[wanabidii] DENI LA TAIFA 2014/2015

Tuesday, June 17, 2014

DENI LA TAIFA

1. Mheshimiwa Spika, Deni la Taifa limeongezeka kwa kasi kubwa sana, hali ambayo inatishia ustawi wa taifa kama halitasimamiwa kwa umakini na haraka. Hotuba ya Waziri wa Fedha inaonesha kwamba hadi kufikia Machi 2014, Deni la Taifa lilifikia shilingi trilioni 30.563 ikilinganishwa na shilingi trilioni 23.674 la Machi 2013. Hili ni ongezeko la takribani trilioni 7 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 29 kwa kipindi cha mwaka mmoja tu.

2. Mheshimiwa Spika, hili ongezeko la mikopo ya takribani shilingi trilioni 7 kwa mwaka mmoja tu, halijawahi kutokea katika historia ya nchi yetu. Ongezeko hili la takribani trilioni 7 ni sawa na bajeti nzima (full budget) ya mwaka 2008/9 ambayo ilikuwa ni shilingi trilioni 6.839. Ikumbukwe kuwa mwaka 2008/9 ni miaka mitano tu iliyopita. Ukopaji wa namna hii unatishia uchumi na usalama wa nchi.

3. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti za Benki Kuu na hotuba za bajeti za miaka iliyopita za Mawaziri wa Fedha, deni la Taifa limeongezeka kwa kasi kutoka shilingi trilioni 9.3 mwaka 2007/8 hadi shilingi trilioni 30.6 mwaka 2013/14. Hii ni wazi kuwa deni liliongezeka kwa kiasi cha shilingi trilioni 21.3. Serikali imelipa shilingi trilioni 4 na kufanya fedha zilizokopwa kuwa jumla ya shilingi trilioni 25.3 katika kipindi hicho cha miaka saba tu. Huu ni ukopaji hatarishi kwa uchumi wa taifa letu.

4. Mheshimiwa Spika, licha ya deni hili kuwa hatarishi kwa uchumi wa Taifa, Serikali bado inatajaria kuongeza deni hilo kwa kukopa shilingi trilioni 4.3 kama ilivyoainishwa katika bajeti ya mwaka 2014/15.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeonesha kushindwa kulipa deni hilo kwa kutumia vyanzo vyake vya mapato, badala yake imekuwa ikikopa ili kulipa deni. Mfano hotuba ya bajeti ya mwaka 2014/15 imeonesha kuwa katika shilingi trilioni 1.8 zilizokopwa katika soko la ndani, zaidi ya shilingi trilioni 1.1 zilitumika kulipa madeni ya hati fungani wakati shilingi trilioni 0.69 tu ziliwekwa kwenye miradi ya maendeleo. Hiki ni kiashiria cha karibu sana kwa serikali kufilisika.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments