WALIOHUDHURIA:
1. DR. WILBROAD SLAA Katibu Mkuu CHADEMA
2. Eng. MOSENA J. NYAMBABE Katibu Mkuu NCCR-Mageuzi
3. Ndg. HAMISI HASSAN Kaimu Katibu Mkuu CUF
4. Ndg. BENSON KIGAILA Mjumbe
5. Ndg. WILFRED RWAKATALE Mjumbe
6. Ndg. FAUSTINE SUNGURA Mjumbe
7. Ndg. HASSAN RUHWANYA Mjumbe
8. Ndg. ABDUL KAMBAYA Mjumbe
9. Ndg. ABDALLAH PAKU Mjumbe
10. Ndg. MARCOSSY ALBAINE Mjumbe
WASIOHUDHURIA:
1. Maalim SEIF SHARIFF HAMAD – Kwa taarifa
AJENDA:
Kimsingi kikao kilikuwa cha dharula na ajenda zilitegemewa kufikiwa kikaoni
AKIDI:
Kikao hakikuwa na akidi maalum kwa maana ya idadi ya wajumbe bali kilitegemea uwakilishi wa vyama vyote vitatu ambapo kimsingi uwakilishi huo ulitimia.
UFUNGUZI:
Kikao kilifunguliwa na Dr. Slaa akiwa kama mwenyeji na pia ikaamuliwa awe Mwenyekiti wa muda hadi pale ambapo wajumbe wataamua vinginevyo, ambapo pia alianza kwa kueleza lengo la kikao kuwa ni kujadili matukio yaliyotokea Bungeni Dodoma na umuhimu wa kuwa na platform nje ya Bunge ili kuwasaidia au kuongeza nguvu kwa wajumbe walioko Bungeni wanao unda UKAWA-Ndani.
Akasema uhalali wa kikao unatokana na consultations kutoka kwa viongozi wakuu wa Vyama vyetu, akadokeza kuwa upinzani Bungeni umekuwa na limitations kwa sababu ya kanuni za Bunge hilo na CCM wana jeshi kubwa ndani ya BMK. Na kuendelea kusema, lengo kubwa ni kwamba sisi vyama vitatu vilivyoanzia Jangwani japo tuna option ya kupanua wigo zaidi tuna mambo matatu ya msingi sana.
Jambo la kwanza, ni kwamba vyama vyote tuna hoja nzito toka zamani kwamba solution ya kero za muungano ni serikali tatu, vyama hivi vya siasa tumekuwa na msimamo mmoja.
Pili, ni kwamba kuna unafki ndani ya BMK, CCM wamekuwa wakitengeneza propaganda kuuchanganya umma.
Na jambo la tatu ni sisi tunafanya nini, kwa sababu;-
(i) Wao (CCM) wamemtumia Raisi kama M/Kiti wa chama chao cha siasa kuhutubia Bungeni, ukweli ni kuwa mambo haya yanachnganya maana kuna muda alianza kuongea kama Raisi baadae kama Mwenyekiti wa chama.
(ii) Wamefanikiwa kwani tulipokubaliana maridhiano tulikuwa tuna give in kila mara, wamerejesha kanuni 15 kinyemela wanataka kutuburuza hatuwezi kukubaliana
(iii) Wamechukua unyekiti wa kamati zote, kama kuna dhamira ya maridhiano wasingebeba zote, na nafasi zote 5 za uteuzi wamechukuwa zote isipokuwa ya Prof Lipumba na tunampongeza kwa kuikataa. Wapinzani tuliingia mtego kwa kumsifu Sitta kama candidate bora jambo ambalo si sawa. 6 amepewa maelekezo ya kulinda chama, pia kwa kumtumia Waziri mkuu CCM imeitisha mkutano na Wahariri wa Vyombo vyote vya Habari, serikali imeamua kuingilia kuingilia kati mchakato mzima hatuwezi kufumbia macho hili.
Siku kama tano nyuma Makamu wa Raisi kazindua msafara wa UVCCM wa bodaboda kufanya operation nchi nzima, tuamke, sasa basi tunataka kama vyama huku nje tumevumilia imetosha, tutapambane na tutoe tamko kuonya haya. TBC1 wanafanya kampeni kila siku wanaonesha viongozi wao wakitoa matamko mbalimbali, radio, magazeti vyote vina manipulate Watanzania, kwa mtindo huu kwenye kura za maoni tutapigwa.
(iv) Kuna mashinikizo dhidi ya Wabunge wa CCM ambao walikuwa na dhamira ya kuitetea Tanganyika, pia baadhi ya taasisi kama TGNP bado hawaelewi kinachotokea, tusipochukua hatua sasa tutalaumiwa na generation ijayo itatulaum, siasa ni game ya tusiwe nje ya muda, muda ukatuacha tukusanye nguvu zetu na resources urgently ili tuanze kupambana, Bungeni kuna UKAWA tuandae umoja wetu na sisi hapa nje. Wao ndani hawawezi kuratibu ya nje, wakifika point wanataka kuja nje wakute tumejipanga tusije tukakwama.
Tumekuwa tukipanga mikakati yetu kule Bungeni ina leak kwa kuanzia hapa nah ii framework tuanze kufanya thinking.
Akatoa updates ya kinachojiri Bungeni kwa muda ule tuko kwa kikao, pia akashauri kuwa Tume ya Warioba ina hasira na sisi kama Makatibu Wakuu tuangalie namna ambavyo tunaweza kuwashirikisha.
Naomba kuwasilisha.
MJADALA:
Benson Kigaila;- Nashukuru kwa sum up, huwezi kujadiliana na mwenye silaha bila kuwa na silaha atakuburuza, CCM tumewaachia muda sana kwa maana ya maridhiano, CCM hawako wengi kama wanavyosema wapo wengi Bungeni na sin je ya Bunge, napendekeza yafuatayo:-
(i) Tu network watu wasio kubaliana na hotuba ya Raisi
(ii) Tufanye mobilization ya watu ili kuwapa pressure CCM, then itajengea UKAWA wa ndani silaha tuta burgain sawa
(iii) Hatujaisema kwa kina hotuba ya Rais Kikwete kwa kuwaonesha Watanzania kwamba Raisi ame dishonest Rasimu ya Warioba.
(iv) Watanzania wajue tunachopigania ni nini
(v) Mawasiliano ya nje yasifanywe na Wabunge yafanywe na Viongozi wa vyama nje. Akatolea mfano wa Kabila kuonesha umuhim wa kuwa na silaha wakati wa majadiliano
(vi) Tufanye mikutano ya hadhara kuonesha kama tuna watu
Hamis Hassan;- Nashukuru kwa kuleta hoja hii, ipo haja ya kufanya tunachokusudia, tujiangalie sisi na tufanye analysis, Kikwete alirubuni baadhi ya taasisi, ila tuangalie tuna watu gani wanaotuunga mkono na tuwashirikishe vipi. Makundi yapo mengi labda yanaogopa, wanakosa pa kuanzia. Kuna haja ya Makatibu Wakuu tujue ipi ni impact ya bodaboda na tu pre empty mapema ili watu wajue mapema kinachofanyika ni propaganda.
Kuna taarifa zisizo rasmi za kuhesabu kura kwa kutumia mashine maalum za kuhesabu kura wakati wa referendum kupima kama zitafanikiwa kama Kenya, Zimbabwe etc, tuangalie namana ya kuunganisha na kushirikisha taasisi nyingine kwa kuanzia hapa Dar.
Wilfred Rwakatale;- Miminamini CCM siku zote si wakweli, kila hatua inayotokea haiji kwa bahati mbaya, wao wamedhamiria kupitisha katiba ya CCM na wanawatumia actors mbalimbali kama vijana ku bluff the public, wata ceaze system na mwisho katiba ya CCM itapatikana.
Napendekeza;
(i) Twende kwa speed kubwa mno kwa sababu wao they are on
(ii) Hatupaswi kuchelewa kama tunataka public ituelewe na tutumie combination zote kama vurugu uhuni ama la
(iii) Wao tuwaache wafanye vurugu ila wakute sisi tumekwishajipanga
(iv) Kwa kujipanga vyema inabidi big guns wa vyama vyetu lazima wawe front, tuanze na kundi kutoka kwa vigogo wa vyama vyetu ndio watoe go ahead.
(v) Tuunganishe bara na Zanzibar ili ionekane tuna mshikamano, Seif aje bara atoe neon ili tuwe na wimbo mmoja kati ya pande zote
(vi) Tusione aibu kucheza rafu, na iende sambamba na uboreshaji wa daftari kuelekea referendum. Wao wanatumia pesa kuwasafirisha watu wa pikipiki dawa ya moto ni moto wakipita wakute bodaboda pia zimeandaliwa katika mikoa husika
Kambaya;- Nataka kujuwa kama zinazotumika ni fedha za wafadhili, je hatuna namna ambayo tunaweza kufikia balozi na kuzieleza namna uhuni wa CCM unavyofanywa.
Dr. akajibu kuwa kuna mchezo hufanywa ambapo peas zile zimechanganywa na kuonekana kama si za wafadhili.
Rwakatale, akasema baadhi ya mabalozi wanakuwa linked na mfumo wa kifisadi ili kuwakata mdomo, ni vema kutumia caucus za mabalozi nchi za nje ili nchi zao ziweze kuwapa pressure.
Ikaazimiwa kutengeneza document proper itakayo circulate kwa mabalozi yote, mabalozi wengi hawana info ya kinachoendelea kwani hawasomi magazeti yetu wala hawahudhurii Bungeni, pia tuwaruke mabalozi ikiwezekana iende huko mbele, tufungue na tutumie avenues zote za kuleta pressure.
Mosena Nyambabe: Nakushukuru ndugu mwenyekiti pia na ndugu wajumbe niwashukuruni, pia kwa walionazisha wazo hili huko bungeni. Kwa kifupi tu ni kwamba mkutano tuliofanya jangwani na Zanzibar uliwafanya ao kukaa vikao takribani 43 kutafakari.
Napendekeza:
(i) Tuainishe mambo ya msingi yaliyo katika rasimu vitu ambavyo vitu ambavyo hatutaki viguswe kabisa tuvijue
(ii) Kuhusu suala la maridhiano viongozi wakuu wamwambie Kikwete tulikuabaliana kwa nia njema ila anakiuka makubaliano hivyo ategemee linaloweza kuja jitokeza
(iii) Tuangalie ni namna gani tunaweza kuelezea muungano vizuri ili wananchi waelewe na waujue.
(iv) Suala la katiba ya Zanzibar kuvunja katiba ya muungano tuangalie kama kuna loopholes wa viongozi kuweza kushitakiwa kwa kiongozi kuvunja katiba.
Michango mbalimbali ikatolewa mwisho ikaamuliwa kuwa Barua kwa Raisi iandikwe as a matter of formality
Marcossy Alabaine: Asasi za kiraia hazipo happy na mchakato unavyokwenda, asasi pia zimekuwa zikijiziwia kuwa zisionekane zipo affiliated na chama Fulani. Hapo awali tulikuwa tunawashambulia wanasiasa wote, baadae tukajuwa CCM ndio tatizo baadae tukagundua zaidi kuwa ni Raisi na kundi lake.
Wengi wa mabalozi walibanwa wasi support mchakato wa katiba kwa taasisi za kiraia, tulipofika ni kwamba taasisi zinaweza kusimama sasa, kwani zinaweza kuita taasisi nyingine zote na kutoa msimamo wao, nashauri kwa hoja hii tunahitaji wanaharakati ambapo wakizungumza wanaungwa mkono.
MAAZIMIO:
(i) Tumekuabaliana kufanya kazi pamoja
(ii) Muda ni huu
(iii) Tushirikishe network pana
(iv) Barua iandikwe as formality
(v) Analysis ya katiba ifanyike
(vi) Intelligence iundwe
(vii) Documents muhimu zianadaliwe
(viii) Tuunde technical committee
(ix) Kukusanya mashoga wote ili waunge mkono jitihada za ukawa
(x) Kukusanya wasagaji wote ili waunge mkono jitihada za ukawa
(xi) Waraka huu uwe wa siri sana ili CCM isitubomoe maana CCM wanajua mbinu nyingi sana za kujitetea
(xii) Atakaye kataa ushoga tutamuondoa kwenye ukawa
TECHNICAL COMMITTEE:
1. MARCOSSY ALBAINE
2. ABDUL KAMBAYA
3. HAMISI HASSAN
4. BENSON KIGAILA
5. JOHN MALLYA
6. HASSAN RYHWANYA
7. FAUSTINE SUNGURA
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments