[wanabidii] SERIKALI IANGALIE UDHALILISHAJI UNAOFANYWA NA CLOUDSTV KUPITIA KIPINDI CHA BIBI BOMBA

Thursday, May 22, 2014

Mimi sio mtazamaji mzuri wa Clouds TV kwa kuwa vipindi vyake vingi ni vya ovyo–havina mvuto wala mafundisho ya maana. Jana, kwa bahati mbaya, nilitazama kipindi cha 'BIBI BOMBA' kinachorushwa na TV hiyo. Nimehuzunishwa sana kuona jinsi bibi na mama zetu wanavyodhalilishwa hadharani. Bibi zetu huulizwa maswali ya kidhalilishaji.

Bibi mmoja aliulizwa kama aliwahi kula mboga inayoitwa 'Biology', akajibu 'ndiyo'. Hili ni swali linalohusu ufahamu na kwa wabibi wale ambao hawakwenda shule, hawajui biology ni nini. Si hivyo tu, hata wale walioishia la saba hawajui biology ni kitu gani. Kuwauliza mabibi swali kama hili ni kuwadhalilisha kitaaluma kwa kuwa tu hawakwenda shule.

Bibi mwingine aliombwa amtongoze kijana yule anayewauliza maswali hadi amkubali. Bibi akatekeleza agizo hilo laivu mbele ya skrini ya TV! Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu.

Kama kweli kinachofanyika katika kipindi kile ni kuwajali bibi wale kwa maana ya kuwapatia pesa wakishinda hebu wanaoendesha kipindi kile siku moja wawalete bibi zao na wawahoji maswali yale ya kishenzi tuone kama itakuwa sawa kwao, kwanini pesa iwe kigezo cha kudhalilisha watu wazima? Tena wanadhalilishwa na vijana wadogo wasio na chembe ya maadili? Hivi kweli kumwambia bibi mtu mzima amtongoze kijana mdogo halafu mbele ya skrini kila watu wa rika tofauti wanatazama wakiwemo watoto hapo tunafundisha maadili gani kwa jamii?

Wizara ya jinsia inapaswa kukataza udhalilishaji huu wa kijinsia. Nasi wananchi tuache kushabikia upumbavu huu–tukatae kuwapigia kura bibi wanaoshiriki

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments