[wanabidii] Wabunge na Wizara ya Nishati na Madini

Friday, May 30, 2014
Ninaangalia Bunge hapa, na mpaka sasa wabunge wanne wote kupitia CCM wamechangia. Wameongea kwa hisia zinazojielekeza katika mafanikio makubwa ya wizara hiyo hususani Waziri wake, Prof Muhongo.

Lakini hoja zao zote zimebaki kumsifia Profesa Muhongo na kutamka "hakuna wa kukufanya ujiuzulu", wengine wanasema "wanaokupinga hawatafanikiwa" na kauli nyingi za aina hiyo.

Binafsi ninaziona kauli hizo kwa mtazamo huu ulio binafsi.
1. Wabunge husika hawajaelewa msingi wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo, hivyo kukosa cha kuchangia isipokuwa kumsifia Muhongo ambaye tayari na yeye alishajisifia jana, wakati akiwasilisha.
2. Inawezekana kuna mambo yanafichwa ili kuikoa wizara hiyo, na kwa maana hiyo serikali. Kwa sababu, kuna maana gani kwa Mbunge kutumia muda wake kumsifia waziri tu na kushindwa kujielekeza kwenye bajeti inayowafanya wawemo bungeni leo wakilipwa posho zinazotokana na kodi za wananchi?
Mnaoliangalia Bunge mnasemaje?

Dah! Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

Share this :

Related Posts

0 Comments