[wanabidii] PANYA WENGI HAWASHIMBI SHIMO - KATIBA

Thursday, April 10, 2014
Msemo wa hakima wa zamani,  "PANYA WENGI HAWACHIMBI SHIMO" ni msemo wa unaoweza kusemwa bila kutiliwa maanani. Nilijifunza nikiwa shule ya msingi. Hakika sikuelewa maana yake. Ni sasa nikiwa karibu na nusu umri wa nusu karne ndiyo natambua maana yake na hata kuona mfano halisi wa usemi huu. Mfano halisi ni Bunge letu maalum la Katiba.

Nimegundua watu 600 na zaidi kidogo hawafai na wala hawahitajiki kutunga katiba. Maoni ya wananchi yalikwisha patikana. Na Kilichotakiwa ni wataalamu wachache, wanasheria, wasomi wa uchumi na mambo ya kijamii kukutana na kuchuja na kuandika Katiba mpya. Kilichojiri mpaka sasa ni mabishano yasiyokuwa na msingi na hata kutusiana na hata kuwadhalilisha waasisi wa Taifa letu hayati Mwalimu Nyerere na hayati Karume kuwa walikuwa waongo katika suala zima la Muungano. Hakika tunakuwa watu wasiokuwa na shukrani kwa wazee hawa maarufu.

Katika hili sasa nisema tu Kuandika KATIBA mpya, wajumbe walioko ni wengi mno. Kwanza hata uelewa wao wa mambo umepishana mno. Kuna ambao mpaka mwisho hawataweza kuchangia chochote maana hawajui mbele wala nyumba. (niombe radhi kwa usemi huu) Lakini ndio ukweli. 

Napendekeza hivi, Bunge hili maalum la katiba LIVUNJWE ili tusiendelee kupata hasara ya Billioni za hela. Tuna shida nyingi, kama vile kutibu wazee au kununua madawa Hospitalini au chemikali za kwenye maabara za shule zetu. Na juu ya yote tukuballiene na usemi kuwa PANYA WENGI HAWACHIMBI SHIMO likamalizika.

Kama wabisha toa hoja zako! 

kessy

Share this :

Related Posts

0 Comments