[wanabidii] ndugu Lukuvi ana matatizo gani? Angalia attachment

Thursday, April 17, 2014
Wanabidii.
Nimemuona ndugu Lukuvi katika taarifa ya habari ITV saa mbili leo akijaribu kujibu hoja kuhusiana na tamko lake kuwa Jeshi litaipindua serikali kama tutaunda mfumo wa serikali tatu.

Bila kufuatia neno kwa neno nimemsikia akisema kuwa rasimu ya pili ya tume ya katiba imetoa vyanzo vya mapato visivyojitosheleza kwa hiyo kitakachoweza kutokea ni Jeshi 'KUAMUA'

Yeye anaamini kuwa hakuna njia au pendekezo kuboresha hapo, ila ni kuwa tuachane na mfumo huo maana jeshi linaweza kupindua nchi.

Simuelewi kwa hiyo nafikiri ana matatizo labda akidhibitisha kinyume.

Kwa mawazo yangu pendekezo la mapato kutojitosheleza jibu lake ni kupendekeza njia nyingine ya kuongeza mapato.
lakini kwa mawazo mengine sioni kwa nini asione kuwa serikali itashindwa kuunda baraza la mawaziri 50 badala yake watakuwa 12 hivyo serikali itakuwa ndogo na kwa hiyo mapato yatatosha.

Lakini tatizo kubwa katika usemi wake ni kusema maneno ya kulichochea jeshi. Hivi ni sahihi kwa kiongozi wa ngazi yake kusema neno kama hilo. kiongozi wa serikali iliyomfungulia Kibamba kesi kwa kusema neno dogo kuliko alilosema Lukuvi?

Kwa nini asiseme wafanyakazi wa serikali kuu watakosa mishahara? kwa nini asiseme Rais atapunguza safari kufikia mara mbili ya safari alizosafiri Nyerere katika miaka 24 aliyokaa Ikulu.

Mahala pengine alipobolonga ndugu yangu ni kusema CUF na CHADEMA 'wameishagawana' nchi. CUF 'wamepewa' Zanzibar na CHADEMA 'wamegawiwa' tanganyika na CCM imebakiziwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Kwa nini kama CCM haiitaki isiache kugombea? Hivi serikali hizi zinagawiwa hivyo? mwenye uwezo wa kugawa serikali hizi ni nani kati ya CUF, CHADEMA na CCM?
Mimi sikumuelewa. Humu niliwahi kumtaja Lukuvi kama mtu mtaratibu anayeweza kuongoza nchi hii kama Rais. Nilikuwa nimekosea sana.
Wananchi wa Tanzania wanataka katiba. Tunaamini wananchi hawategemei kupewa (kama ambavyo Martin Luther King anasema katika kiambatanisho hicho) lakini sitegemei CCM iwapelekee watanzania kudai katiba kama wanaMsumbiji walivyofanya kwa msaada wa Tanzania na CCm yenyewe. hapana. Waturuhusu kistaarabu kupata katiba tuitakayo Tunataka katiba kama tulivyoieleza Tume na namini majeshi yetu yataitumikia katiba hiyo.

Elisa Muhingo

Share this :

Related Posts

0 Comments