[wanabidii] UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA PUMA ENERGY (T) LTD NA WAKURUGENZI WA BODI

Friday, March 14, 2014
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA YA UMMA

UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA PUMA ENERGY (T) LTD NA WAKURUGENZI WA BODI
 
Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amemteua Dkt. Ben E. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya PUMA Energy (zamani ilijulikana kama BP Ltd). Uteuzi huo wa Dkt. Ben Moshi ni wa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 1 Machi, 2014.
 
Kutokana na uteuzi huo Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter M. Muhongo (Mb.) 
amewateua wafuatao, kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya PUMA Energy (T) Ltd kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 1 Machi, 2014:
Mhandisi Dkt. Malima MP. Bundara, Mwenyekiti Mtendaji wa Kituo cha GARETRACE;

Bw. Solomon R.M. Odunga; Katibu Mkuu Mstaafu;
Bw. James Andilile, Kamishna Msaidizi wa Nishati katika Wizara ya Nishati na Madini; na
Bw. Daniel N. Nsanzugwanko, Mtaalam Mshauri wa masuala ya biashara.

Imetolewa na
KATIBU MKUU

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments