Vijana Njooni CCM,
Miongoni mwa sifa ambazo Chama Cha Mapinduzi kimejipambanua nazo katika Nyanja za kimataifa na kitaifa ni pamoja na utaratibu na mfumo bora wa uendeshwaji wake, kwamba ni Chama kilicho kamili katika muundo wake, misingi yake, kanuni na taratibu zake. Lakini pamoja na hayo CCM inayo historia iliyotukuka si tu ya kuikomboa TANZANIA kutoka katika mikono ya wakoloni lakini pia kusaidia mataifa mengine ya kusini mwa jangwa la Sahara.
Chama Cha Mapinduzi, pamoja na mambo mengine bora, kimetimia vyema katika muundo wake kwa kuwepo kwa jumuiya imara zinazoishikilia na kuipa nguvu kila Uchao. Ipo jumuiya ya Vijana ambayo lengo kuu la Kuundwa kwake ni kuhakikisha kuwa Chama na Taifa linaandaa na kulea Viongozi wake wa kesho. Ni chama cha Mapinduzi pekee miongoni mwa vyama vyetu vya siasa hapa nchini ambacho kina "Sera ya malezi ya Vijana" iliyotungwa tangu 1981 na kuendelea kufanyiwa review mpaka sasa.
Vijana ndani ya Chama Cha Mapinduzi wanamatumaini Zaidi na wanaandaliwa na kusafishiwa njia ya mafanikio yao kwa mapenzi na weledi wa Viongozi. Tabia hii ya viongozi wa CCM kuwaandaa Vijana makini na kuwatengezea mazingira kwa kuwalea na kuwadhibiti katika matendo na mienendo ndio ambayo inakihakikishia Chama hiki Uhai wa miaka mingine 50 na hata Dahari. Ni wazi leo ukiwaangalia Vijana ndani ya CCM unaona picha ya Viongozi bora wa kitaifa wa Miaka 20 ijayo, ukiomuona JANUARY, NAPE, JERRY, n.k unaona picha ya Viongozi bora wa baadae tofauti na ukiangalia wenzetu SUGU, LEMA., NASSAR etc unaona kiza na wingu zitto.
Tofauti na vyama vingine, CCM ukiwa kijana una-reside your right of trial and error, kwa maana tumeshuhudia Vijana wengi ambao walikosea lakini wanapewa nafasi na kuwa Viongozi wakubwa na wazuri baadae, mifano hii iko mingi, binafsi nimewahi kufanya makosa lakini niliitwa na kuonyeshwa njia, na nilifanyiwa hayo sio kwa sababu mimi ni msukuma ama ------, kwa sababu kwenye Chama Chetu Usukuma ama ukwere sio sifa ya kuwa kiongozi kwa maana sikuangaliwa kabila langu ili niadhibiwe ama nisamehewe. KABILA halimbebi mtu ndani ya CCM.
Ipo siku niliitwa na Mzee wangu KINGUNGE NGOMBALI na akawa ananifundisha darasa la ITIKADI, tukaendelea na mjadala nikamuuliza ameweza vipi kuwa kiongozi mkubwa na mwenye heshima ya kipekee ndani ya Chama hali yeye haamini katika DINI yeyote.,akanijibu kwa ufupi na ufasaha kuwa DINI ya mtu sio sifa ya kuwa KIONGOZI ndani ya CCM. Kwenye CCM kila kijana na kila kiongozi ana sifa sawa na wengine, hakuna aliye mbora mbele ya wenzake, vipo vigezo vinavyotumika kumpata kiongozi, sio lazima uwe PADRI ama MCHUNGAJI ndio uonekane unafaa kuwa kiongozi ndani ya Chama, kwetu sisi DINI ya mwanachama sio sifa ya kuwa bora kwa wengine.
Nitoe wito kwa Vijana wenzangu kuuona ukweli huu na kuufuata, ufike wakati Vijana wajiandae na waandaliwe kuwa Viongozi Bora wa Kizazi Chao. Njooni CCM ambako ndoto zenu zitatimia, michango, uwezo na mawazo yenu itathaminiwa. Njooni ambako mtaonyeshwa njia ambayo mtakuwa tayari kuifata.
MWENYEZI MUNGU AWABARIKI NA AWAONGOZE KATIKA NJIA YA SAWASAWA.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
Vivaa Vijana Vivaaa…!!!
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments