[wanabidii] BARUA YANGU KWA KANISA LA MORAVIAN TANZANIA

Friday, May 23, 2014
mwanakondoo ameshinda......Ni matumaini yangu katika bwana wote mtakuwa mu buheri wa afya njema.

   Lengo la kuandika barua hii fupi ni kuwaombeni viongozi na watendaji kazi wa kanisa letu hili ufafanuzi na hatma ya haya yanayotokea sasa katika makanisa mbalimbali ya Moravian Tanzania.

   Sina haja sana ya kurejea na kuyaanika yote hapa yaliyowahi kutokea hapo nyuma bali nitafanya kutolea mfano wa moja tu tuliloliona hapo jana kwenye vyombo vya habari uhusiana na kanisa letu huko kinondoni.Ni dhahili kanisa hili limejijengea heshima kubwa sana tangu zamani enzi za maaskofu,Kisanji,Jongo,Mwakasyuka na wengine wote,sasa haya yanayo tokea ni nini hasa chanzo chake? pili ninini hatima yake kama sio kuliweka kanisa katika hali ya kumkaribisha ibilisi ambaye tangu tukiwa watoto tumefunzwa kumkana kwa akili na vinywa vyetu.

      Kuna wakati nafika mbali kidogo na kujiuliza hivi ni maslahi gani yaliyonyuma ya ugomvi huu? pili ni ibilisi gani huyu aliyeko nyuma ya ugomvi huu ambaye hatoki hata kwa kemewa na viongozi wetu ambao kimsingi ndio vichwa vya kanisa? tatu nafikia hata hatua ya kuwakumbuka wazee wetu waliowahi kuongoza kanisa hili kama mzee Jongo,na wengine kana kwamba je hata enzi zao kulikuwa na haya? kama ndio je nao walichukua muda mrefu kuyatatua kama ilivo sasa? Hapa nieleweke kuwa sina tatizo na viongozi hata kidogo bali tatizo langu ni kwann uongozi unaendelea kuyaangalia haya licha ya kuwa kuna taarifa za kusuruhishwa ugomvi huu ulowahi kutokea hapo nyuma.

    Nina mengi sana ya kuyajua na kuyasema kwa kanisa langu hili ila kwa sasa naomba niishie hapa nikiwaomba viongozi wangu watiifu waingilie kati mgogoro huu na watoe maamuzi sahihi yenye kumpendeza Mungu kwa maslahi ya sisi waumini wake,pili nakemea hila zote zote za ibilisi mwenye maslah katika ugomvi huu na kuwaomba waumini wote kuwa macho na kuzidisha maombi.natoa pole kwa yeyote aliyeathirika na ugomvi huu nikumwomba mwenyezi mungu asimame katikati yetu na amalize haya ili kanisa liendelee kusimama imara.Mwana kondoo ameshinda...........
                           wenu katika bwana

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments