[Mabadiliko] CHADEMA NDIYO WAKUNIOMBA MSAMAHA-ZITTO

Friday, December 12, 2014

Katika mahojiano na RAI. Hii ikiwaachia aibu walioshindwa kuelewa alichosema Zitto siku chache zilizopita.pamoja nao ni Shigela, Godfrey Kundi, Dello nk wa mabadiliko.

Gazeti la RAI lilifanya
mahojiano maalumu na Zitto
ili kueleza changamoto
anazokumbana nazo jimboni
kwake pamoja na masuala
mbalimbali yanayohusu mustakabali wake kisiasa
pamoja na hali ya kisiasa
nchini, pamoja na mambo
mengine Mwandishi wa RAI
alimuuliza,
RAI: Hivi karibuni Profesa Abdalah Safari ameteuliwa
kuwa Makamu Mwenyekiti wa
Chadema, pia alizungumzia
kutokuwapo kwako ndani ya
chama hicho hakuna
kilichoharibika, je unamzungumziaje? ZITTO: Nimesikitishwa sana na maneno ya Profesa Safari
naomba aweke akiba ya
maneno yake, asiongee sana
atakuja kuyameza hayo
maneno baadaye, yeye siyo wa
kwanza kushika nafasi hiyo aliyo nayo.
RAI: Lakini pia Profesa Safari amesema iwapo utakuwa
tayari kuomba radhi wao wako
tayari kumaliza tofauti, je
utakuwa tayari kwa hilo? ZITTO: Nikiomba radhi watanisamehe!! Mimi sina kosa
wao ndio wanapaswa
kuniomba radhi, sio mimi
kuwaomba wao radhi, sina
kosa hata moja, hakuna
tuhuma yoyote ndani ya Chadema ambayo mtu
anaweza kudhibitisha.
RAI: Unazunguziaje misukosuko uliyopitia kisiasa? ZITTO: Katika hali ya kawaida kama nisingekuwa imara
ningeanguka, naamini wengi
walitegemea ningeanguka,
lakini niko imara zaidi ya
nilivyokuwa awali.
Wanashangaa mimi bado nafanya kazi zangu, nina kazi
nyingi za kufanya, sijali nini
wanachokifanya, juhudi zozote
wanazozifanya kwa ajili ya
kunishughulikia
katika jimbo langu au katika mkoa wangu watashindwa,
naaimini nimeingia kwenye
mioyo ya watu wa Kigoma,
kwa sababu mimi ni alama
yao, hivyo
wanajifurahisha.Mimi kuna kazi nafanya, siwezi
kuhangaika na watu
wasiokuwa na kazi za kufanya,
wasiokuwa na kazi ya kufanya
wao ndiyo wanadili na Zitto,
mimi hiyo siyo aina yangu ya siasa, nafanya mambo mazito
kwenye siasa.Kamati ya Bunge
imenipa kazi kubwa ya
kufanya, nalitumikia taifa,
tayari tumeshaliita Jeshi lije
kueleza matumizi na mapato yao, hili ni jambo zito ambalo
halijawahi kufanyika, kama
ilivyo kwa polisi na Usalama wa
Taifa.
Extract ya mahojiano
itaendelea...

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CACMr6Qg2uRKnj%2BMZxQgMaHkJrm-UFmQMNF3iRLrjcfwv3mwzfA%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments