[wanabidii] WAZEE NA WASTAAFU WANAPASWA KUANGALIWA

Tuesday, March 25, 2014
Ndugu zangu ,

Leo katika harakati zangu za kutafuta gazeti Fulani nilikutana na kitu ambacho si cha kawaida katika maisha yangu , ilibidi nirudi nyuma niangalie picha yake vizuri nikadhibitisha ni yeye .

Nilikutana na Waziri wa Zamani Stendi ya Mabasi makubwa ubungo , amekaa pembeni ya muuza magazeti anapigwa na vumbi linalotoka barabarani na jua kali la maeneo hayo jumlisha na kelele za magari na wapiti kwa miguu kule nje .

Huyu ni waziri tena aliyekuwa kwenye wizara nyeti tu na wakati wa kupokea uwaziri wake aliapa kulinda siri za nchi , za baraza la mawaziri pamoja na nyingine za majukumu yake ya kila siku .

Alikuwa waziri wakati wa kipindi cha Benjamin Mkapa .

Nilijiuliza maswali mengi , hivi mzee kama huyu aliyepanda cheo kuwa mbunge mpaka waziri kamili amekosea nini nchi hii , amekosea nini chama chake cha CCM mpaka kuwa kwenye hali ile ? Mbona nilisikia kuna baraza la wazee huko CCM , vipi hawa tunaokutana nao mtaani ?

Hii ni aibu kwa chama kilichomlea yaani CCM , serikali ya Tanzania na watanzania wote kwa ujumla kwa kushinda kupanga maisha yajayo kwa wazee na wastaafu wengi wanaoendelea kuishi maisha ya tabu na ya shida kama haya pamoja na kutumika kwa miaka mingi .

Wabunge wa bunge la katiba waangalie na suala hili la wazee na wastaafu liwe vizuri kwenye katiba ili tuweze kuokoa wazee wetu wengi pamoja na wastaafu siku zijazo .


--

Yona Fares Maro

Institut d'études de sécurité - SA


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments