika na kukosoa?
Jitazame na jimulike mwenyewe. Kwa kila jibu utaona kama wewe ni sababu ya tatizo au suluhisho.
Nchi hii haiwezi, narudia HAIWEZI kuendelea bila kuwa na viongozi makini na wenye uwezo ngazi za vijiji na mitaa. Ni lazima tuimarishe uongozi chini.
Imebaki miezi michache kabla ya kufikia uchaguzi. Vyama vya siasa vitakurupuka na kuanza 'kutafuta' wagombea. Ni wachache sana watagombea kwa sababu wanaweza.
Wengi watagombea kwa sababu tu wametafutwa, kuna nafasi za kugombea au hakuna mtu mwingine bora zaidi wa kugombea. Wengi zaidi watagombea kwa ajili ya maslahi binafsi.
Kutokushiriki kwako kutasaidia kundi la wagombea wa kutafutwa au kujaza nafasi na kwa ajili ya maslahi kushinda.
Hatuwezi wote kukimbilia ubunge ili tuitwe waheshimiwa! Ili tupate posho na tupige madili. Ili tutajirike haraka haraka. Ili tupate nafasi za mbele kwenye sherehe na misiba!!
Ni vyema kama kweli tuna nia ya dhati kuleta maendeleo katika nchi yetu tukaelekeza nguvu kwenye ngazi za chini za uongozi. Kama tuna misingi imara basi ni wazi nafasi za uongozi za juu zitaimarika. Wabunge na mawaziri watawajibika zaidi kwa wananchi. Rasilimali zetu zitasimamiwa vizuri zaidi. Na faida nyingine nyingi tu.
#5 Je unamjua Mwenyekiti wako wa serikali ya Kijiji au Mtaa?
#6 Je unawajua wajumbe wa serikali yako ya Kijiji au Mtaa?
#7 Je umewahi kupiga kura?
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments