Telegrams "NISHATI"
Simu: +255-22-2117156-9
Nukushi: +255-22-2111749
Barua pepe: ps@mem.go.tz
5 Barabara ya Samora Machel,
S. L. P. 2000,
11474 DAR ES SALAAM
TAARIFA KWA UMMA
TAARIFA GAZETI LA TANZANIA DAIMA HAZINA UKWELI
Mnamo Mei 14, 2014 gazeti la Tanzania Daima toleo nambari 3449 lilichapisha taarifa yenye kichwa cha habari "JK AOMBWA KUMTIMUAMUHONGO". Gazeti hilo lilidai kuwa Waziri wa Nishati na Madini ProfesaSospeter Muhongo anadhalilisha taifa kwa kugawa madini kwa wageni na kuwaacha wazawa wakisotea gharama za ushuru zilizopandishwa hadi Dola 10,000 za Kimarekani. Taarifa hiyo inapotosha umma na wala si sahihihata kidogo kwani Profesa Muhongo hajawahi kutoa vitalu vya madini kwawageni tangu alipoingia madarakani mwaka 2012.
Pia, taarifa hiyo ilidai kuwa Profesa Muhongo amebuni mbinu ya kukwamisha wazawa kwa
kupandisha gharama za leseni kutoka Dola za Kimarekani 100 hadi 10,000 kwa mwaka. Taarifa hii si sahihi kabisa kwanihakuna leseni inayotozwa Dola za Kimarekani 10,000. Marekebisho yaliyofanyika katika ada ya leseni ni kama ifuatavyo:-
Leseni za utafiti mkubwa wa madini imeongezeka kutoka Dola za Kimarekani 100 hadi 300 wakati leseni ya uchimbaji mkubwa wa madiniimeongezeka kutoka Dola za Kimarekani 2,000 hadi 5,000.
Leseni ya uchimbaji wa madini wa kati imeongezeka kutoka Dola zaKimarekani 1,000 hadi 2,000. Aidha, leseni kwa ajili ya wachimbaji wadogoimeongezeka kutoka shilingi za kitanzania 20,000 hadi 50,000.
Sababu za kupandisha viwango hivyo ni kushuka kwa thamani ya shilingi na ada za awali kupitwa na wakati kwani zimekuwa zikitumika kwa mudamrefu takribani miaka kumi iliyopita.
Pia, lengo la Serikali ni kupunguzawachimbaji waliokuwa wanatumia mwanya wa ada ndogo iliyowapa fursa ya kuhodhi maeneo makubwa bila kuyafanyia kazi.
Ikumbukwe pia kwamba madini ni chanzo muhimu cha mapato yaSerikali. Hivyo, viwango vipya vimelenga kuongeza mapato ya Serikali nakurejesha heshima ya leseni za madini. Aidha, viwango hivyo vipya vya adaza leseni ni vya ushindani kimataifa.
Kwa mfano nchi ya Zimbabwe inatoza Dola za Kimarekani 500,000 kwaleseni ya utafiti mkubwa wa madini ya Platinum; na jimbo la Victoria huko Australia linatoza Dola za Kimarekani 500 kwa leseni ya utafiti mkubwa wa madini. Ni wazi kuwa viwango hivyo vipo juu ukilinganisha na viwango vyahapa nchini.
Kwa hakika tunasikitishwa na taarifa zilizotolewa na gazeti hili ambazolengo lake ni kumchafua Waziri Muhongo, pamoja na taswira ya Wizara ya Nishati na Madini kwa ujumla. Ninaomba kuwakumbusha Waandishi wahabari wenzangu kuzingatia maadili na miiko ya uandishi wa habari kwa kuhakiki taarifa zao kabla ya kuzitoa na hata kupata maelezo ya upande wa pili badala ya kuandika habari zinazoegemea upande mmoja tu. Pia nawakumbusha kwamba Wizara ya Nishati na Madini kupitia Ofisi ya Mawasiliano ipo wazi na tayari kushirikiana na vyombo vya habari na kwa kila mwenye maswali ama maoni anaweza kuwasiliana na ofisi ya Mawasiliano wakati wowote ili kupata taarifa sahihi ili kuepuka kuandika habari za uzushi na uchechezi usiokuwa na tija kwa taifa letu!!!!
Badra Masoud
Msemaji wa Wizara
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments