[wanabidii] UFAFANUZI WA CHADEMA KUHUSU CHOPA 3 KATA 3

Friday, March 07, 2014
Kumekuwa na vijembe vya hapa na pale kuituhumu CHADEMA kuwa imetumia nguvu nyingi sana katika kampeni kwa kutumia helkopta 3 na kisha kuambulia ushindi katika kata 3 tu, na kwamba ushindi huo haulingani na nguvu iliyotumika.


CHAMA KINATOA UFAFANUZI.
1. Chama kilianzisha zoezi lililojulikana kama M4C- Operationi Pamoja daima(M4C-OPD), katika zoezi hili chama kilifanya mikutano zaidi ya 360 karibu inchi nzima sehemu palipokuwa na uchaguzi na sehemu nyingi palikuwa hapana uchaguzi wowote. Lengo la operationi hiyo lilikuwa ni kutoa elimu ya uraia ambayo raia wengi wanaikosa na kwamba elimu kama hii huwa haitolewi na chama tawala kwa makusudi kudhihirisha ule usemi wa Kiswahili unaosema USIMWAMUSHE ALIYELALA UKIMWAMSHA UTALALA WEWE.


Kikubwa katika zoezi hilo ilikuwa kutoa elimu ya uraia kuhusu mchakato mzima wa kuandika katiba mpya na ni nini wajibu wa raia kuhusu zoezi hilo kikubwa kilichoongelewa ni:
a. Hali zoofu ya muungano baada ya Zanzibar kuandika katiba yao ambayo imepelekea muungano kudhoofu sana umekuwa muungano jina tu.
b. Chama tawala CCM kuteka nyara mamlaka ya tume maalumu ya rais iliyokuwa inakusanya maoni toka kwa raia ilimaarufu tume ya Jaji Warioba, operationi hiyo ya CHADEMA ilikuwa inawafungua macho wanainchi waone jinsi chama tawala kinavyojitahidi kuingilia mchakato huo kwa manufaa ya wachache badala ya manufaa ya taifa zima na vizazi vyake.
c. Sehemu kulikokuwa na uchaguzi wa madiwami CHADEMA ilifanya kampeni pamoja na kutoa elimu hii ya uraia, nafikiri wanainchi wanajionea wenyewe sasa uhuni unaoendelea kenye bunge maalumu la katiba unaoasisiwa na chama tawala mwenye macho haimbiwi tazama.


Matokeo ya uchaguzi wa katika kata 27 uofanyika tarehe 8 February



Chama cha CHADEMA kiliibuka na ushindi mnono kuliko Lumumba wanavyofiria hadi kuitisha kikao na waandishi wa habari eti kuwashukuru wanainchi kwa kuendelea kuwaamini mkutano ulioitishwa na domo kaya wao Nape Nnawiye. Siyo kweli eti CCM Ilishinda uchaguzi huo ukweli ni kwamba CCM ilishindwa vibaya kwa sababu za kisayansi zifuatazo;


a. Katika sehemu CCM ilikoshinda kata za vijijini wanainchi wake hawajitambui, hawajui kinachoendelea pembeni yao, hawana habari , wanafichwa , hawaelimishwi, hawajui hata matukio, mfano tuliwauliza ni wapi mwenyekiti wa CCM alipigwa na mawe na wanainchi wenye hasira , alipigwa kama mwizi hadi akafa? Hawajui. Pia tuliwauliza ni mbunge gani wa CCM anatuhumiwa kubaka na kumwambukiza mtoto wa shule UKIMWI? Hawajui. Sasa ukishinda uchaguzi maeneo ya watu kama hao na wewe utajihesabu umeshinda?
b. Katika sehemu CHADEMA ilikoshinda zile kata tatu yaani Sombetini Arusha , Kiborloni Moshi na Njombe mjini kata hizi wanaichi wake wanajitambua kata hizi thamani yake ni Dhahabu na ninafikiri wana bodi mnafahamu kwamba katika mashindano ya Olympic inchi moja ikishinda medali za dhahabu 3 na ingini ishinde medali za fedha 200 kama CCM ilivyofanya basi ile iliyoshinda dhahabu inakuwa juu sasa leo iweje CCM itake kudai ushindi katika uchaguzi huo wakati iliambulia medali za fedha tu ? Shame on them.


Hitimisho



Chama cha CHADEMA kinajivunia na kitaendelea kujivunia mafanikio kiliyopata katika zoezi la M4C-OUD kwani kimesambaza elimu ya uraia , wanainchi wanaendelea kufunguka macho na sasa wanajionea wenyewe uhuni unaofanyiaka katika bunge maalumu la katiba na ni wazi kwa wale wote wanaojitambua wanajua uhuni huo sababu yake ni nini. Pili kilipata ushindi mnono na kunyakua medali zote 3 za dhahabu katika uchaguzi wa madiwani uliopita, CCM iliambulia fedha na shaba tu, hebu waje hapa akina Nape na Ngulu Mchemba wakanushe hili.


Aksanteni

Toka kurugenzi ya habari ya CHADEMA
Leo hii 7/3/2014.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments