Hawa wanaotokana na majimbo ya uchaguzi nilidhani ni wawakilishi wetu kumbe nilikuwa nakosea si wawakilishi wetu. Maana kama wangekuwa wawakilishi wetu wangekuja kutuuuliza majimboni kama kweli alichoandika WARIOBA ndicho tulichomtuma. WARIOBA alitufuata kutuuliza tunachotaka akakiandika lakini kuna watu wamejipa mamlaka ya kutusemea sisi kwa wenyewe hatujui kujisemea tunalolitaka. Wapo wabunge wengi toka majimboni ambao 2010 walipita kwa kishindo kama wanavyopenda kusema lakini kwa sasa hatakiwi tena na hata majimboni kwao hawapiti hawa wanakuwaje wawakilishi wetu.
WARIOBA amekosea kwa vile ameandika mawazo ya wananchi wakati alitakiwa aandike mawazo ya chama chake kiyukufu.
Waliotoka bungeni wamekosea sana na waliobaki wamekosea vilevile kwa kuwa mjadala ulishafungwa kwa hotuba ya Rais, maana kwa kinywa chake alisema hataki serikali tatu na kama zitapita basi si wakati wake labda baada ya yeye kumaliza muda wake. Sasa hawa waliobaki wanajadiliana nini, kubariki maneno ya rais au kungojea posho maana mjadala umefungwa.
Warudi majimboni watuulize cha kusema kwa niaba yetu kama kweli hawakai pale kwa ajili ya posho. Nilidhani baada ya wapinzani wao kuondoka wangeendelea kujadiliana hoja za msingi lakini mipasho kwa wasiokuwapo inaendelea, ni ya nini wakati hawapo?
Hawa wote ni wezi wa fedha za umma kwa vile kinachotakiwa kimeshatamkwa na mkuu wa nchi. Nchi hii ni shamba la bibi, tume imetumia pesa zetu wamekwenda na mamilioni, bunge maalumu wanachukua zingine na katiba waliyoipendekeza wananchi haitakiwi pesa zinaendelea kuliwa na sisi tunashabikia tu bila kuhoji. Huu ni uzalendo unaohubiriwa hapa kwetu Tanganyika, Wazanzibari wasingekubali upuuzi huu
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments