[wanabidii] Muungano wa Tanzania: UNA UFA WA KUFA

Sunday, March 23, 2014
Muungano wa Tanzania: UNA UFA WA KUFA
Kama kuna kitu watanzania tunaweza kujivunia ni Muungano. Muungano ambao tunastahili kuuonea fahari vizazi na vizazi. Muungano ambao tunastahili kuulinda kwa garama yoyote ile. Muungano ambao mtu akionekana kuusaliti kila mwenye akili anamshambulia.
 Tunaposema Tanganyika tunasema nchi ambayo mipaka yake ilitengenezwa na wakoloni kwa faida yao. Tunaposema Zanzibar tunamaanisha nchi ambayo mipaka yake iliandaliwa na wakoloni kwa manufaa yao. Hatukuamua mipaka hiyo. Huenda mimi mtu wa Bukoba ningeulizwa ningeamua kuwa sehemu ya Burundi au Uganda au vyovyote.
Ukisema Tanzania una maana nchi ambayo mipaka yake imetengenezwa na sisi wenyewe (kwa maana uamuzi ulifanywa na viongozi tuliowachagua).
Ni uzetete na umbumbumbu kufanya jambo lolote linaloweza kudhoofisha au kuua Muungano huu sasa au baadaye.
Enzi hizo waasisi wa Muungano walifikiri sana na kuamua kuunda muungano wa serikali mbili wakiwa na matumaini kuwa Utanganyika ukifa baadaye uzanzibari utakufa basi itakuwa nchi moja yenye serikali moja. Ndiyo ilikuwa sababu ya kuwa na serikali mbili. Hii ya Zanzibar ilikuwa serikali dhaifu inayoratibu mambo madogo ambayo yalikuwa hayakuingizwa katika muungano.
 Ili kuimalisha muungano viongozi wetu waliunganisha vyama vilivyokuwa vinatawala wakati huo yaani Afro Shirazi Party (Zanzibar) na Tanganyika African National Union (Tanzania Bara). Kabla ya vyama hivi kuungana wakati huo vyama vimeshika Hatamu maamuzi ya serikali yanaposubiri chama kuamua ilibidi vikao vya ASP na TANU vikae. Wakati huo ilikuwa rahisi kufanya uchochezi kwa kushawishi chama tuseme cha ASP kukataa jambo na ikaleta shida (japo haikuwahi kutokea). Sio jambo tamu kusema lakini moja kati ya faida ya kuunganisha vyama ni pale 'Hali ya hewa ilipochafuka kule Zanzibar' na ikapelekea Halmashauri kuu ya CCM kumuondoa madarakani Rais Aboud Jumbe. Ingekuwa vyama vilikuwa havijaungana ingeleta shida kufikia uamuzi mgumu kama huo.
Sasa yapata miaka tunasema Muungano una kero. Niliwahi kuandika makala zamani kidogo ambamo nilisema ''Tushughulikie kero za muungano ili muungano wenyewe usije ukawa kero''.
Hizi kero zimekosa dawa na mimi naweza kusema sababu kubwa ni udhaifu wa viongozi wetu. Wanapenda kuheshimiana badala ya kuheshimu taratibu. Kuheshimiana huku kumeendelea na kusababusha nyufa katika muungano wetu nyufa ambazo mtu mmoja ambaye sipendi kumtaja aliwahi kuandika kuwa Muungano una NYUFA ZA KUFA.
Yako mambo mengi ambayo nitayataja machache kuonyesha udhaifu wa ajabu katika muungano wetu. Ni mambo hayo ambayo kwa sababu ya kuyafumbia macho sasa yametufikisha mahala tunajidai ni kawaida lakini ni dalili za uharibifu, na uharibifu unaotupeleka kuuua muungano na si ajabu tukaanza kulaumiana huko na waharibifu ndio watakaolaumu, (kwanza wana majukwaa na wanasikilizwa.
Naanza na hili:
Majuzi wakati Kamati ya kuratibu maoni na kuandika katiba ilipokuwa inakabidhi rasimu ya katiba ilikabidhi kwa ''Marais'' wetu wawili. Tanzania ina marais wangapi? Wawili kweli? Jamhuri ya Muungano inaongozwa na Marais wawili? Kwa Katiba gani iliyopo inayoelekeza hilo.
Pili:
Ili kujadili katiba wajumbe wa Bunge la katiba wanatokana na a) Wabunge wa Bunge la jamhuri ya Muungano (yaani wabunge wa Tanganyika na Zanzibar); b) wajumbe wa baraza la wawakilishi kutoka Zanzibar; c) Wajumbe 201 walioteuliwa na Rais ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano akitaka kuwateua awe ameshauriwa na Rais wa Zanzibar. Sio baraza la Mawaziri ambalo ndani yake Zanzibar imewkilishwa. Baraza la wawakilishi limo bungeni nalo ni baraza kamili la Zanzibar. Linajadili katiba ya Jamhuri ya Muungano na lilijadili katiba ya Zanzibar bila ya Bunge la jamhuri ya Muungano kuhusika kana kwamba katiba ya Zanzibar haina uhusiano na jamhuri ya Muungano. Bunge la katiba linaloendelea halina mamlaka ya kujadili katiba ya Zanzibar hata pale ambapo katiba hiyo ina athali kwa katiba ya Muungano. Huu ni umbumbumbu ambao sikumbuki kukutanoa nao popote katika siasa za ulimwengu na kuwa na matokeo mazuri
Tatu:
Tanzania imeishi sasa miaka kadhaa (toka Zanzibar imepitisha katiba yake) na inaishi na Katiba mbili zinazopingana. Na viongozi wetu au kwa kuogopana au kwa 'kuheshimiana', kama ni kuheshimiana kweli wanaweza kwendelea na kutokea mbele ya wananchi wala huoni hata mkoja anasumbuliwa na jambo hili. Halisumbui kiasi kwamba watu tunaliongea wala hakuna anayekuja mbele na kuliongelea.
Viongozi wetu wanasimama na kusherekea uhai na muungano kana kwamba upo kumbe ulimeguka zamani na umeshikiliwa na gundi ya maji (kuogopana). Kama ni ufa huu ni wa kufa.

Mwalimu wangu Fulani aliwahi kuniambia kuwa 'If you don't in your finger, you will put in your head'. Tume ya mabadiliko ya katiba imeliona hilo na kulifanyia utafiti wa kutosha na kuja na mapendekezo ambayo sio matakatifu sana lakini hata bwege anaona kuwa yanalenga kuondoa kero na nyufa hizi zinazotishia uhai wa Muungano. Tume inabezwa na wanaoibeza wala hawaongelei nini kifanyika ile nyufa hizi zitoke hasha. Wanakataa dawa na kuileta yao bila kuelezea hii dawa inatibu nini. Wengine ugonjwa wameuleta wao au wameuona ukija wanacheka tu.

 Mchungaji Chiristopher Mtikila alipoanza kuongea habari za Tanganyika watu wengi walimuona kichaa au bwege fulani. Wenye akili waliliona kuwa huyu anasema kweli. Sasa Swala la Tanganyika si swala la mtu aliyefirisika kwa walio na wapangaji vichwani wala sio swala la either or. Ni swala la when and how. Kwa mtu anayejua kusoma alama za nyakati atajibu ''Now and under our supervision''. Kama swala hili halitashughulikiwa sasa ndani ya katiba hii na kwa makusudi ya kuulinda muungano huenda muungano utakuwa umekufa tunapozindua katiba hii ila harufu itategemea kuanza kusikia.

Muungano si wa wanasiasa. Ni wa Watanzania. Najisikia vibaya kuona wanasiasa wanauua nasi tunaangalia. Tatizo ni kila utakapoanza kuushughulikia lazima upitie siasa au utumie wanasiasa, vinginevyo nje ya hapo sioni, labda nguvu ya Umma? Tufanyeje kuunusuru. Enzi za Mwalimu tungemwambia Rais
Elisa Muhingo

Share this :

Related Posts

0 Comments