[wanabidii] Ili kufikia BRN, wanafunzi wafanya mtihani kiwanjani

Friday, May 16, 2014
Juzi katika shule ya msingi Majengo wilayani Kahama mkoani Shinyanga walikutwa wanafunzi wakiwa wameketi chini katika kiwanja cha shule hiyo wakifanya mitihani wa kufunga mhula wa kwanza.

Imeelezwa kuwa, licha ya kuwa shule hiyo kuwa na madawati ya kutosha, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo William Ngulu alisema kuwa hiyo ni mbinu ya kuwafanya wanafunzi wake wafanye mitihani kwa akili binafsi bila kuangaliziana.

Ngulu ameongeza kuwa mitihani hiyo hufanyika mida ya asubuhi tu wakati jua halijawa 
kali na hali hiyo inaleta mafanikio makubwa katika shule yake katika kufikia mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN) BIG RESULT NOW.

Mwl Ngulu amesema kuwa mbinu hiyo wameanza kuitumia toka mwaka 2013 na ndiyo siri ya mafanikio ya shule hiyo kuwa ya kwanza kiwilaya katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2013.

Naye mwenyekiti wa mtaa wa majengo ambaye ni mzazi katika shule hiyo Noel Mseveni amesema kuwa swala hilo si jema kwa kuwa ni kuwadhalilisha watoto na wazazi. Ameshauri wanafunzi hao wafanye mitihani kwa awamu mbili za asubuhi na jioni ili kuwapa fursa wote wafanye mitihani wakiwa wameketi kwenye madawati.

Afisa Elimu ya Msingi katika Halmashauri ya mji wa Kahama, Aluko Lukolela Aluko amesema kuwa mbinu hiyo ameianzisaha yeye alipohamia wilayani hapo na imeleta mafanikio makubwa katika kuinua elimu.

Sambamba na hayo Aluko amepinga mbinu mbadala iliyotolewa na Mwenyekiti wa mtaa huo na kusema kuwa mbinu hiyo itasababisha kuvujisha mitihani hiyo kwani wanafunzi watakaofanya asubuhi watakuwa na nafasi kubwa ya kuwaambia maswali wenzao watakaoingia jioni.

--- Habari kwa mujibu wa Kijukuu Blog

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments